Nilikuwa naangalia taarifa ya habari na nikasikitishwa na takwimu juu ya hali ya kisukari na magonjwa ya moyo yanavyowaathiri watu nchini Tanzania. Takwimu zinaonesha kuwa 26% ya watanzania wote wameathirika na kisukari na magonjwa ya moyo peke yake.
Shirika la Afya Duniani (WHO) wana takwimu zinazolingana na hizi. Kutokana na takwimu za WHO kwa Tanzania,vifo vinavyotokana na kisukari ni 2%, na magonywa ya moyo 9% wakati magonjwa mengine yasiyoambukiza ni 13%.
Ina maana 31% ya vifo vyote Tanzania vinasababishwa na magonjwa yasiyoambuzika kwa jina jingine ni magonjwa ya mitindo ya maisha au “magonjwa ya kujitakia”
Hii ni hatari kubwa ambayo inanisukuma kuijadili hapa kujua nini chanzo na namna rahisi kabisa za kujiepusha na magonjwa haya mawili makubwa katika jamii yetu.
Magonjwa haya yanatokana na mitindo ya maisha. Maana yake yanasababishwa na jinsi tunavyoishi-vyakula tunavyokula, namna tunavyokula na misongo ya mawazo inayotokana na kazi na familia.
Japo magonjwa haya yamekuwa yakiwaathiri wengi hasa katika umri mkubwa lakini kama hatua stahiki zikichukuliwa inawezekana sana kupunguza idadi ya waathirika.
1. Kisukari
Kisukari ni ugonjwa unaosababishwa na upungufu wa kongosho kushindwa kutengeneza kemikali ya insulini ambayo ni muhimu katika umenge’enyaji wa sukari aina ya glukozi (Kisukari Daraja I) au mwili unaposhindwa kumenge’nya sukari hiyo hata kama insulini ikiwepo (Kisukari Daraja II). Zoezi hili linaposhindwa kufanyika sawasawa linasababisha sukari nyingi kubaki katika damu na nyingine kuingia katika mkojo.
Vyanzo vya Kisukari:
- Uzito wa wa kupita kiasi na kutofanya kazi za kutumia nguvu
- Umri mkubwa(zaidi ya miaka 45)
- Utumiaji kwa wingi kwa baadhi ya madawa ya tiba
- Shinikizo la damu
- Unywaji wa pombe kupita kiasi
- Kula vyakula vyenye mafuta
- Vyakula vya nafaka zisizokobolewa
- Kutoka katika familia zenye tatizo la kisukari
Mbinu za Kuzuia Kisukari
- Kupunguza msongo wa mawazo
- Kuwa na uzito unaofaa na kufanya kazi zenye kutumia nguvu au mazoezi
- Kupunguza matumizi ya madawa
- Kutumia chumvi na sukari kwa kiasi kidogo
Mbinu za Kuzuia Kupunguza Madhara Kisukari kwa Mgonjwa:
- Kuacha kutumia sukari
- Kuacha kula vyakula vya unga uliokobolewa
- Kuacha kula nyama na mayai
- Kuacha kula matunda kama ndizi,tofaa(apple)
- Kuacha kunywa maziwa ya ng’ombe
- Kula matunda kwa kiasi kidogo
- Kutafuna chakula vizuri na taratibu
- Kufuata ratiba ya chakula na kula kwa wakati
2. Magonjwa ya Moyo
Haya ni magonjwa yanayosababishwa na ufanyazi kazi wa moyo. Hapa tunazungumzia magonjwa matatu yanayoendana na utendaji kazi wa moyo:i. Shinikizo la Damu
Shinikizo la damunikiasimkandamizo ambao damu inaweka katika yakuta za mishipa yadamuwakati moyo unaposukuma damu mwilini.
Vyanzo vya Shinikizo la Damu:
Shinikizo la damu linasabaishwa na vitukadhaa vikiwemo:
- Kuwa na uzito mkubwa
- Ukosefu wa mazoezi
- Kula vyakula nyenye chumvi nyingi
- Kula vyakula nyenye lehemu na mafuta mengi (Nyama nyekundu kama za ng’ombe,mbuzi na nguruwe ni hatari zaidi. Nyama nyeupe kama kuku na samaki wana madhara kidogo zaidi)
- Uvutaji Sigara-Uvutaji sigara unaongeza hatari ya kufa kabla ya miaka sitini kwa magonjwa ya moyo mara 10 zaidi kuliko asiyetumia. Nikotini katika sigara husababisha mishipa ya damu kubana na hivyo kuongeza shinikizo la damu
- Urithi katika familia yenye magonjwa ya moyo
ii. Kiharusi au “Stroke”
Kiharusikwa kawaida hutokea wakatidamu inaposhindwa kupelekwa katika ubongo ambako kunasababisha kupunguzamtiririko wa oksijeni kwenyeubongo, na kusababishaselikufa.
Kuna aina kuu mbili za kiharusi
- Ischemic Stroke: Hutokea wakati mishipa ya damu inapokuwa imefungwa
- Hemorajiki Stroke: Hutokea wakati mishipa ya damu katika ubongo inapopasuka na kusababisha damu kuchanganika na ubongo.
Vyanzo vya Kiharusi:
- Shinikizo la damu
- Kiasi kikubwa cha lehemu katika damu
- Kula chumvi nyingi(sababu kubwaambayo inaibuashinikizo la damu)
- Kuwa na umri mkubwa
- Jinsia- Wanaume wanaathirika zaidi kuliko wanaume. Na wanawake wanaoathirika wana hatari zaidi ya kufa kuliko wanaume.
iii. Ugonjwa wa Moyo
Ugonjwa wa moyo ni neno linalotumika kuelezea kile kinachotokea wakati ugawaji wa damu katika moyo unapopungua au kufungwa na kusababisha moyo kushindwa kufanya kazi sawa sawa.
Vyanzo vya Ugonjwa wa Moyo:
- Shinikizo la damu
- Kiasi kikubwa cha lehemu katika damu
- chumvi(sababu kubwaambayo inaibuashinikizo la damu)
- umri mkubwa
Mbinu za Kuzuia Magonjwa ya Moyo:
Magonjwa ya moyo(Shinikizo la damu,kiharusi na mengine) yanaweza kuzuiwa yasitokee kwa kufanya yafuatayo:- Kupunguza ulaji wa chumvi
- Kufanya mazoezi ya viungo-Kufanya mazoezi angalau kwa dakika 30 siku 5 kwa juma inapunguza hatari ya magonjwa ya moyo
- Kula vyakula vyenye mafuta kidogo na visivyo na asili ya nyama( Vyenye lehemu kidogo).
- Kuacha uvutaji wa sigara
- Kula vyakula vya mimea zaidi kuliko ya wanyama
- Kupunguza au kuacha kabisa unywaji wa pombe
- Kupunguza misongo ya mawazo
Kubadilisha Mfumo wa Maisha Kutasaidia Kupunguza Hatari ya Kisukari na Magonywa ya Moyo
Madhara ya magonywa haya yanaweza yakadhibitiwa na kuokoa maisha ya watu wengi kama tutabadilisha jinsi yua kuishi. Ulaji wa vyakula visivyofaa kwa afya zetu,kufanya mazoezi na kuacha matumizi ya vinywaji kama pombe na uvutaji wa sigara ni mojawapoya mambo ya kuzingatia. Tujenge mazoea na tabia mpya zenye kuzingatia afya zetu na sio kuishi tu bila kufikiria madhara ya mienendo yetu katika maisha.Mabadiliko huanza nyumbani,hivyo familia zijenge taratibu mpya na tuwafundishe watoto wetu misingi hii mipya ya maisha yenye kuzingatia afya ili kukabiliana na janga la kisukari na magonjwa ya moyo. Vitu kamna vyakula na vinywaji ni suala la familia nzima. Mazoezi ya mwili pia ni utamaduni unaoanzia nyumbani.
Serikali nayo kupitia wizata na taasisi husika zihimize na kutoa elimu juu ya umuhimu wa kubadili mitindo ya maisha na sio kusubiri watuwaugue ndio watoe huduma za matibabu. Kisukari na magonjwa ya moyo yanaweza kuthibitiwa na kupunguza athari zake kama mikakati na elimu sahihi vitatolewa kwa watu.
0 comments:
Post a Comment