Unywaji wa Pombe: Athari zake Kiuchumi,Kiafya na Kijamii


unywaji-wa-pombe-1
Unywaji wa pombe ni suala la kihistoria,pombe imekuwa ikitumiwa katika jamii nyingi kote duniani toka karne na karne kama kinywaji na kiburudisho. Ukiachia kuburudisha pombe imekuwa na madhara mengi kwa binadamu kuliko faida zake ukiachia umaarufu na matumizi yake kuwa mkubwa sana.
Pombe ina athari hasi kiafya,kiuchumi na kijamii. Pombe inajenga kasumba ambayo inamfanya mtumiaji kujisikia kuihitaji na kuitumia mara kwa mara na hivyo kujenga utumwa wa aina fulani kwa kinywaji hiki.
Bila shaka kwa kujua madhara yake pombe imetajwa kuwa kitu kibaya na kukatazwa katika mafundisho ya dini zote kubwa duniani ambazo misingi yake imejengwa katika kusimamia maadili mema.

Unywaji wa Pombe wa Kupita Kiasi:

unywaji-wa-pombe-2
Wataalamu wanasema uwezo wa wanawake na wanaume katika kunywa na kuhimili pombe unatofautiana. Wanaume wanatajwa kuhimili pombe zaidi kuliko wanaume. Unywaji wa kawaida wa pombe ambao una madhara kidogo unasemwa kuwa ni glasi au bia moja (14 gm za kilevi) kwa mwanamke na glasi au bia 2 (28 gm za kilevi) kwa mwanaume, unywaji zaidi ya hapo unatajwa kuwa unywaji wa kupita kiasi na ndio hasa unaoleta madhara zaidi kama ambavyo yunaeleza katika makala hii.
Hata hivyo wataalamu wa afya wanaeleza baadhi ya watu kutotumia pombe kabisa:
  • Wajawazito au wale wanataka kupata mtoto
  • Wagonjwa wanaotumia dawa
  • Waathirika wa baadhi ya magonjwa ambayo pombe italeta madhara zaidi kama ukimwi,kisukari n.k
  • Watu ambao wanafanya au wanapanga kufanya kazi zinazohitaji kufikiria au kuwa na fikra timamu kama kuendesha gari na mitambo,kusoma au kupanga mambo.

1. Madhara ya Unywaji wa Pombe Kiafya

Ni jambo lisilopingika kuwa pombe ina athari mbaya kwa mtumiaji na ni kitu ambacho usipokitumia kabisa au ukiacha kukitumia utapa faida za kiafya
unywaji-wa-pombe-madhara-kiafya-2

Madhara ya Muda Mfupi

Unywaji wa pombe wa kupita kiasi una madhara ya moja kwa moja kwa afya ya binadamu anayetumia. Baadhi ya madhara hayo ni kama ifuatavyo:
  • Kuharisha
  • Kutapika
  • Maumivu ya kichwa
  • Kuumia kutokana na ajali za magari au pikipiki,kuanguka na kuungua
  • Ukatili,kujinyonga,ubakaji na ugomvi
  • Kuathirika na sumu katika pombe kutokana na kilevi kilichopitiliza
  • Tabia hatarishi kiafya kama kufanya mapenzi bila kinga au kuwa na wapenzi wengi wa nje.
  • kutoka kwa mimba kwa wanawake au kuza watoto kabla ya wakati
  • Hupunguza hamu na uwezo kujammiana

Madhara ya Muda Mrefu

Matumizi ya muda mrefu ya pombe yanapelekea kupata magonjwa sugu na madhara mengine kiafya yakiwemo:
  • Msongo mkubwa wa damu-Presha na magonjwa ya moyo
  • Magonjwa ya ini na magonjwa ya mfumo wa chakula
  • Kansa ya matiti,mdomo,koo,ini na kansa ya utumbo
  • Kupoteza kumbukumbu na uwezo wa kujifunza (Sababu ya ukosefu wa Vitamini B1)
  • Matatizo ya kiakili-Kukosa dira katika maisha ya mbele (Depression)
  • Kujenga kasumba ya kutumia pombe (Utumwa wa matumizi ya pombe)
  • Vidonda vya tumbo
  • Kuongezeka kwa uzito-Kutokana na kiwango cha wanga katika pombe
  • Ugonjwa wa mifupa(Osteoporosis)-Pombe inapunguza uwezo wa kalsium kutumika kujenga mifupa
  • Matatizo ya Uzazi-Wanaume wanapungukiwa nguvu za kiume na wanawake kushindwa kushika mimba kirahisi.
Kunywa pombe kidogo kunaweza kupunguza kwa mkiasi kikubwa madhara haya

2. Madhara ya Unywaji wa Pombe Kiuchumi

unywaji-wa-pombe-madhara-kiuchumi-1

Gharama za Pombe:

Matumizi ya kununua pombe ni mojawapo ya gharama kubwa katika familia yenye wanywaji wa pombe. Wanywaji hutumia wastani wa saa moja mpaka tisa(Zaidi ya robo siku) katika unywaji wa pombe na hunywa wastani wa bia 3 mpaka 20 kulingana na uwezo kifedha na uhimili.
Nchini Tanzania wastani wa bei ya bia moja ni sh 2,000.
Bia 3=2,000x 3=6,000/= (Shilingi Elfu Sita za Tanzania)
Bia 10 =2,000×10= 20,000/= (Shilingi Elfu Ishirini za Tanzania)
Bia 20= 2,000×20=40,000/= (Shilingi Elfu Arobaini za Tanzania)
Matumizi Kwa Mwezi: Hutumia kati ya shilingi 180,000, 600,000 na 1,200,000
Hizi ni fedha nyingi sana.
Lakini pombe haiendi peke yake,kuna chakula na vitafunwa(Nyama choma,samaki,supu n.k) hivi vinaleta gharama nyingine karibu sawa na hesabu za bia.
Unaweza ukazidisha mara mbili katika gharama za awali na utapata matumizi ya kati ya shilingi za kitanzania 360,000,1,200,000 mpaka 2,400,000 kwa mwezi.

Gharama za Magonjwa yatokanayo na Pombe:

Gharama nyingine ni zile za matibabu yamagonjwa au madhara yanatokanayo na pombe
Kama ilivyoonyeshwa awali pombe huchangia magonjwa ya moyo,kisukari,vidonda vya tumbo na saratani. Pia huchangia kuumia katika ajali, na uharibifu wa magari na vyombo vingine.
Matibabu ya magonjwa na madhara mengine yaliyotajwa yanaongeza gharama kubwa kwa familia na mtu momoja mmoja.

Utendaji na Uzalishaji Hafifu

Ulevi uanapunguza nguvu kazi. Wafanyakazi walevi hufanya kazi kwa ufanisi wa chini kuliko kama wangekuwa wanywi pombe. Huenda kazini wakiwa na pombe kichwani na uwezo wa kufikiri na ufanisi huwa chini katika hali hii.
Baadhi huchelewa kazini au kutohudhuria kabisa kwa baadhi ya siku au hata kwa muda mrefu.

3. Madhara ya Unywaji wa Pombe Kijamii

unywaji-wa-pombe-madhara-kijamii-1
Madhara ya Unywaji wa pombe yako wazi kabisa katika jamii. Majumbani,sehemu za kazi na hata mitaani. Madhara haya ni kama ifuatavyo
  • Ukosefu wa staha na maadili– Katika ulevi watu wanakosa kujiheshimu, mfano matumizi ya lugha za matusi,ugomvi na hata kujisaidia hadharani ni vitu vinavyotokea.
  • Ubakaji na Ukatili– Katika hali ya ulevi matukio ya ubakaji na ukatili yamelipotiwa majumbani na mitaani
  • Kuvunjika kwa Mahusiano na Familia- Familia nyingi zinavunjika kutokana na ulevi wa wenza wote au mmojawapo
  • Kushuka kwa Heshima: Heshima toka kwa jamii inayokuzunguka toka katika familia yako hadi nje itashuka kutokana na mambo unayoyafanya ukiwa umelewa.
  • Kukosa Muda na Familia: Walevi wanatumia muda mwingi katika unywaji na hivyo kuwa na muda kidogo na familia zao na hivyo kukosa mshikamano na wenza wao na watoto.

Maisha Bila Unywaji wa Pombe Inawezekana

unywaji-wa-pombe-madhara-acha-pombe
Kwa kuona madhara yaliyotajwa,kuna kila sababu ya kuacha kabisa kunywa pombe au kunywa kwa kiasi kidogo ili kupunguza madhara yake. Lakini kuishi bila kunywa pombe inawezekana na watu wengi siku hizi wameona hili na wameamua kuishi katika mtindo mpya wa maisha bila pombe.
Kwa baadhi ya watu ambao ni wanywaji wa kila mara wameathirika na wamejenga kasumba, hawa wanahitaji kupata msaada wa kitabibu na kisikolojia ili waweze kuondokana na utegemezi huu wa wa unywaji wa pombe.
Kama wewe ni mnywaji wa pombe hebu fikiria kidogo juu ya madhara haya na amua.  Amua kuacha kabisa au kupunguza kiwango.
[ Soma: Steps to Quit Drinking Alcohol ]
Na kama wewe hujaanza na unafikiria kuanza kunywa pombe,acha. Una kila sababu za kutokunywa.
Je nini maoni yako juu ya unyaji wa pombe? Wewe au familia yako imethirika kiasi gani katika maisha yako? Tuandikia katika kisanduku cha majibu hapo chini.
Nawatakieni mabadiliko na afya njema.

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger