Showing posts with label mahusiano. Show all posts
Showing posts with label mahusiano. Show all posts

Angalia thamani yako, yanini kumng’ang’ania asiyekupenda?


Ili mapenzi yaweze kuwa bora kwa kila aliye katika mahusiano, huwa ni vyema kila mmoja kuiona thamani ya mwenzake. Ukipenda kujiangalia mwenyewe  si ajabu mwenzako kupata hisia za kuwa humthamini wala humjali.

Muunganiko wenu katika mapenzi maana yake tayari mmekuwa kitu kimoja. Katika mimi unaweka sisi.

Ila pia ni vyema ikakumbukwa ladha na maana halisi ya mapenzi ipo kwa anayekupenda na kukuthamini. Unapokuwa na uhakika kama anakupenda na kukuthamini hapo ndipo nafsi yako itatulia na kuwa na amani. Ndani ya mapenzi na mtu wa aina hii ni amani na utulivu kwa kwenda mbele. Hakuna majuto wala majonzi ya kila siku.

Unapoamua kuwa katika mahusiano na mtu ambaye hakupendi, bali unakuwa naye kwa kuwa tu unampenda jua umejiingiza katika utumwa. Mapenzi ni suala la kihisia zaidi. Mwenzako anapokosa hisia na wewe maana yake hata uwepo wako hauthamini inavyopaswa. Na hapo ndiyo tunaona yale mahusiano ya kingono yanapozaliwa na si ya kimapenzi kwa maana halisi.

Yaani mwenzako anapokuwa na mihemko ya kingono ndipo anapokutafuta na si vinginevyo. Niliwahi kuongea na msichana mmoja aliyewahi kuniambia anampenda kijana mmoja ambaye anauhakika kabisa yeye hampendi. Alinambia uhakika huo kaupata kutokana na kijana huyo kumtakia  kuna msichana yupo anampenda na kumjali ila si yeye.

Kuonesha zaidi kumpenda msichana yule mwingine, jamaa aliwahi kumwambia kama ikitokea hata huyu msichana akagombana na yule mpenzi mwingine wa yule jamaa, kijana yule alikuwa radhi kumdhuru huyu msichana.

Hata kwa matazamo wa haraka hapo unaweza kugundua ni kwa namna gani huyu msichana alikuwa haitajiki. Ila cha kushangaza msichana huyu(aliyeongea na mimi) alimwambia mvulana husika yuko radhi kuwa naye hivyo hivyo.

Aliamua kuwa hivyo akiamini ipo siku jamaa atamuelewa. Kweli walikuwa pamoja. Ila  unajua kinachomkuta sasa?

Kila jamaa anapogombana na yule msichana mwingine anamtumia huyu kingono na mambo mengine yasiyo ya kimapenzi, na bila kutafakari mara mbili huyu msichana anafanya kwa kile anachoamini hali hiyo itamfanya huyu jamaa amfikirie zaidi. Kuna kitu cha kuangalia hapa.

Suala la mapenzi si suala la kuoneana huruma wala aibu. Mapenzi ni hisia. Unapojitoa kwa mwenzako kwa kila jambo na unamuona haelekei ujue hana hisia na wewe. Kwanini unakubali kuteseka na kuumia kila siku kwa kumuangalia yeye tu?

Ndiyo, unampenda sana, unamjali sana na unamuhitaji sana, ila kama yeye hakutaki wa kazi gani? Ni muda wa kujiangalia na wewe sasa.

Ona thamani yako kama binaadamu, jionee huruma jinsi unavyoteseka kila siku kwa mtu asiyeona thamani yako.

Wewe ni binaadamu mwenye hadhi na thamani, bila kujali muonekano wala rangi yako. Unahitaji mwenye kukuthamini na kukujali na si anayekufanya kama mdoli wake ngono au kadi yake ya pesa. Kataa utumwa wa mapenzi kwa kuiona thamani yako.

Ni vyema ukalia kwa kumkosa kuliko kuonekana unaye wakati moyoni siyo wako. Hakuna sifa ya kuwa na mtu mwenye fedha au muonekano mzuri ikiwa hakujali wala haupo moyoni mwake. Mapenzi ni amani na raha.

Mapenzi hufanya watu wafurahi na kusahau shida zao. Ila jiulize kwanini kwako hayako hivi? Unaenda kwa mwenzako badala afurahie uwepo wako, yeye anaona unajipendekeza. Unampigia simu na kumpa maneno mazuri ya faraja, yeye anaona unamsumbua. Sasa wa kazi gani? Siku njema wapendwa.

Jinsi Ya Kumshawishi Mwanamke Kuwa Yeye Ni Mrembo


Kila siku huwa tunapenda kuwaambia wanawake ni warembo. Neno hili limewaingia katika akili zao kiasi cha kuwa ile maana msingi ya neno ‘wewe ni mrembo’ imepotea. Hii ni kwa sababu baadhi ya wanaume wasiojua kutongoza wanaishia kulitumia neno hili vibaya kiasi cha kuwa neno hili limepoteza uhalisia.
Ok, tukiachana na hayo, je ulikuwa wajua kuwa wanawake hupenda kusifiwa? Na ulikuwa ukijua kuwa kumsifia mwanamke mara kwa mara ni njia moja wapo ya kutongoza? Well, leo tumekuja na mambo tofauti ambayo unapaswa kutumia ili umshawishi mwanamke kuwa ni mrembo, na wala hataona kama ni maneno unalompakizia ama maneno ambayo ameyazoea kuyaskiliza awali...
Zama nami...

Jambo la #1
Wakati unapotaka kumsifia mwanamke kuwa ni mrembo, usimwambia, “Wewe ni mrembo” mara kwa mara kwa sababu itafikia mahali flani neno hilo litaisha ladha. Badala yake tafuta sehemu muhimu kutoka kwa mwili wake ambayo utaitumia kama kigezo cha kumsifia. Kwa mfano kama umependezwa na pua yake mwambia, “Nimependezwa na pua yako, kila mara nikiiona najiskia na furaha.” Ama kama umependezwa na mashavu yake unaweza kumwambia, “Mashavu yako ndio nuru ya macho yangu, yanapendeza.” Kumwambia mwanamke maneno kama haya yatamfanya atamani kuwa kando yako. Pia ataona kuwa unamwona anapendeza, unamakinika kuuona urembo wake kupitia kwa viungo vyake vya mwili.

Jambo la #2
Kumsifia mwanamke urembo wake hakuhusishi ngozi yake ya nje pekee, bali pia sehemu yake ya ndani, yaani nafsi yake. Wanaume wengi huwa wanamakinika kumsifia mwanamke umbo, sura na shepu yake huku wakisahau kuwa nafsi ya mwanamke ina umuhimu. Kumsifia mwanamke kwa ujasiri wake, ubunifu wake, hikma, na ujanja kutakupa mkono wa mbele zaidi wakati unapomtongoza ama unapomshawishi. Jambo hili tulishawahi kulizungumzia katika moja ya hatua ya kumtongoza mwanamke ambaye hayuko ligi sawa na wewe. Kumshawishi na kumsifia mwanamke nafsi yake kutamfanya ajiunganishe na wewe zaidi kuliko mwanamke yeyote yule, hivyo hatua iko kwako sasa.

Jambo la #3
Unapomsifia mwanamke usitumie maneno yayo kwa hayo. Yaani wewe kila siku ukikutana na yeye unamwambia, “Nakupenda, leo umeangaza nafsi yangu.” Matumizi ya neno moja siku nenda siku rudi kutamfanya mwanamke atilie shaka iwapo unasema maneno hayo ndani ya moyo wako ama unasema kumridhisha tu. Well, mbona usije na misamiati mipya? Ama mbona usije na maneno ambayo angetamani kuyaskia? Ukitumia maneno kama ‘hurulaini’, ‘malkia, leo nimekuja kwa milki yako’, ‘ua langu la waridi’ nk kutamfanya mwanamke akupende zaidi na zaidi. So anza kutafuta maneno ambayo anayapenda. Usiingiwe na uvivu wa kutumia maneno yayo kwa yayo. Kumbuka hapa unataka kuwa mbora zaidi kati ya wanaume wale wengine. Chukua hatua sasa.

Jambo la #4
Wakati ambapo umeamua kumsifia mwanamke kama huyu, hakikisha kuwa unamwangalia machoni. Kama ni mwanamke ambaye ndio unaanza kumfukuzia basi jenga confidence ya kumwangalia machoni. Usimsifie huku ukiangalia pembeni ama kuangalia kando. Kumbuka wewe ni Mwanaume Alpha, na wanaume alpha huwa hawatatiziki kama wanatoa hisia zao kuhusu wanawake wanaowapenda.

Hatua Za Kufanya Kama Mwanamke Hataki Kujibu Texts Zako


Unafukuzia mwanamke mzuri mnaanza kuzungumza. Mnachukua muda wa dakika 20 hadi 30 kuongea na yeye mara ya kwanza. Anapendeza na kuvutia, na unaona kama ni mwanamke ambaye ni yule aliyekuwa ndotoni mwako maishani mwako. Mazungumzo yenu yanaenda vizuri mpaka ukwamwomba namba yake.

Baadaye unajaribu kumtumia text na hazijibu. Labda mnaeza kuchat kwa madakika halafu baada ya hapa anakataa kujibu texts zako. Unabaki ukijiuliza maswali ni kitu gani ambacho umefanya ambacho umekosea. Ok labda anaweza kuwa yupo buzy unampa muda kiasi ajibu text zako...unangojea masaa, siku, wiki mpaka inafikia wakati unagundua kuwa amekupuuza. Kwa nini hajajibu text zako?

So kwa nini hakujibu text zako?
Katika situation nyingi ni kuwa sababu kuu ambayo amekataa kujibu texts zako ni kuwa haukumpendeza mara ya kwanza ulipokutana naye. Ok labda sababu nyingine inaweza ni kuwa ameibiwa simu yake wakati alipokuwa akitext na wewe barabarani ama kitu kingine kama hicho, lakini hapa acha tumakinike na hatua ya kwanza uliokutana naye...yaani first impression ambayo unakudana na mwanamke yeyote.

1. Hakikisha unampendeza mara ya kwanza unapokutana naye
Anaweza kuwa hana muda mrefu wa kukaa na wewe ili akutambue zaidi so kile kitu ambacho unahitaji kufanya ni kuwa lazima uuonyeshe upendo wako kwa kuwa mpole, mkarimu na mtulivu. Hii itamfanya yeye kumakinika na labda kutaka kukufahamu. Hakikisha kuwa wakati unapoongea na yeye tumia mbinu za kuonyesha kuwa ungependa kukutana na yeye wakati mwingine. Kama hakuonyesha dalili zozote za kukuelewa basi hata kama atakupatia namba yake ya simu fahamu ya kwamba itakuwa ni kazi bure.

2. Taja sababu zako za kuongea na yeye
Mfano: Nimefurahia sana kuongea na wewe. Kusema kweli nimependa maonezi yetu machache. Nataka kwenda lakini naonelea wikendi nitakutext tukutane ili tuongee tena. Hapa utakuwa umeeleza ajenda yako kwake hivyo ukianza kuchat na yeye baadae haitakuwa vigumu kwake kukujibu.

3. Hakikisha kuwa unamtumia text wakati ufaao
Ukiomba namba ya simu kwa mwanamke inamaanisha kuwa wewe umeonyesha intrest kwake vilevile mwanamke akikupatia namba yake ya simu inamaanisha kuwa labda itakuwa amependezwa na wewe. Lakini je, ni muda upi unaotakikana hadi umtext mwanamke huyo.

Wanawake wanapenda kuona wanababaikiwa na kufukuziwa. So usijaribu kumtext hapo hapo wakati amekupatia namba yake. Hakikisha umejibatia shughli nyingi ili usahau kabisa kama uchukua namba kwa mwanamke. Masaa mazuri ambayo yangekuwa sawa ya kumtext ni baada ya masaa 24 baada ya kuchukua namba yake. Hii itamfanya mwanamke yeyote kujiuliza maswali ya kwa nini umechukua muda mrefu kumtext. Itamfanya kuingiwa na maswali ya kama: kwani hajapenda chat yangu? yuko na mwingine? nk. Ukichukua muda huu mrefu hadi kumtext, itakuwa rahisi kwake kukujibi.

ONYO: Hakikisha ya kwamba haupitishi zaidi ya siku tatu kwani anaweza kukusahau kwa haraka ama kuona unampotezea wakati wake.

4. Kitu cha kuandika kwa text yako ya kwanza
Messages za kwanza ambazo utazituma kwa mwanamke zitachangia pakubwa kuona kama wewe uko uko interesting ama unaboa. Unaweza kuuharibu mchezo mzima kama iwapo utaanza kumtext na mambo ambayo hayana manufaa kwake. Kile kitu unachohitajika kufanya hapa ni kuonekana hauna haraka na ujaribu kutumia lugha za kirafiki. Mfano unaweza kujaribu kumtext swala ambalo aliligusia kwa chat iliyopita. Labda aliongea kuhusu kwenda shopping na nduguyake, so swali lakini linaweza kuwa: Je ile shopping yenu na nduguyako iliendaje?. Hii itamfanya kuwa interested na wewe manake ataona ya kuwa ulikuwa umemakinika wakati mlipokuwa pamoja. Hii itamfanya kujibu text zako mara kwa mara bila yeye kuchoshwa.

5. Jaribu kuhepa stori ambazo hazitafikia popote
Mara ya kwanza anaweza kukujibu lakini itafikia pahali atanyamaza. KUMBUKA: Siri kuu ya kumfanya mwanamke ajibu texts zako ni uwe makini kwake, yaani unamtext vtu ambavyo unajua yuko intrested navyo.

6. Weka wazi kuwa unataka mkutano
Acha stori za kumzungusha huku na huku kama wanaume wengine. Ukitaka akujibu text zako hakikisha ya kuwa unadhihirisha azma yako kwa kumwambia kuwa unataka kukutana naye.

7. Usikate tamaa
Kuna wanaume wengine kama wamekataliwa kujibiwa texts zao mara moja basi wanakasirika na wanaachana kabisa na kushungulika tena. Tatizo labda linaweza kuwa mwanamke anakupima akili aone bidii yako kwake. Kama tujuavyo tabia za wanawake ni kuwa hawapendi kuonekana kama ni watu wa kukubaliana na kila kitu hivyo basi wakati mwingine wanakuwa hawaeleweki.
Ukiona mwanamke amekataa kujibu text yako kwa siku tatu, fanya kumtext tena huku ukionyesha kuwa hauna intrest naye sana vile halafu achana naye. Hii itamfanya yeye kuona una interest na yeye lakini hauna haraka. Baadaye anaweza kuanza chat yeye mwenyewe.

KUMBUKA: Kuna sababu tofauti tofauti ambazo zinaweza kumfanya mwanamke kukataa kujibu texts zako. Labda umemtusi, hujampendeza, ni mwanamke mwenye haya nk. So hizi hatua zitategemea na vile imetokea katika situation yako.

MADHAIFU MATANO (5) YANAYODIDIMIZA MAHUSIANO NA NDOA

Makala hii ni tafakari huru kuhusu mambo ya msingi katika mahusiano.  Hapa utapata tafakari ya maana ya maneno na imani ambazo zinatutatiza wengi wetu.
1. Mchanganyiko mkubwa kuhusu maana ya mahusiano, mapenzi na ndoa:
Labda kipengele hiki tuanze kwa kueleza kuwa kunaweza kuwepo ndoa, lakini yasiwepo mahusiano wala mapenzi. Inaweza kuonekana kama inachanganya kidogo, lakini ndio ukweli wenyewe.  Ndoa ni namna tuu ambayo wawili walio kwenye mahusiano wanaamua kuwataarifu rasmi watu wengine kuwa wao wapo rasmi katika mahusiano. 
Ndoa ni kiapo mbele ya watu wengine , na ni namna ya kutaka kumuhakikishia mwenza wako kuwa endapo kiapo hicho kitatokea kuvunjika, basi unakubali rasmi kuwajibika kwa mujibu wa taratibu zilizopo za ndoa husika, ikiwemo kukubali kuitwa kwenye mabaraza ya usuluhishi, kugawana mali, n.k. Na kwa upande wa kiroho, inabeba maana zaidi kuwa unaweka kiapo kwa Mungu wako kuwa utalinda mahusiano yako na huyo unayemchagua.
 Hivyo basi, ndoa haijengi mahusiano wala mapenzi. Kiuhalisi inabidi kwanza yawepo mahusiano na mapenzi kisha ndio kiapo kifanyike, kwani kinyume cha hivyo ni kuwa unakula kiapo ‘feki’.
Ndio maana basi, ni muhimu kwa wapenzi kutambua kweli kama wanahitajiana, kuwa kwenye mahusiano na kutafakari kwa uhuru kama kweli wanataka kuweka kiapo rasmi cha kuwa pamoja.
Kutumia ndoa kama kinga ya kuhakikisha mahusiano yako yanadumu ni maamuzi magumu ambayo pengine yanaweza yasilete faida hapo baadae.
2.Mahusiano na ndoa nyingi huyumbishwa na Matarajio yasiyo halisi
Kabla hata ya kuingia katika mahusiano na hatimaye ndoa wengi wetu huwa na matarajio binafsi ya kimaisha. Matarajio haya yanajumuisha vile tunavyotaka sie wenyewe kuwa hapo baadae, pamoja na matarajio ya vile tunavyotaka wenza wetu wawe.
Hata hivyo katika hali halisi tunajikuta sisi wenyewe hatuwezi kujibadilisha au kujiweka kwa usahihi vile tunavyotamani kuwa (kwa sababu kwa kila tunachojaribu kufanya kuwa bora, tunajikuta bado tuna madhaifu mawili matatu). Pamoja na ukweli huu, tunajikuta tupo na matarajio ya kuwafanya wenza wetu wawe watu wa aina fulani. Kwakuwa kiasili binadamu ni kiumbe huru, tunajikuta wenza wetu nao wakiwa ‘busy’ kutimiza ndoto za vile wanavyotamani kuwa iwe kimavazi, aina ya marafiki, utafutaji wa kazi , kujiendeleza kimasomo, aina ya mali za kununua, hata kufikiria tofauti aina ya maisha wanayotaka muishi.
Matokeo yake ukinzani huu wa matarajio ni mkanganyiko wa mgongano wa mawazo kati ya wawili nyie, na mwanzo wa vita ya chini kwa chini ya nguvu ya maamuzi katika mahusiano yenu.
3. Kuweza kumbadili tabia mwenza wako
Mojawapo ya jambo ambalo hufanywa na wengi walio katika mahusiano ni kuwa na ‘tamaa’ ya kutaka kumbadili tabia fulani mwenza wake. Hata hivyo ‘tamaa’ hii ni sehemu ya yale tunayoyaita matarajio yasiyo halisi, kwani tabia ya mtu hujengwa na mambo mengi sana, ikijumuisha aina ya makuzi, aina ya mfumo wa imani mtu anaouamini, aina ya marafiki alio nao, uwezo wake wa kujiamini katika kubadili tabia kwani wengine wameshakata tamaa kuwa hawawezi kukata tamaa, na zaidi sana, mabadiliko ya tabia huhitaji mfumo endelevu na wenye kusoma vema asili ya tabia ili kuweza kuirekebisha.
Hata hivyo wengi wetu kwenye mahusiano, hutegemea ‘mapenzi’au vitisho tuu kama vile ‘nitakuacha mie ’,  kama sababu ya kumfanya mtu abadilike kitabia.Udhaifu wetu katika kutambua asili ya tabia ya mtu husika na mbinu za kisayansi za kubadili tabia hufanya zoezi la kubadilishana tabia kuwa gumu na pengine lisilowezakana.
4. Kuvumilia ndio kuonyesha upendo na ndio kudumisha mahusiano
Hii ni aina nyingine ya matarajio ambayo sio halisi kwani kiukweli kila mtu analo jukumu la kufanya bidii kuwa mtu mwema, hivyo hauhitaji kubeba ‘uzembe’ wa mwingine kwa kisingizio tuu cha kuwa unaonyesha upendo hususani pale ambapo ni kwa uzembe tuu au kutokujali kwake mwenza husika amefanya jambo fulani.
Kwa jinsi kasumba hii ilivyo enea sio ajabu kukuta mtu akifanya mambo mabaya kwa mwenza wake kwa makusudi ili tuu eti apime kama kweli mwenza wake ni mvumilivu.
Kumbuka hapa hatumaanishi kuwa kusamehe ni kosa. Hapana, kusameheana ni muhimu, lakini sio kwamba ni muhimu tuu katika mapenzi. Kusameheana ni jambo la asili, na tunapaswa kusameheana kwa mambo mengi nje hata ya mahusiano. 
Tunachosema ni kuwa kuna  kasumba ya baadhi yetu kuona kuwa wanayo ‘haki’ ya msingi ya kukosea eti tuu kwakuwa tuu mwenza wake analazimika kusamehe ili kuonyesha kweli anao upendo wa dhati.
Amini usiamini, kasumba hii ya kutarajia aina ya pekee ya kusamehewa na kuvumiliwa kwa kisingizio tuu cha kuwa upo kwenye mapenzi na mwenza wako, hurudisha nyuma maendeleo ya mahusiano yenu kwani mwenzi wako nae ni binadamu na kumbuka anayo matarajio mengine ya maisha, isitoshe na yeye anahitaji upendo na kujaliwa na wewe, hivyo kutarajia kwako kusamehewa na kuvumiliwa kuna mnyima haki mwenza wako. Hatimaye kutegema kwako kusamehewa kila wakati, kunamfanya mwenza wako atilie mashaka upendo wako kwake.
5. Uaminifu = Upendo= Kudumu kwa mahusiano
Pamoja na ukweli kuwa mwenza wako anatarajia utakuwa muanifu kwake, elewa kuwa kuwa mwaminifu pekee katika mahusiano yako sio tiketi ya kudumu kwa mahusiano yenu kwakuwa watu wanaingia kwenye mahusiano sio tuu kwa kuwa wanataka kuwa na mtu mmoja muaminifu bali wana mahitaji mengine wanayohitaji.
Zungumza na mwenza wako, fanya utafiti wako binafsi kuhusu mpenzi wako ujue mambo mengine anayohitaji toka kwako. 
Pia msikilize anapokutaka urekebishe mambo kadhaa au ufanye mambo fulani. Inapendeza pale unapomfanyia mtu mambo yanayompendezesha kwa kuwa hivyo ndivyo anavyotaka, sio kwakuwa tuu wewe unadhani kufanya hivyo kutampendezesha mhusika.

SABABU 5 KWANINI UPENDO HAUTOSHI KUJENGA MAHUSIANO BORA

Ukisoma kwa kutafakari makala hii utagundua kuwa kuweza kujifahamu sisi wenyewe vema, kuweza kujitawala sisi wenyewe, na pia kuweza ‘kuwasoma’ vema wenzi wetu , ni mambo ya msingi sana ili upendo tulionao uweze kudumisha mahusiano.  Msisitizo ni kwamba, pamoja na ukweli kuwa upendo ni kitu cha muhimu katika mahusiano, makala hii inaeleza kuwa kutegemea upendo pekee kama nguzo kuu ya mahusiano bora kunaweza kuwa jambo la hatari kwa mahusiano, kwa sababu zifuatazo:-
1. Binadamu ni kiumbe huru: Ni muhimu kukumbuka hili hasa kama unadhani kwakuwa unampenda fulani na umemuonyesha mapenzi yako yote basi hicho ni kama kifungo kwake kuwa hatoweza kutoka katika penzi lenu. Kwa asili binadamu ni huru, na anaweza kuamua kuutumia uhuru wake kufanya maamuzi mengine yoyote tofauti na unavyofikiri ni lazima afanye.  Kwa kuwa pia ni mbinafsi, basi kama upendo wako wote kwake hauendani na yale anayotazamia , unaweza kukuta ameshindwa kukaa katika penzi , ambalo kwa watu wengi wanaona kuwa ni penzi zito.
2. Binadamu ni mbinafsi kwa asili: Binadamu kwa asili huangalia maslahi yake kwanza kabla ya kuangalia ya mwingine. Mfano dhahiri wa ubinafsi huu ni pale inapotokea ajali , mara nyingi mtu huwaza kujiokoa mwenyewe kwanza kabla ya kufikiria wa karibu yake. Tumesikia habari za mama mzazi kuacha kitoto kichanga ndani wakati moto ukiendelea na yeye kutoka nje. Kuna habari pia za mama kumtumia mtoto wake kama ‘kifaa’ cha kuvunjia kioo cha gari , ili aweze kujiokoa, pale ambapo ajali ilitokea. Hivyo upendo tuu pekee hautoshi kumfanya mtu aendelee kukaa katika ndoa au mahusiano kabla ya ndoa (uchumba), ni muhimu yawepo mambo mengine yenye manufaa kwa mtu husika.
3. Binadamu ana mahitaji mengi  na yasiyo na kikomo:  Mwenza wako ana mahitaji mengi na yanaongezeka na kubadilika siku hadi siku kutegemeana na mabadiliko mbalimbali kama vile hali ya hewa, aina ya kazi,  watu anaokutana nao, mabadiliko ya teknolojia, mabadiliko ya kiuchumi n.k. Upendo wenu, hausimamishi mahitaji haya yasitokee, na kwamba upendo pekee hauwezi kuwa jibu la kutimiza mahitaji hayo. Inahitajika bidii katika kujituma kujiletea kipato, kuwa na mawasiliano bora kati yenu, kutambua mabadiliko na kuchukua hatua kabla mabadiliko hayajawabidilisha, na zaidi sana muweze kuwa na utamaduni wa kupanga mambo pamoja na kuwa waaminifu katika kutimiza yale mnayopanga. 
Chukulia mfano, wa wanandoa walioishi vema kwa miaka 5 ya ndoa, halafu ndoa ikaanza kulemaa kwa kuwa mmoja wao anaona hakuna uwajibikaji katika kumsaidia mwengine kujiendeleza kielimu, kibiashara, au kutimiza ndoto nyingine ambayo mwanandoa amekuwa nayo.
4. Binadamu wengi wanashindwa kujitawala:  Uwezo wa mtu kujitawala unaweza ukakinzana na upendo wake kwa mwenza wake, hivyo kuleta hali ya kutoridhika kwa mwenzi wake, kitu ambacho kinapunguza  au pengine hata kuondoa raha ya mahusiano. 
Mfano utakuta kwa kufuata makundi ya marafiki aliyonayo, mwanaume anakuwa mlevi wa kupindukia,  na kujikuta akiingia katika anasa na maamuzi mengine yasiyo mazuri kwa mpenzi wake na familia kwa ujumla. Hata hivyo mwanaume huyo huyo ukimuuliza kama anampenda mke wake au la, atakujibu anampenda sana. Tatizo nini ? Utajibiwa, ni pombe tuu ndio mmemtawala, na kwamba jamaa ana ‘kampani’ mbaya.
5. Maana isiyo sahihi ya upendo: Kuna wengi wanaodai wanao upendo lakini kiukweli walichonacho sio upendo bali ni tamaa au matakwa ya kuhitaji kutimiziwa mambo fulani. 
Maana halisi ya upendo sio vile unavyotaka fulani akufanyie mambo au jambo fulani, upendo sio vile unavyojisikia baada ya fulani kukutendea jambo uliloliona jema kwako, upendo sio vile fulani anavyokufanya ujisikie kwa sababu ya sura yake au umbo lake, BALI, upendo ni utayari wako wewe kufanya mambo yanayompendeza mwingine, kuwa tayari kuona mwingine ana furaha juu yako.  
 Kwa maana rahisi , upendo si jambo linalokuhusu wewe unajisikiaje, bali ni vile unavyotaka mwingine ajisikie.
Kwa maana nyingine, utatimiza vema upendo wako kwa kujitahidi kumfahamu mwenza wako, kutimiza yale anayohitaji (ili awe na furaha) sio kutimiza yale unayotaka wewe kwa makusudio yako binafsi. Upendo unahitaji kumheshimu mwenza wako, kumsikiliza, kumfanya akuamini, na aendelee kukuamini.
Pamoja na kuwa hisia za kimwili (chemistry) ni muhimu sana katika kujenga mahusiano yenu,  hisia za kimwili zisichanganywe na upendo. 
Kwakuwa fulani amekuvutia kimwili haina maana kuwa basi unampenda mtu huyo. 
Kufanya tendo la ndoa, sio lazima iwe ndio ishara ya uwepo wa upendo katika yenu, kwani wapo hata wanaofanya tendo la ndoa kama biashara.
Hitimisho
Mahusiano hususani mahusiano ya kimapenzi yanatutaka tuwe waajibikaji kwa wenzetu, na kwetu wenyewe. Kuwajibika kwa wenzetu ni pale tunapojifunza vya kutosha tabia,  na yale yanayompendeza na yasiyompendeza mwenza wetu. Wakati tunawajibika kwetu wenyewe kwa kujifunza kuhusu mapungufu yetu, na kujituma kujirekebisha. Mapenzi yanaleta majukumu, na bila kutambua na kutimiza majukumu husika, mara nyingi mapenzi yatageuka kuwa karaha, badala ya furaha.

FANYA HAYA 6 KUZUIA WATU WASIINGILIE MAPENZI YENU

Sio mbaya kwa marafiki wa karibu au ndugu na jamaa kufahamu kushirikiana nanyi katika mapenzi yenu kama vile wakati wa sherehe au msiba. Pia sio mbaya kujuliana hali na kutambulisha mambo ya msingi yanayoendelea katika mahusiano yako wewe na mpenzi wako. Hata hivyo kuna wakati watu wengine wa pembeni, wawe majirani, ndugu, wazazi au marafiki wanaweza kuwa ‘sumu’ ya mahusiano yako, hasa pale unapowategemea sana kutoa msaada, maoni au maelekezo katika maisha yako ya mapenzi.  Makala hii inaeleza mambo ya msingi unayoweza kufanya ili kupunguza uwezekano wa rafiki, ndugu, jamaa, au wazazi kuwa ‘sumu’ ya mapenzi yako.
1. Udhibiti wa taarifa kwa wengine:  Kadri unavyoelezea mahusiano yako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa nafasi watu kutoa maoni, na hata kudhani kuwa wana dhamana ya kukuelekeza unavyotakiwa kuishi na mwenza wako. Hivyo basi, chukua muda wa kutosha kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu maswala yako ya mahusiano kabla haujaanza kutafuta maoni, ushauri kwa watu wengine. Ni bora ukasoma vitabu, na makala mbalimbali, hususani zihusuzo tabia na maisha ya mahusiano, zitafakari vema ili kuona zinahusiana vipi na unayokumbana nayo katika mahusianao yako.
2. Upekee wa mambo:  Tambua kuwa tabia ya mpenzi wako inaweza kuwa ni ya kipekee, mazingira pia ya tukio linalokufanya utake ushauri au maoni kwa wengine yanaweza kuwa ni ya kipekee, hivyo ushauri au maoni utakayopokea yanaweza yasikusaidie moja kwa moja katika suluhisho lako. Ukitambua hili, utafanya bidii ya kujenga uwezo binafsi wa kuchambua tatizo unalokumbana nalo katika mahusiano na kutafuta suluhisho kabla ya kutegemea watu wengine.
3. Mwenye maamuzi ni wewe: Ni kweli kuwa kuna nyakati ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa watu wengine, na zaidi sana watu wenye uelewa sahihi na unaowaamini, hakikisha kuwa unatambua kuwa wewe mwenyewe ndio mwenye kubeba lawama ya maamuzi utakayochukua. 
4. Kuwa na subira: Usichukue maamuziya haraka katika mahusiano hususani uamuzi wa kuamua kuwashirikisha watu wengine habari ya mambo yahusuyo uhusiano wako. Unapofanya uamuzi wa kuwashirikisha wengine kwa haraka  unajinyima nafasi ya kulichunguza jambo kwa ufasaha hususani madhara yanayoweza kutokea kwa kuwaeleza wengine, au kama ni tatizo, basi kufikiria njia sahihi ambazo ungeweza  kuzitumia kupata suluhu ya tatizo. 
5. Fungua njia za mawasiliano kati yenu: Pengine chanzo cha wewe kutaka kuzungumza mambo ya ndani yanayohusu mahusiano yenu kwa watu wengine ni kwakuwa umekosa  nafasi ya kuzungumza kwa ufasaha na mwenzi wako. Tafuteni nafasi za kutosha, jengeni mazingira ya kuzungumzia mambo yenu kabla ya kutaka kuwashirikisha watu wengine. 
6. Kuweni peke yenu:
Hata kama hautaki kueleza watu kuhusu mambo yanayoendana na maisha yenu, mazingira unamoishi yanaweza kuchangia watu kutaka kuingilia mahusiano yenu –kwa kutoa maelekezo, ushauri au maoni  kuhusu muishivyo wewe na mpenzi wako. Inapobidi hakikisha hamuishi karibu na wazazi wenu, ndugu au rafiki wa karibu. Au haufanyi kazi na mwenzi wako sehemu moja, kwani hiyo itakuwa njia rahisi sana ya watu kuona mnavyoishi.  Inapobidi kuwa karibu na watu wengine , hakikisha mnakubaliana wewe na mwenza wako namna bora ya kuendesha mawasiliano kati yenu mbele za watu, ili msiwape nafasi ya wao  kumi‘soma’ na kisha kuanza waje waanze kutoa ‘maelekezo’ ya vile wanavyoona mnapaswa kuishi.
7. Nenda ‘darasani’ :  Kumbuka mahusiano yanahitaji sana uelewa mkubwa wa jinsi ya kufanya mawasiliano fasaha, kuelewa hisia za mwenzi wako, kutambua mbinu za kusuluhisha migogoro, na zaidi sana kufanya mipango ya muda mrefu ya uhusiano wenu. Jizoeshe kusoma makala na vitabu mbalimbali vyenye kuboresha ufahamu wa mambo ya msingi kama hayo tuliyoeleza hapo juu. Mfano wa makala unazoweza kusoma ni kama vile: MADHAIFU MATANO KATIKA MAPENZI

Malezi ya Kuchapa Watoto-Nidhamu au Ukatili?

malezi-ya-kuchapa-watoto
Adhabu ya kuchapa watoto kwa dhumuni la kukanya na kufundisha imekuwa ni njia mojawapo ya malezi kwa familia na shuleni kwa nchi nyingi duniani ukiachia baadhi ya majimbo ya Marekani na nchi za ulaya. Wataalamu wa saikolojia wanahusisha adhabu ya kuchapa na tabia zao ukubwani ukiachia mbali uvunjaji wa haki za binadamu na watoto.
Nchi 37 duniani zimekataza kabisa watoto kuchapwa,iwe na mwalimu,mlezi hata mzazi mwenyewe na nchi 113 zinazuia adhabu ya kuchapa watoto mashuleni,lakini kwa nchi zinazobakia ikiwemo Tanzania adhabu ya kuchapa watoto kwa wazazi ,walezi na hata mashuleni ni ruksa
malezi-ya-kuchapa-watoto-3
Mtoto akicharazwa viboko na mwalimu shuleni

Kuchapa Watoto ni Ukiukwaji wa Haki za Binadamu na Watoto

Kutokana na sheria za haki za watoto duniani “Kuchapa mtoto ni ukatili” na zinashauri serikali duniani kuzuia aina hii ya adhabu kwa watoto.
Kutokana na haki za binadamu “Kila mtu ana haki ya kupata ulinzi juu ya mwili wake” na mtoto ni bianadamu pia. Kwa nchi nyingi kama si zote duniani, kumpiga na kumsababishia maumivu mtu mwingine ni kosa la jinai,kwanini kumsababishia mtoto maumivu iwe kwa sababu nyingine yoyote isiwe kosa? Haya ni mambo yanayotakiwa kuangaliwa na kufanyiwa mabadiliko kama tamaduni nyingine zisizotakiwa katika karne hii kama ukeketaji wa wanawake na ukatili kwa wanawake.
malezi-ya-kuchapa-watoto-ni-ukatili
Baadhi yao Hupata Majeraha Makubwa na Hata Ulemavu

Madhara ya Uchapaji Watoto

Kuchapa watoto kunaathiri tabia zao ukubwani,Utafiti unaonesha kuwa adhabu ya uchapaji watoto ina madhara hasi(hasara) zaidi kuliko chanya(Faida). Watoto wanaochapwa mara nyingi wanakuwa na tabia za kuchapa wengine mbeleni katika maisha yao na inahusihwa pia na ukatili kwa wengine.

Sababu 5 za Kuacha Kuchapa Watoto

1. Zinawafundisha Watoto Wenyewe Kuwa na Tabia ya Uchapaji

malezi-ya-kuchapa-watoto-ugomvi
Watoto wanafanya vile wanavyoviona toka kwa wazazi na walezi wao
Utafiti unaonesha kuwa watoto wanaochapwa utotoni wanajenga tabia ya kuwa makatili na wachapaji wakiwa wakubwa na watu wazima. Majambazi na wauwaji wengi wamegundulika kuwa walikuwa mojawapo ya watoto walionyanyaswa au kufanyiwa ukatili wakiwa wadogo. Ifahamike tabia za watoto zinajengwa kwa kiasi kikubwa kwa kuiga wazazi au wakubwa wao wanachofanya hasa wakiwa katika umri mdogo.

2. Inatia Hofu Kwa Watoto na Kuwafanya Wakose Upendo

malezi-ya-kuchapa-watoto-hofu
Mtoto anapochapwa hujenga hasira,kukata tamaa na hisia za kisasi na kukosa upendo.
Watoto wengi wanapochapwa huhisi wameonewa na humchukia aliyewaadhibu hata kama ni mzazi wao. Adhabu za aina hii zikiwa zinatolewa kwa muda mrefu huweza kuwajenga watoto wasio na upendo kwa wengine na hata wao wenyewe.
Hasira za utotoni zinafukiwa ndani na zinakuja kulipuka wakiwa wakubwa,usishangae kwanini watoto wako wamekuwa na tabia za ajabu wakati uliwafundisha maadili mzuri.
Pia wanajifunza kuwa ni sawa mwenye nguvu kumuonea asiyenazo na inawajenga kuamini kuwa mwenye nguvu ni wakuogopwa na wanajifunza kukubali kuonewa na kunyanyaswa.

3. Zinakata Muunganiko wa Upendo kati ya Mzazi na Mtoto

malezi-ya-kuchapa-watoto-utengano
Utengano wa Kihisia ni Mtokeo ya Malezi Wanayopewa Watoto
Si asili ya binadamu au kiumbe yeyote kumpenda mtu anayemuumiza. Adhabu za kuchapa hata kama zinaonekana kufanya kazi nzuri,madhara yake ni makubwa kwa siku za mbele kwani matokeo unayoyaona yanatokana na hofu pekee na ni ya muda mfupi.

4. Inawafanya Wazazi Kutojifunza Njia Nyingine za Malezi

Wazazi ambao wamekua katika mfumo huu wa kuchapa kama njia ya malezi wanakosa nafasi ya kujifunza njia nyingine ambazo zina matokeo mazuri,sababu hii ni njia pekee ambayo imekuwa ikitumika na wanayoijua. Ni wakati sawa wazazi wakaangalia njia nyingine.

5. Inawafundisha Watoto Kukubaliana na Uonevu

Watoto wanajifunza kuwa ni sawa kwa mwenye nguvu kumuonea asiyenazo na inawajenga kuamini kuwa mwenye nguvu ni wakuogopwa na wanajifunza kukubali kuonewa na kunyanyaswa.

Utamaduni wa Kuchapa Watoto ni Budi Kukomeshwa

malezi-ya-kuchapa-watoto-ukomo
Kumsababishia binadamu mwingine maumivu kwa sababu yoyote ile ni ukatili na unyanyasaji ambao ni lazima tuukomeshe. Sisi wenyewe tumeathirika na unyanyasaji toka enzi za ukoloni na utumwa ambapo aina hizi za adhabu zilitumika sana,inashangaza kama na sisi bado tunatumia kwa watoto wetu wenyewe.
Hali ni mbaya sana mashuleni hasa shule za msingi ambapo watoto wanachapwa viboko kwa wingi na bila kipimo maalumu. Nguvu zinazotumika katika utoaji wa adhabu kwa watoto ni kubwa sana na inatumika kwa viumbe visivyo na msaada wowote wa kujitetea.
Watoto unafanyiwa ukatili mkubwa mashuleni na ni muhimu kila mmoja wetu achukue hatua dhidi ya ukatili huu. Ni wakati sasa wa kufanya utafiti na kutumia majibu ya tafiti juu ya malezi bora katika kuelimisha na kulea watoto wetu ambao ni taifa la kesho.

Ushiriki wako Ukoje?

Tuambie ushiriki wako katika kuchochea au kuzuia aina hii ya ukatili kwa binadamu hawa wadogo-Watoto. Unafikiri vipi juu ya hili? Unafikiri viboko na vichapo ni njia ya kibinadamu ya kulea na kukanya watoto? Je kuna njia nyingine ambayo unafikiri inaweza kutumika kama mbadala na ambayo ina matokeo mazuri?
Changia mada hii kwa kutuandikia katika kisanduku hapo chini na tuendeleze vuguvugu hili na kuleta mabadiliko katika suala hili.
Kumbuka “kukaa kimya juu ya ukatili ni sawa na kushiriki” chukua hatua.

Mambo Yanayomfanya Mtu Kupendwa na Watu



kupendwa-na-watu-2
Kila mtu anahitaji kupendwa kama mtu,mzazi,mwenza,mtoto au mfanyakazi. Inaleta raha na faraja kubwa moyoni. Lakini wakati mwingine si rahisi sana kupendwa na watu wengi. Wengine wanasema kuwa haiwezekani kupendwa na kila mtu,kwasababu kila mmoja ana vigezo tofauti vya kuchagua nani anampende na kinyume chake. Ila kuna vigezo ambavyo watu wengi wanathiriwa navyo juu ya maamuzi yao ya kupenda. Kwakweli maamuzi haya si ya hiyari ila yanakuja kwa hisia zaidi kutoka katika mawazo ya kina ambayo yanaongoza hisia za watu.
Hisia hizi zinajijenga taratibu ndani ya moyo wa mtu kutokana na matukio yanayotokea kila siku au kila mara na kuwekwa katika mawazo ya kina.
Ili upendwe na watu unatakiwa kujenga tabia amabazo watu watazipenda na hivyo wewe mwenyewe kupendwa. Kumbuka unatakiwa kujenga tabia na si kufanya kama roboti. Haya yanatakiwa kutoka ndani ya moyo wako. Unatakiwa kuwa halisi na sio kuigiza vinginevyo hutapata matokeo mazuri.

Tabia 8 Kuu za Kupendwa na Watu

Kuna mambo mengi ambayo yanachangia kupendwa lakini haya ni yale ambayo nimeyaona yanamchango mkubwa na kama yakifanywa kwa ukamilifu yataweza kukupa matokeo mazuri na ukafanikiwa sana katika kuishi na kufanya kazi na watu sehemu yoyote iwe ni kazini nyumbani au sehemu nyingine za kijamii.
  1. Gusa nyoyo zao-Shiriki Hisia zao

Binadamu wanaongozwa na hisia zaidi,maamuzi mengi bado yanategemea hisia kuliko utashi.
Ingia katika nyoyo zao na ufahamu nini kimo ndani na uwe mshiriki.
Fahamu kuhusu afya zao kwa kwenda zaidi ya salamu ya kawaida. Uliza juu ya watu wanaowapenda sana na wanaomaanisha maisha yao kama watoto,wenza au wazazi.
Uliza maswali kama “Watoto wanaendeleaje? Wako darasa la ngapi?” ukiweza taja majina yao katika mazungumzo “John na Maria wanaendeleaje? Wameanza shule?”
Kama ni kazini ulizia kuhusu mradi wa mfanyakazi mwenza wako, “Umefikia wapi na mradi wako wa kutokomeza malaria?”
Shiriki katika mambo ya kijamii,sikukuu za kuzaliwa,misiba na sherehe kama harusi.
  1. Kuwa Msikivu

Katika mazungumzo,jenga tabia ya kusikiliza zaidi kuliko kuongea. Ongea pale mwingine anapokuwa amemaliza kusema. Usifanye kitu chochote kingine ukiwa unaongea na mtu kama vile kutuma ujumbe katika simu na muangalie usoni. Kwa namna hii unaonesha kujali anachosema na hukupandisha katika alama za kupendwa.
Kama uko katika nafasi za uongozi iwe nyumbani,kazini au sehemu nyingine,toa nafasi kwa watu kuongea na kutoa mawazo na hisia zao,kisha toa mtazamo wako au ushauri juu ya suala husika. Wakati unafanya hivyo usioneshe hata kidogo kuwa mawazo yao hayana maana. Sababu kila jambo lina maana,kama simkwako basi kwa aliyeliongea. Jali mawazo ya kila mtu.
  1. Kuwa Mkweli na Timiza Ahadi

Sema kweli mara zote,ukweli utalkuweka huru lakini kubwa zaidi watu watakupenda na watakuwa wakweli kwako pia.
Ahidi kilichopo ndani ya uwezo wako na utimize kwa wakati uliosema kuwa utafanya.
  1. Onesha Mfano,Tembea Katika Maneno Yako

Ongoza kwa mfano,fanya yale unayoamini na unayoyasema. Katika nafasi za uongozi ni vizuri kufanya japo kwa kiasi fulani kile unachowapangia wengine kufanya. Katika mazingira ya nyumbani unaweza ukaamua kulisha mifugo wikiendi mojaau kukata majani viungani.
  1. Toa Msaada

Saidia pale inapowezekana. Saidia wasiojiweza kama katika majumba ya kutunza wazee,walemavu au watoto wenye mazingira magumu.
Saidia ndugu na jamaa katika shida zao za msingi kama elimu au masula mengine ya kijamii kama misiba na magonjwa .
Saidia watoto katika masuala yao ya masomo,unaweza kuchagua somo moja kama kiiengereza au hesabu na kuwafundisha angalau kwa wiki.
Msaidie mweza wako katika kazi mbalimbali nyumbani. Kama wewe ni Baba basi msaidie mkeo kazi za nyumbani kama kufua kunyosha n.k kila inapowezekana.
  1. Toa Shukurani na Pongezi

Shukuru kwa kila jambo zuri hata kama likiwa dogo kwa namna gani. Sema “Asante” neno hili lina maajabu makubwa ambayo hatuyatumii inavyopaswa.
Kushukuru kunaonesha kujali juhudi za mwingine na zinafanya urahisi wa kupata tena siku nyingine au mara nyingine. Inasemwa kuwa kushukuru ni kuomba tena.

Kutoa pongezi ni namna nyingine ya kuvuta upendo toka kwa watu. Katika kila kizuri kinachofanya na mtu usisite kutoa pongezi. Unapopongeza huongeza nguvu na jitihada kwa mlengwa na kuweza kufanya bora zaidi.
Wapongeze watoto kwa kufanya vizuri shuleni au mwenza wako kwa kupendeza na kuwa mke au mume mwema na msaidizi mzuri kwako.
  1. Kuwa Halisia

Unesha uhalisia katika maneno yako na mwonekano wako. Usifanye mambo yaliyo nje ya uwezo wako na yasiyoonesha hali au uwezo wako halisi. Usilazimishe kuishi kitajiri au kisomi wakati sio kweli. Ishi ndani ya uwezo wako na onesha sura halisia kwa watu.
  1. Tabasamu

Tabasamu halimtupi mtu,onesha furaha kwa watu. Tabasamu unapoongea nao na bila shaka watatabasamu pia. Kuna maajabu makubwa katika kitendo hiki. Jaribu leo na uone, kwa kila utakayempa tabasamu ni lazima atafanya hivyo hivyo kwako-ni uhakika.

Tabia za Kupendwa na Watu Zinafundishika

Kupendwa na watu ni jambo muhimu sana katika maisha ya mtu yeyote. Ni muhimu katika utendaji wa majukumu yako ya kila siku iwe kazini,nyumbani kama mwanafamilia na katika mambo mengine ya kijamii na zinafundishika
Ukipendwa na watu ni rahisi kutoa ushawishi juu ya mambo utakayoyatoa kwao. Katika kutafuta masoko,uongozi wa watu au siasa kupendwa na watu ni jambo la muhimu sana.
Fuata mbinu hizi kujenga tabia zitakazokufanya kupendwa na watu siku zote.

Madhara ya Kupongeza Watoto-Kama unafikiri umekuwa ukifanya vyema basi fikiri tena.

pongezi_kwa _mtoto_3
Je wewe ni mzazi au mlezi,au mwalimu? Je unafanyaje mtoto wako au mwanafunzi anapofanya vizuri katika kazi zake? Najua wengi mtampongeza kwa namna tofauti. Maneno kama “wewe ni bora kuliko wote”,”una akili sana” n.k.

Lakini unafahamu madhara ya kupongeza watoto? Ukweli ni kwamba kuna madhara makubwa kwa kutoa pongezi za aina hii kwa watoto kuliko ambavyo unaweza kufikiria. Kuna faida kwa muda mfupi tu na madhara makubwa siku za mbeleni.

Watoto watafurahi sana watakapopongezwa, mfano “hongera sana, umepata “A” hakika wewe ni mtoto mzuri sana” mtihani unaofuata mtoto anapopata alama ”C”,unajua atakachofikiri? atakufa moyo sana na kujiona kwamba “yeye si bora”,”si mtoto mzuri” sababu hakuweza kupata alama “A”.
Atajisikia vibaya na pengine hata kudanganya juu ya matokeo yao kwasababu hatapenda kusikia vinginevyo toka kwa mzazi wake.

Wataalamu wa saikolojia ya watoto wanashauri kupongeza watoto kwa njia tofauti na zile ambazo tunazitumia sana kama nilivyoeleza hapo juu. Badala ya kupongeza matokeo peke yake badala yake tuangalie njia na jitihada walizotumia kufikia matokeo hayo ya mwisho na kutoa maoni yetu inavyofaa.

Njia iliyo bora zaidi kumpongeza mtoto aliyepata alama “A” kwa mfano ingekuwa kumpongeza kwa jinsi alivyosoma kwa muda mrefu na kuuliza maswali kwa walimu na wazazi ambavyo vimefanya kufikia matokeo hayo-“Hongera sana,uliweka muda mwingi sana na umesoma kwa bidii,hakuna nguvu zinazoenda bure,unastahili matokeo haya”.
Kwa kusema hivi unamfanya mtoto aelewe kuwa kumbe mafanikio yanakuja kwa kufanya kazi na wala si kwa bahati mbaya au njia za mkato kama ambavyo kushindwa hakuji kwa bahati mbaya pia.
kupongeza-watoto_kujifunza
Pongezi ziendane nakuainisha juhudi na njia zilizopelekea mafanikio
Pale mtoto anapofanya vibaya ni jukumu la mzazi au mwalimu kutoa maoni yake ya kweli kwa mtoto. Sema mfano “unajua kuna wanafunzi wengi darasani kwako ambao wanasoma kwa bidii pia kama wewe,hivyo ili upate matokeo bora zaidi kuliko haya inakupasa kuongeza jitihada ili uwe moja ya kati ya wale wanaofaulu zaidi”.

Usiseme maneno ambayo yamvunja moyo wa kupenda masomo au kazi zake. Kama ambavyo pongezi zinaumiza lawama zina madhara makubwa zaidi. Hivyo tafuta jinsi ya kufanya kwa kipimo au kiasi kinachofaa. Maneno kama “wewe ni mjinga wa kwanza,unaniabisha sana” au “wewe huwezi kufanya sayansi” yanashusha kujiamini na uwezekano ni kuwa mtoto ataendelea kufanya vibaya.
kupongeza-watoto_lawama
Lawama pekee bila kuonyesha njia ya kuondokana na kushidwa hupelekea mtoto kushindwa zaidi

Ujumbe mkuu hapa ni kuwa pongeza kwa jinsi ambavyo mtoto ataelewa kuwa amefanikiwa kwa sababu alifanya kitu fulani. Kuwa matoke mazuri yanatokana na kufanya baadhi ya mambo kama kusoma kwa bidii,kufanya majaribio mengi,ushirikiano na wanafunzi wengine n.k.
Hiyo italeta maendeleo endelevu na pale atakapo anguka atajua hakufanya yale yanayostahili kuleta matokeo mazuri.

Nakutakieni malezi mema!!!.

Tafadhari toa maoni yako hapa chini,shiriki nasi yale ambayo umekuwa ukifanya kwa watoto wako katika kupongeza na kushauri pale wanapofeli katika kazi.

Faida ya Kutengeneza Bajeti ya Nyumbani


Faida ya Kutengeneza Bajeti ya Nyumbani
Kutengeneza bajeti ya nyumbani inaweza kuwa ni mawazo kutisha kwa watu wengi. Watu wengi huangalia bajeti ya nyumbani kama kitu ambacho huzuia kufanya mambo yao. Katika hali halisi bajeti ni chombo ambacho kitakusaidia kukuongoza wewe kifedha katika kufanya manunuzi na mambo mengine ya kimaendeleo yanayohitaji fedha.
Mojawapo ya mambo muhimu kwa ustawi wako wa kifedha katika familia ni kuweza kutengeneza bajeti na kufuata.
Watalamu wa falsafa za mipango wamesema “Usipopanga basi unapanga kushindwa” . Ili uweze kupima mafanikio yako basi sharti uwe umepanga nini ufanye kwanza.
Zifuatazo ni faida utakazozipata kwa kuwa na bajeti ya ndani:

Faida 5 za Kutengeneza Bajeti ya Nyumbani

1. Udhibiti wa fedha zako kwanza

Udhibiti wa fedha zako na za familia ni kitu muhimu sana. Ukijua kiasi gani cha fedha unaingiza na kiasi gani unatoa itakusaidia sana kufanya maamuzi sahihi juu ya fedha zako.
Badala ya kuelekeza nguvu juu ya jinsi ya kutengeneza pesa zaidi, unaweza kupunguza matumizi yako yako.Kuwa na bajeti kutakuonyesha unatumia fedha kwenye vitu gani na hivyo itakusaidia kujua wapi upunguze hivyo kukupa uwezo wa kufanya maamuzi bora.

2. Tengeneza mpango fedha(“Financial Plan”)

Hakuna mtu anataka kufanya kazi sikuzote za maisha yake . Bajeti itakusaidia kuanza kutengeneza Mpango Fedha , ili uweze kuhakikisha kwamba unafikia malengo yako ya kifedha. Tunafanya kazi kwa wastani wa miaka 35-40 ya maisha yetu, hivyo kwa nini tusifanye fedha zetu sisifanye kazi kwa ajili yetu badala ya kuzitumia kwa matumizi ambayo si ya msingi sana na kutufanya tuwe masikini daima?.

3. Itakupunguzia msongo wa mawazo

Kama unajua wapi fedha yako inakwenda kila mwezi , utakuwa hutakuwa na shida juu ya kutumia fedha au hata kutokuwa nazo za kutosha.
Mara baada ya kuwa na uelewa mzuri wa hali yako ya kifedha na kuanza kufanya baadhi ya mabadiliko , hutasumbuka sana juu ya kipato chako cha kila mwezi.

4. Ishi kwa kipato chako

Kumbuka bajeti inatuambia nini tunaweza kumudu kununua , lakini haiwezi kukuzuia kununua. Hivyo kama hufuati haifanyi kazi, unahitaji kuiheshimu na kuifuata.
Unapojua nini unamudu katika mwezi inakufanya uanze kuishi kwa kipato chako na hivyo kuishi bila madeni.

5. Kugundua nini ni muhimu

Unapoweza kuona fedha inayoingia na kutoka kila mwezi ,unaweza kuanza kuona kwamba baadhi ya mambo si muhimu sana na hivyo itakupunguzia msongo wa mawazo juu ya wapi upate fedha ya ziada kama vile kuazima au kufanya kazi masaa mengi zaidi ambayo mwishowe itakuweka mbali na familia na kuhatarisha afya yako
Fahamu kwamba kutengeneza bajeti ya familia inaweza kuchukua muda mrefu . Lakini mara ukianza utaona jinsi hali yako ya kifedha inavyoboreka .
Kuna sababu nyingi za kutengeneza bajeti zaidi ya zilizosemwa. Kama hujaanza,unasubiri nini? Anza leo na uone faida zake kwako binafsi na kwa familia yako

Njia 5 za Kudumisha Mahusiano ya Mapenzi


wapenzi
Kuna nukuu inayosema “Uhusiano mzuri hautokei tu peke yake bali huchukua muda, uvumilivu, na watu wawili ambao kikweli wanataka kuwa pamoja.”

Japo inasemwa kuwa mapenzi hayana njia moja ya kufuatwa lakini kuna vitu ambavyo vinajulikana kuchangia katika kuboresha mahusiano baina ya wapenzi.
Mahusiano ya mapenzi yenye kudumu ni sharti yapandwe katika udongo wenye rutuba kama ulivyo mmea,yatahitaji maji ya kumwagilia na mbolea ya kukuzia.  Na zaidi ya yote yanahitaji muda wa kukua kabla matunda kuonekana.

Uaminifu
Kumwamini mwenza wako ni jambo la msingi sana katika kudumisha mahusiano. Usimshuku mpenzi wako kuwa si muaminifu bila ushahidi wowote.
Kushukiwa kukosa uaminifu pasipo ukweli inasononesha sana na kumkosesha raha mpenzi wako.
Imesemwa na wanafalsafa wa mawazo ya binadamu kuwa “Unachofikiri na kuamini kinatokea” hivyo unashauriwa kutofikiri vibaya juu ya mpenzi wako kwani haileti afya katika mahusiano.
Hali kadhalika na wewe uwe mwaminifu na mwenye kusema kweli mara zote. Ongeeni juu ya mipango na mawazo yenu bila kufichana.
Watambulishe kwa mpenzi wako ndugu ,jamaa na marafiki wakaribu ili kumpa mwenza wako amani.

Weka muda kwajili ya Mwenza wako.
Mahusiano mazuri kati ya wapenzi yanahitaji muda wa wapenzi hao kukaa pamoja. Wapenzi wasio na muda wa kukaa wana hatari ya kupoteza mvuto wa mahusiano yao na hivyo kuhatarisha uhai wa mapenzi kati yao.
Kama wapenzi wapo mbali mbali basi wanahitaji kuweka muda wa kuongea kila inapowezekana.
Tafuta muda wa kutoka pamoja,hata kama mtaenda mkahawani kunywa chai au juisi tu,inatosha sana na inawaweka karibu zaidi.

Mawasiliano
Mawasiliano ni muhimu sana baina ya wapenzi.
Hata kama umebanwa na kazi pata dakika chache za kuongea na mpezi wako na kumtaka hali. Andika hata ujumbe wa maneno au barua pepe. Mwambie mpenzi wako ulipo kila mara inapobidi ili kumjengea imani na wewe na kumpa amani moyoni. Tuma ramani ya mahali ulipo kama unatumia simu ya “Smart” (Tuma location kwenye whatsapp)
Mawasiliano ni ufunguo wa kudumisha upendo.
Wakati kuwasiliana na mpendwa wako, kumbuka kwamba upendo ni muhimu. Ongea toka moyoni na si kwa ajili ya kutimiza wajibu tu,kwani mpezi wako atajua tu kama hakuna mahaba katika mawasiliano yenu hivyo kutoleta faida ile inayotegemewa.
Mawasiliano mengine ni yale ya kuelezana yaliyo moyoni. Mweleze mwenza wako linalokusibu ili kupata ufumbuzi wa pamoja. Wapenzi wanaoongea kwa utulivu siku zote watakuwa pamoja.
Zawadi
Tafuta kitu cha kumpa mpenzi wako. Si lazima kiwe na thamani kubwa.Inaweza ikawa pipi au matunda tu.
Mnunulie zawadi kila inapowezekana hasa unaposafiri au katika siku yake ya kuzaliwa.

Onyesha Upendo wako
Kila mtu anajinsi yake tofauti ya kuonyesha upendo, lakini vyovyote itavyokuwa ni jambo la muhimu sana kuonyesha hisia zako kwa mpenzi wako.
Mara nyingi wapenzi wa muda mrefu wanasahau juu ya hili.
Maneno kama “Nakupenda”au majina ya mahaba kama “Mpenzi” au ”La-azizi” yanachangia sana kuonyesha mapenzi na kumfanya mwenza wako kujisikia vizuri.
Maneno haya yanaposemwa kwa hisia halisi na toka moyoni yana mchango mkubwa katika kuboresha mahusiano

Hatua 5 za Uhusiano wa Mapenzi: Wewe upo Katika Hatua Ipi?

Hatua 5 za Uhusiano wa Mapenzi: Wewe upo Katika Hatua Ipi?

uhusiano-wa-mapenzi
Kwa nini baadhi ya mahusiano ya mapenzi  huvunjika na mengine hudumu daima?
Je, umewahi kujiuliza “Kwa nini ni uhusiano wetu una shida sana? Mambo yalikuwa mazuri sana tulipoanza,nini kimetokea?
Jibu ni kwamba mnaweza mkawa mmetoka katika hatua moja na mko katika hatua nyingine ya mapenzi.
Uhusiano wa mapenzi hupitia katika hatua kubwa 5 zinazoenda katika mfuatano,na wakati ungine kujirudia. Ni muhimu sana kwa watu ambao wapo katika uhusiano wa mapenzi kufahamu hatua hizi ili kuweza kukabiliana na changamoto zake ili kufanikisha mahusiano yao.
Katika kila hatua kuna changamoto zake. Watu tofauti hutumia muda tofauti katika kila hatua. Wengine huenda kwa haraka na wengine hukaa katika kila hatua au baadhi yake kwa muda mrefu zaidi.
Makala hii inaonesha hatua hizi na kuangalia changamoto katika kila hatua na jinsi ambavyo wapenzi wanaweza kukabiriana nazo.
Hapa ni hatua 5 ya uhusiano kama ambavyo imebainishwa na watafiti katika mahusiano ya wapenzi:
1. Mahaba(“Romance”)
2. Uhalisia na Ugomvi
3. Kujitathimini na Kujitambua
4. Kujirudi na Utulivu
5. Makubaliano na Kujitoa
Hatua mbili za mwanzo ni hatua ngumu na wapenzi wengi wanaishia hapo. Hivyo ni hatua ambazo wapenzi wanahitaji kuzizingatia zaidi na kujipanga kukabiliana na changamoto zake.

Hatua #1: Mahaba (Ulevi wa Kupenda)

uhusiano-wa-mapenzi_mahaba
Ni asili kila mtu kupenda. Hii ni hatua mabayo kila binadamu anapitia.
Kila mtu anahitaji mtu wa jinsia nyingine kuwa mwenza wa maisha yake. Mapenzi ni mojawapo ya mahitaji mengi ya kimwili, kihisia na hata kiroho kwa mwanadamu.
Mara nyingi tunakutana na watu ambao tunatofautiana sana kuliko kulingana. Hii ni wazi kutokana na kukua katika familia na mazingira tofauti. Kama tofauti hizi zingefahamika mapema basi watu wengi wasingeingia hata katika hatua hii ya awali.
Sayansi ya Kupenda:
Unapoingia katika mapenzi na mtu ubongo wako unatengeneza mchanganyiko wa kemikali na kuziachia mwilini. Kemikali hizi ni pamoja na Oxytocin, Phenylethylamine na Dopamine. Kemikali hizi huongeza mapingo ya moyo na kusisimua mwili. Na hali hii ndiyo tuyoita mapenzi au mahaba.
Hali hii ni sawa kabisa na ile ambayo watumiaji wa madawa ya kulevya wanaipata.
Kama walevi wa madawa,mtu ambaye ameingia katika mapenzi anaanza kuona vitu tofauti ni uhalisia. Vitu vinaonekana ni vizuri sana na ubaya unajificha kabisa. Unaona vile vitu vizuri tu ambavyo vinakufanya ujisikie vizuri na kupuuza vyote ambavyo vinakufanya ujisikie vibaya.
Ulevi huu unakufanya uone vile vitu ambavyo wewe na mpenzi wako mnafanana na kutupilia mbali vile vyote mnavyotofautiana na vibaya.
Unakufanya pia useme na kufanya vile ambavyo vinampendeza na kumfurahisha mpenzi wako pekee.
Hali hii itaendelea mpaka kilevi kikiisha nguvu na huweza kuchukua muda wa miezi 2 hadi miaka 2. Katika hatua hii, ubongo wako unaaacha kuzalisha kemikali hizi za mapenzi na unajikuta unashangaa ilikuwaje umekuwa na mtu huyo.

Hatua #2: Uhalisia na Ugomvi (Mapambano ya Mamlaka)

uhusiano-wa-mapenzi_uhalisia
Asilimia kubwa ya talaka za ndoa na kuvunjika kwa mahusiano hutokea hapa. Ni kipindi cha miaka 3 na 4.
Watu wanaanza kuona mambo kwa uhalisia na mnagundua hamfanani na mnatofautiana sana.
Hiki ni kipindi kigumu kwa wapenzi wengi,ni kipindi cha kukata tamaa na hasira. Ni kipindi ambacho ndoto zenu za kupendana daima zinaingia dosari.
Hivyo, unapata kazi ya kuanza kujaribu kumbadirisha mwenza wako ili awae kama ulivyofikiri alikuwa au kama ambavyo ungependa awe.
Ugomvi na na hata kupigana kunatokea katika hatua hii.
Hatua hii inaweza kuchukua miezi michache hadi miaka mingi, kutegemea na hatua ambazo wapenzi hao wanazichukua au kupata masaada toka kwa wengine.
Bila maarifa ya kupambana na ugomvi huu wa mamlaka na kutatua tofauti zao na kujitambua,wapenzi watarudi katika hatua hii mara kwa mara katika uhusiano wao.
Namna ya Kukabiliana na Hatua Hii
Kuna njia kadhaa ambazo wapenzi wanaweza wakachukua kukabiliana na matatizo yao wao wenyewe au kwa msaada wa watu wengine wa nje.
  1. Kukubali na kufahamu tofauti ya kila mmoja
  2. Kujifunza kugawana mamlaka, na kutambua kwamba kutumia nguvu kamwe hakutasaidia kupata unachokitaka
  3. Kutambua nafasi yako katika mahusiano
  4. Kukubaliana na maisha kwa jinsi yalivyo
Vyovyote vile ilivyo kukabiriana na kushinda hatua hii si kazi rahisi na walio wengi wanashindwa na kuvunja mahusiano ya muda mrefu.
Ukweli ni kwamba kushinda hatua hii ni muhimu sana kushirikisha na kupata msaada wa watu wengine,iwe ni ndugu rafiki au wataalamu wa ushauri wa mahusiano.

Hatua #3: Kujitathimini na Kujitambua

uhusiano-wa-mapenzi_Kujitahmini
Katika hatua hii kila mmoja anajitathmini kama anahitaji kuendelea na mahusiano au la.
Wapenzi wanatengeneza utengano kati yao na upendo unapungua sana kipindi hiki. Kujitenga na kuwa mbali kihisia kunatokea kati yao.
Ni rahisi kwa wapenzi kudanganya na kujihusisha na wapenzi wengine.

Hatua #4: Mapatano

uhusiano-wa-mapenzi_mapatano
Baada ya kipindi kirefu cha tathimini na wakafanikiwa kubaki pamoja,wapenzi wanatambua namna ya kushughulikia matatizo yao kwa namna ambavyo wote wanafaidika.
Katika hatua hii, hatimaye inakuwa wazi kuwa huwezi kubadili tabia ya mwenza wako na unaamua kumpokea na kumpenda kama alivyo.
Unakubali ukweli kuwa mpenzi wako yuko tofauti na wewe. Mnaamua kuweka mipaka yenu wazi na kujifunza kuheshimiana. Kama hii haiwezekani basi mnarudi tena katika hatua ya nyuma ya ugomvi.
Msisimko wa kuwa katika mapenzi unarudi zaidi ya ilivyokuwa katika hatua ya kwanza.
Katika hatua hii hasa ndio unakuwa tayari kuingia katika ndoa na kuwa na mipango ya pamoja ya muda mrefu.

Hatua #5: Makubaliano na Kujitoa

uhusiano-wa-mapenzi_makubaliano
Katika hatua hii ya uhusiano wa mapenzi wapenzi wanakuwa wameamua kuwa pamoja na kama timu wanafanya mambo pamoja.
Wapenzi wanapendana ki kweli na wameamua kuwa pamoja ukiachia tofauti zao.
Wapenzi wanakuwa marafiki katika hatua hii. Inasemekana asilimia ndogo sana ya wapenzi wanafika katika hatua hii (inakadiliwa kuwa chini ya 5% ya wapenzi wote)

Kuhitimisha..

Hatua hizi haziendi moja ka moja katika mfuatano. Mara nyingi huenda mbele na kurudi nyuma tena kama wapenzi hawazingatii na kuelewa mambo ya muhimu ya kukabiliana na changamoto za jatua husika.
Wapenzi wengi wanafunga ndoa wakiwa bado katika hatua za mwanzo. Wengi wanakuwa katika ulevi wa mapenzi na wanaishia kuachana. Ni muhimu sana kupitia hatua hizi na kuzifahamu.
Unapofahamu changamoto za kila hatua ni rahisi kwa wapenzi kuwa wavumilivu na kutafuta mbinu za kuatatua matatizo yao na kukua katika uhusiano wa mapenzi.
Je unafahamu wewe na mpenzi wako mko katika hatua gani?
Tafadhali acha maoni yako katika kisanduku hapa chini.

Njia 4 za Kuzuia Migogoro katika Mahusiano

migogoro-katika-mahusiano-1
Migogoro katika mahusiano ya mapenzi ni kitu cha kawaida kutokea. Wenza katika mahusiano hugombana na ugomvi mwingine hupelekea hadi kupigana na kusababishiana maumivu hata kuumizana.
Lakini migogoro mingi inaweza kuepukika kama tu wenza hao wakitambua vitu vinavyosababisha kugombana kwao na kuweka mikakati itakayowasaidia kuishi kwa amani zaidi na kuifuata.
Mara nyingi katika mahusiano ugomvi hausababishwi na ujumbe au mawazo tofauti yanayotolewa na mmoja wao bali namna ujumbe huo unavyotolewa na jinsi mpokeaji anavyotafsiri.
Hii inamaana kuwa kama wenza hao wakikubaliana na wakawasiliana hoja zao katika namna ambavyo kila mmoja wao anahisi kusikilizwa na kujaliwa namba za magomvi zitapungua sana.
Hebu tuone namna ambavyo migogoro katika mahusiano inaweza kupunguzwa na kusuluhishwa:

Mbinu # 1: Acha Kujihami

migogoro-katika-mahusiano_boxing
Mapambano kati ya wenza wawili yanaweza kufananishwa na mpambano wa mchezo wa ngumi. Bondia mmoja anapotupa makonde mfululizo na mwingine anajaribu kuzuia ni kawaida atakuwa narudi nyuma na kuruhusu mwenzake aendelee kumvamia.
Vivyo hivyo katika ugomvi katika mahusiano ya wapenzi. Mwenza mmoja napomvamia mwenzake kwa maneno makali na tuhuma kwa mfano, na mwingine akawa anajihami nayo kwa kupinga au kwa kurudisha tuhuma,kinachotokea ni kuwa mapambano yataendelea.
Kama unatengeneza mazingira ya kujihami na mpenzi wako basi unafanya aendelee kukushambulia na hivyo kuendeleza mgogoro kwa muda mrefu.
Zuia kujihami na toka katika uringo wa mapambano. Kumbuka bondia hawezi kupigana na upepo,kama hakuna mpinzani basi hakuna pambano.
Epuka majibizano ya maneno ambayo yatapelekea ugomvi. Kuwa wa kwanza kukaa kimya,ikiwezekana kuondoka kwa muda huo na muendelee mazungumzo baadae wakati kuna utulivu na kusikilizana.

Mbinu # 2: Toa Nafasi ya Kusikiliza

migogoro-katika-mahusiano_usikivu
Kuna haja kubwa kwa binadamu yeyote kupenda kusikilizwa na kueleweka.
Mpenzi wako anapokuwa amekasirika au amepandwa na jazba au ameumizwa kihisia anapenda kusikilizwa shida yake na apate kueleweka.
Unahitaji kutoa nafasi ya kusikiliza na kuelewa nini anafikiri au kuhisi moyoni. Jaribu kurudia kile alichosema kumhakikishia kuwa umemsikia vizuri. Pia inaonyesha kuwa unajali. Mpenzi yeyote anapenda kuona kuwa mawazo yake na yeye mwenyewe yanajaliwa.
Unaporudia kutamka alichosema kuna maana mbili, ya kwanza ni kuwa umemsikia vizuri lakini pili ni kuwa inaonyesha kuwa unajali.
Mfano: “Najua jambo hili ni muhimu kwako,lakini nafikiri tungeangalia mambo yanayohusu watoto na mahitaji yao kwanza na hilo lifanyike baade”
Jaribu mbinu hii kwa mwenza wako mnapokuwa na migogoro na uone jinsi inavyofanya maajabu.
Kumbuka sauti inayotumika iwe yenye kuonyesha kujali na sio kuongea kama vile ni polisi.

Mbinu # 3: Chukua Wajibu

migogoro-katika-mahusiano_wajibu-1
Tatizo linapotokea na likazusha mgogoro ni jambo la busara kwa mmoja wenu kukubali kuwajibika katika suala hilo na sio kurushiana lawama kila mmoja akimlaumu mwenzake kuwa amekosea.
Kama mmoja wao akikubali kuwa ni kosa lake,hakutakuwa na ugomvi tena. Wengine hukubali kosa hata kama si lao ilimradi tu kuwe na amani. Utasikia mtu akisema “Nakubali yaishe..”
Mfano:
i. Mapambano
Mke: “Tumelala bila kufunga milango leo,kwanini hukuangalia milango kabla hatujalala?”
Mme: ”Hilo ni tatizo lako,kwanini wewe ndio ulikuwa wa mwisho kuingia”
ii. Kuwajibika
Mke: “Tumelala bila kufunga milango leo,kwanini hukuangalia milango kabla hatujalala?”
Mme: ”Ahh.. Samahani! Ni kweli kama baba wa nyumba ni jukumu langu kuhakikisha usalama wa nyumba. Nitakuwa makini zaidi,ni kosa langu”
Katika mfano wa kwanza ni lazima mabishano yataendelea,na usishangae yakaishia hata kupigana. Lakini katika mfano wa pili,mgogoro umeisha,sana sana watacheka na kukumbatiana.

Mbinu # 4: Kusimama Pamoja

migogoro-katika-mahusiano_umoja-2
Mapambano mengi baina ya wapenzi husababishwa na kuvunjika kwa mawasiliano. Kunasababishwa na kutoelewa madhumuni ya mwenza wake.
Kutoelewana ni adui ambaye anaweza kuwasambaratisha wapenzi,na wakaharibu mahusiano yao.
Ni muhimu sasa kwa wapenzi kwa pamoja kushambulia KUTOELEWANA.
Kutoelewana kunapotokea ni muhimu kupeana nafasi ya kufafanua maana ya maneno yake ya awali au matendo yake.
kwa namna hii utaweza kufahamu madhumuni yake.
Kufaninisha hili ni lazima kuwa msikivu(Mbinu #2) vinginevyo utakosa kusikia ufafanuzi wake.
Ni muhimu kutumia neno “SISI” na siyo “MIMI” katika kufafanua mazungumzo yenu.
Mfano:
Mme:”Ni kweli tumelala bila kufunga milango,ila wote tulikuwa tumechoka sana na kazi za siku nzima,tuwe waangalifu zaidi siku zijazo”

Fanyia Kazi..:

Hebu tumia mbinu hizi nne rahisi kabisa katika kutatua migogoro katika mahusiano yako, ni hakika kuwa utafanikiwa sana na kuleta amani na maelewano na mweza wako.
Kumbuka hakuna mshindi katika mabishano yanayotokea katika mahusiano yako,wote mnapoteza. Mkilitamba hili kwapamoja mtasimama pamoja na mtaangalia mbinu sahihi ambazo zimetajwa katika makala hii kuwasaidia kuondokana na migogoro katika mahusiaono yenu.
Je huwa unagombana na mpenzi wako mara kwa mara? Najua jibu la wengi ni ndiyo. Basi jaribu mbinu hizi nne zilitotajwa na uone matokeo yake.
Kama una maoni juu ya mada hii,tuandikie mawazo yako katika kisanduku cha maoni hapa chini . Pia tutumie mbinu nyingine ambazo unazitumia na zinafanya kazi ili tufaidik

Njia 7 za Kufuata Kuleta Suluhu za Mifarakano Katika Mahusiano

Njia 7 za Kufuata Kuleta Suluhu za Mifarakano Katika Mahusiano

mifarakano-katika-mahusiano
Migongano na tofauti kati ya watu wawili katika mahusiano ni kitu kisichoepukika iwe ni mahusiano ya mapenzi ,mahusiano ya mzazi na mtoto na hata mahala pa kazi. Sababu za mifarakano katika mahusiano ziko wazi;kwamba watu hawa wametoka na kukulia katikla mazingira tofauti na hivyo tabia na hulka zao ni lazima zitatofautiana.
Katika hali kama hii migongano na kutoelewana wakati mwingine ni vitu ambavyo vinatokea na kunahitajika busara na mbinu mahususi za kukabiliana na tatizo hili

Njia 7 Muhimu za Kutatua Mifarakano Katika Mahusiano

1. Kuwa wa Kwanza Kuchukua Hatua

Kunapotokea kufarakana kati ya watu wawili kwa kawaida mawasiliano huvunjika au kuwa magumu na mabaya. Kila mmoja anaweza akwa na kinyongo na mwingine. Kwa wapenzi hali hii inaweza ikawa ya kuumiza zaidi kwani inahusisha hisia kwa kiasi kikubwa;ni jukumu lako wewe kufunja ukimya na kuwa wakwanza kuleta suluhu.
Tafuta nafasi na omba kujadili na kuongea kuhusu tofauti zenu.

2. Anza Kwa Kuangalia Kosa Lako Kwanza

Ni kawaida katika ugomvi na mifarakano kwa mmoja kumuona mwenzake kuwa ndiye mkosaji,na kusahau kuwa huenda kosa likawa upande wake pia. Kama suala hilo limemuudhi mwingine pia huenda kuna tatizo toka kwako pia,au labda yeye anaona kuna tatizo upande wako.
Kutambua hilo unahitaji kujihakiki mwenyewe kwanza na kumsikiliza mwenzio kama ana hisia gani. Kama utaona kuna shida upande wako pia basi ni wakati wa kuomba msamaha kwa nafasi yako kwanza.

3. Sikiliza kwa Umakini Shida na Mtazamo Toka Upande wa Pili-Vaa Viatu Vyake

Inasemwa kuwa sababu kubwa ya malumbano na ugomvi ni kuwa tunataka kusema zaidi kuliko kusikiliza upande wa pili,na kwa kufanya hivyo tunakuwa wabinafsi.
Ukisikiliza vizuri toka upande wa mwingine na kujaribu kusikia hisia zake huenda ukaliangalia jambo husika katika namna nyingine ambayo itapelekea maelewano. Ni muhimu sana kuonesha kuwa unajali hisia zake.

4. Kuwa Mkweli na Maanisha Unachokisema-Sema toka Moyoni

Mdomo unaweza kutamka chochote bila kumaanisha,kweli hutoka moyoni. Unaposema kitu kwa hisia na kwa dhati unasikika zaidi. Ongea toka moyoni na maanisha unachosema na matokeo yake yatakuwa mazuri.

5. Jizatiti Katika Kusuluhisha Tatizo na Sio Kulaumu

Lawama hazisaidii kuleta suluhisho la tatizo mbele yenu,ukweli ni kuwa linasababisha upande wa pili kujihami,ni asili kwa mtu anayeshambuliwa kujihami hali kadharika katika mazungumzo.
Badala ya kulaumu ni vyema kama mtaangalia tatizo lenyewe ni nini na mzizi wake.

6. Kazania katika Kupata Maelewano na Sio Kumaliza Tofauti Zote

Si kitu rahisi mkamaliza tofauti zenu kwa kuwa ni watu wawili mliotoka katika mazingira yasiyofanana,badala yake mukubaliane namna ambazo mtaishi kwa amani na kuheshimu hisia na nafasi ya mwingine.
Kuwa tayari kukubaliana kutokubaliana katika baadhi ya mambo. Maelewano ndio jambo la msingi katika kuleta suluhu.

7. Kazania katika Kuonesha Kipi ni Sahihi na Sio Nani yuko Sahihi

Katika mifarakano si vyema kumtaja mwingine kuwa hayuko sahihi,kwasababu ya kwanza ni kuwa huenda wewe mwenyewe ukawa hauko sahihi lakini ya pili ni kuwa huko ni kurusha makombora ya lawama ambako kutamfanya mwingine kujihami na hivyo kutofikia maelewano.

 Jambo la Mwisho la Kuzingatia

Mnapotafuta suluhisho la ugomvi au mfarakano katika mahusiano ni muhimu kuzingatia vitu viwili vikubwa,kuondoa ubinafsi na kujishusha. Kwasababu ukosefu wa vitu hivi viwili ndio sababu kubwa katika mifarakano yote.
Na msingi upo katika kusikiliza hisia za mwingine. Usikivu ni bora zaidi kuliko kusema,unaposikiliza unaonesha kujali zaidi na inakuwa rahisi kufikia maelewano na kumaliza ugomvi na mifarakano katika mahusiano yoyote.
Je una mbinu nyingine unazotumia na zinafanya kazi? Changia ili kukuza uelewa kwa wasomaji wetu kwa kuandika katika kisanduku cha maoni hapa chin

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger