WADAU TUNAOMBA RADHI KAMA KUNA PICHA ITAKUKWAZA KUFUATIA AJALI HII ILIYOTOKEA LEO MKOANI SINGIDA.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela, akitoa taarifa ya
ajali ya Noah T.730 BUX kuongwa na Lori aina ya Scania T.687 AXB katika
barabara kuu ya Singida- Dodoma eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya
Ikungi wilaya ya Ikungi.Abiria 13 waliokuwa kwenye Noah wamefariki dunia
na watatu wamepata majeraha madogo madogo.Ajali hiyo imetokea
leo.(Picha na Gasper Andrew).
Baadhi
ya wakazi wa kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoa wa
Singida, wakitoa miili ya abiria wa Noah T.730 BUX waliofariki baada ya
gari hilo kugongwa na lori aina ya Scania T.687 AXB kwenye barabara kuu
ya Singida – Dodoma leo. Noah hiyo ilikuwa ikitoea Itigi wilayani
Manyoni akienda Singida mjini.(Picha na Nathaniel Limu).
Pichani
juu na chini ni Baadhi ya miili ya abiria wa Noah T,730 BUX waliofariki
leo kwenye ajali iliyotokea eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi
wilaya ya Ikungi baada ya kugongwa na lori T.687 AXB.(Picha na Nathaniel
Limu).
ABIRIA
13 wakiwemo watatu wa familia moja wamefariki dunia mkoani Singida leo,
baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah T.730 BUK, kugongwa
na Lori aina ya Scania.
Ajali
hiyo ya kusikitisha imetokea leo saa 1.32 asubuhi katika barabara kuu
ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya
Ikungi mkoani Singida.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida,SACP ,Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina
ya Noah lilikuwa likitokea Itigi wilaya ya Manyoni na lilikuwa na
safari ya kuja Singida mjini.
Amesema
hadi sasa miili ya abiria 10 wamekwisha tambuliwa na ndugu zao na miili
ya abiria watatu,bado haijatambuliwa na miili yote bado imehifadhiwa
kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida
Alitaja
waliotambuliwa na makazi yao kwenye mabano kuwa ni Omari Shaban (44) na
mke wake Salma Omari na mtoto wao Nyamumwi Omari (10) wote wakazi wa
Itigi mjini.
Kamwela
alitaja wengine kuwa ni Haji Mohammed (29) (Msisi),Mtunku Rashidi (68)
(Sajaranda),Salehe Hamisi (28) (Sajanranda),Samir Shaban (20)
(Puma),Mwaleki Nkuwi (35) (Ikungi),Athumani Kalemba (38) na Ramadhan
Mkenga (Sajaranda).Katika ajali hiyo,abiria watatu walinusurika na
kupata majeraha madogo madogo.
Amefafanua
juu ya ajali hiyo,Kamanda huyo alisema kuwa lori aina ya scania T.687
AXB wakati likipishana na noah,lilihama upande wake na kuifuata noah
ambayo ilikuwa upande wake wa kushoto,na kuligonga na kisha kuliburuza
kati zaidi ya 15.
“Kwa
sasa bado hatujajua chanzo cha ajali hiyo mbaya ingawa baadhi ya watu
wanadai kuwa huenda dereva wa lori alisisia na kusababisha lori hilo
kuhama upande wake na kufuata noah.Uchuguzi utakapokamilika,tutatoa
taarifa hiyo”,amesema.
Wakati
huo huo,mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini Singida,Dk.Banuba
Deogratius amekiri kupokea miili ya abiria hao 13 na kusema kati
yao,watoto ni wawili.
0 comments:
Post a Comment