Uamuzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga
ya Tanzania (TCAA) kupunguza safari za ndege za Shirika la Ndege la
Kenya (KQ) kutoka 42 hadi kufikia 12, kulingana na sheria za usafiri
wa anga zimeanza kuliathiri shirika hilo.
Tayari shirika hilo la ndege la
taifa la Kenya limetangaza kuwastaafisha marubani wake waandamizi 10,
ili kupunguza hasara itakayotokana na kupunguzwa kwa safari za ndege
za shirika la KQ, kutoka 42 kwa wiki hadi 12.
Taarifa iliyotolewa na shirika hilo
la Ndege Kenya kwa wateja imeeleza kuwa wamepunguza safari za kuja
Dar es Salaam kutoka 42 hadi 12 kwa wiki, na litasafiri mara mbili
kwa siku kuanzia jana 2015.
0 comments:
Post a Comment