MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga, leo
wameichabanga FC Platinum ya Zimbabwe mabao 5-1 katika mchezo wa Kombe
la Shirikisho barani Afrika.
Mchezo wa leo ni wa mzunguko wa kwanza wa kombe hilo kwa Yanga baada ya awali kuwatoa BDF XI ya Botswana kwa mabao 3-2.
Wafungaji wa mabao ya Yanga ni Salum Telela, Haruna Niyonzima, Amissi Tambe na Mrisho Ngassa (2) huku bao pekee la FC Platinum likiwekwa wavuni na Walter Musona
0 comments:
Post a Comment