UNYAMA: PADRI AMCHARANGA MAPANGA KIMADA ALIYEZAA NAE, HII NI AIBU...!!
Vitendo
vya kikatili vimekuwa vikitekelezwa katika sura mbalimbali, ila tukio
la mtumishi wa Mungu, Padri Celestine John Nyaumba, 35, kumgonga kwa
gari makusudi na kumcharanga mapanga mzazi mwenzake ni aibu isiyo na
mfano.
Padri Celestine, anayetoa huduma kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Homboro, Dodoma, anatuhumiwa kumtendea unyama huo, mzazi mwenzake, Selestina Anania Kibena, 35, Jumamosi iliyopita, Kata ya Kiluvya, Pwani.
Hii ni aibu isiyomithilika kwa sababu padri kufanya ukatili huo ni kashfa nzito, ongezea kwamba alimfanyia hivyo mzazi mwenzake, wakati kwa sheria za kanisa, ni mwiko kwa padri kujihusisha na mapenzi achilia mbali kufikia hatua ya kuzaa.
Aibu hiyo, inapata uzito zaidi kwa kuwa Selestina (mzazi mwenza wa padri), alikuwa mtawa (sister), lakini usista ulimshinda baada ya kupata mimba, takriban miaka minne iliyopita.
TUKIO LILIVYOKUWA
Padri Celestine, akiwa anaendelea na utoaji wa huduma kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, alipata nafasi ya kujiendeleza kimasomo, Chuo Kikuu cha Ardhi, Kitivo cha Ubunifu na Uchoraji wa Majengo, Dar es Salaam.
Akiwa Dar, Padri Celestine anaishi Mbezi Shamba, wakati Selestina ni mkazi wa Maili Mbili, Dodoma.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, mapema wiki iliyopita, Padri Celestine, alimwita Selestina, aungane naye Dar es Salaam, ‘wapumzishane’ kwa siku chache, kwani inadaiwa kwamba uhusiano wao wa kimapenzi ulikuwa unaendelea kwa siri.
MPANGO WA KIKATILI
Habari zinatiririsha mambo kama ifuatavyo:
Ijumaa iliyopita, Selestina aliwasili Dar es Salaam na kufikia nyumbani kwa Padri Celestine.
Siku hiyo (Ijumaa), walizungumza mengi, ikiwemo kupanga mambo mbalimbali kuhusu maisha yao na mtoto wao ambaye sasa ana umri wa miaka mitatu.
Siku iliyofuata (Jumamosi iliyopita), Padri Celestine, alimwomba Selestina, waongozane kwenda Kiluvya, Pwani.
Selestina hakuwa na shaka juu ya hilo lakini akataka sababu ya kwenda Kiluvya, badala ya sehemu nyingine.
Celestine akamweleza kuwa Kiluvya kuna sehemu nzuri ya kupumzika, vilevile ana jambo la kikazi atalifanya akiwa huko.
UKATILI UKATENDEKA
Ilipofika usiku wa siku hiyo (Jumamosi), Padri Celestine na Selestina, walianza safari ya kutokea Mbezi Shamba kwenda Kiluvya, wakiwa na gari aina ya Suzuki lenye namba za usajili T220 AJN.
“Walipofika Kiluvya, Padri Celestine ambaye alikuwa anaendesha gari hilo, alikata kushoto kuelekea porini. Gari likiwa porini kabisa, Padri Celestine alisimamisha kisha akamwambia Selestina ashuke kuangalia chini, kwani alihisi kuna tatizo,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Selestina alishuka akainama chini kwenye uvungu wa gari kuangalia tatizo, ile anafanya hivyo tu, Padri Celestine aliendesha gari kwa spidi ili amgonge Selestina. Bahati nzuri Selestina aliruka lakini gari lilimgonga kwenye paja la kushoto.
“Baada ya hapo, Celestine aligeuza gari amgonge tena lakini Selestina alijirusha sehemu yenye kishimo fulani hivi, kwa hiyo gari lilikuwa haliwezi kumfikia. Kuona hivyo, Padri Celestine alianza kumpiga mawe Celestine.
“Pengine aliona yale mawe hayana uzito wa kutimiza kile ambacho alitaka kukifanya kwa Selestina, kwa hiyo Padri Celestine alifuata panga kwenye gari, akamfuata Selestina, akamcharanga mapanga kichwani, kwenye mikono yote miwili na mguu wa kushoto.
“Kabla hajaendelea zaidi, Selestina alimrukia, purukushani ikaendelea. Padri Celestine alimng’ata Selestina katika shavu la kushoto, mwanamke huyo naye akajibu mapigo, akamng’ata padri katika shavu la kulia.
“Baada ya purukushani ya muda mrefu, Padri Celestine aliona mambo magumu, ikabidi amwombe msamaha Selestina kwamba shetani alimpitia, akamwomba ampeleke hospitali.
“Selestina alikubali lakini ile Padri Celestine anafuata gari, Selestina alijitutumua na kukimbia mbali zaidi, Padri Celestine aliporudi pale alipomwacha, hakumwona tena.”
HOSPITALI NA POLISI TUMBI
Chanzo chetu kilisema: “Selestina alijivuta mpaka Hospitali ya Mkoa wa Pwani, Tumbi. Vilevile alitoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Tumbi.
“Polisi walianza kufanya upelelezi wao na kufanikiwa kumkamata Padri Celestine, Jumapili iliyopita jioni.”
RPC ANENA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alikiri kutokea kwa tukio hilo na akafafanua kwamba baada ya Padri Celestine kuhojiwa, alisema alipitiwa na shetani kutokana na usumbufu aliokuwa anaupata kutoka kwa Selestina.
Kamanda Matei alisema, Padri Celestine alidai kuwa Selestina alikuwa anamuomba fedha nyingi za matumizi kwa ajili ya mtoto wao, kwa hiyo shetani alimpanda na kufikia hatua ya kufanya kile alichokitenda.

0 comments:
Post a Comment