Uongozi wa muziki nchini marekani unao muongoza msanii wa R&B Chris
Brown umetoa taarifa kwa uongozi wa muziki Tanzania unao muongoza msanii
kutoka Tanzania ALI KIBA msanii ambae yupo chini ya uongozi wa Kampuni
za SAMSUNG....
Kwa taarifa zilizopo katika mtandao wa VIP Beats nchini marekani
zinaeleza kua tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka 2014 uongozi wa msanii Chris
Brown ulipokea maombi ya muungano wa wasanii wawili kufanya wimbo wa
pamoja kati ya msanii Ali kiba na Chris Brown maombi hayo
yaliambatanishwa na Softcopy zilizobeba nyimbo tatu za msanii Ali kiba
ikiwemo SINGLE BOY,
MWANA pamoja na wimbo aliofanya katika project ya ONE 8. Uongozi wa
Chris Brown umethibitisha kupokea taarifa za maombi hayo na umeonesha
kupenda sauti ya msanii Ali kiba na kutoa tamko kua wapo tayari
kusimamia kazi ya pamoja itakayofanywa na wasanii hawa.
Upande wa msanii Chris Brown amesema hana tatizo yupo tayari
kushirikiana na msanii Ali kiba kwani alipata nafasi ya kutazama project
ya One 8 na ameona kiwango cha msanii Ali kiba kinaridhisha
Japokua anahitaji marekebisho madogo sana. BBC SWAHILI
Tunampongeza msanii Ali kiba kwa juhudi zake tunamtakia kila lakheri
katika kazi hii, kuipata habari hii kamili tembelea mtandao wa VIP
Beats, Channel 0 au unaweza kuipata katika American Spring news.
Uongozi wa Msanii Chris Brown Upo Tayari Kufanya Kazi na Ally Kiba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment