Jitibu magonjwa 300 kwa kutumia Mlonge

Mlonge au Moringa oleifera kwa kiingereza umekuwa ukijulikana kama mti wa miujiza kwa karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na katika nchi za Caribbean. Mti huu umeripotiwa kutibu zaidi ya magonjwa 300 ikiwemo magonjwa mbalimbali sugu.

Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika kama dawa. Majani ya mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wa mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.

Mbegu za mlonge zimekuwa dili kubwa duniani kwa sasa, zinahitajika kwa kiasi kikubwa katika nchi ya Marekani na China na kwa mjibu wa taarifa ni kuwa zinauzwa mpaka shilingi 45000 ya Tanzania kwa gramu 500. Walikuja pia wachina kuzinunua kwa wingi na walipokuwepo hapa Tanzania bei ya mbegu za mlonge ilifika mpaka 11000 kwa kg kwa bei ya jumla yaani kwa anayechukua kg 100 au 500 au 1000 na kwenda juu. Taarifa zisizo rasmi zinadai Wachina hawa walikimbia nchini baada ya serikali kuanza kufuatilia na kuwakamata wakwepaji kodi bandarini. Isingekuwa hivi mpaka leo mlonge ungekuwa umeshatoweka wote Tanzania.

Faida za mlonge zimeandikwa na majarida ya afya na lishe kadhaa duniani. Kile ulikuwa hujuwi ni kuwa viwanda na makampuni mengi ya dawa za hospitalini yamekuwa yakitumia virutubishi vilivyomo kwenye mti huu kutengenezea madawa kwa ajili ya binadamu na wanyama.

MLONGE UNA:

  • Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe
  • Potasiamu mara 15 zaidi ya ile ya kwenye ndizi
  • Una vitamini A mara 10 zaidi ya ile ya kwenye karoti
  • Una protini nyingi mara 9 zaidi ya ile ya kwenye mtindi (Yogurt)
  • Una Klorofili (kemikali ya rangi ya kijani ipatikanayo katika mimea) mara 4 zaidi ya ile ya kwenye nyasi au majani ya ngano (wheatgrass)
  • Una madini chuma (iron) mara 25 zaidi ya yale ya kwenye Spinach
  • Una vitamini A mpaka Z,
  • Una Omega 3, 6, na 9
  • Una asidi amino zile mhimu zaidi zinazohitajika na mwili
  • Una kiasi cha kutosha cha madini ya Zinc ambayo ni madini mhimu katika kuongeza homoni za kiume na nguvu za kiume kwa ujumla


MLONGE NDICHO CHAKULA CHENYE AFYA ZAIDI KULIKO CHAKULA KINGINE CHOCHOTE JUU YA ARDHI;

Mlonge una jumla ya virutubishi 92, mmea au mti mwingine wenye virutubishi vingi baada ya mlonge una virutubishi 28. Mlonge una viondoa sumu 46 na viondoa uvimbe mbalimbali mwilini 36, una asidi amino 18 na asidi amino mhimu zaidi 9 ambazo miili yetu haina uwezo wa kuzitengeneza.

Unga wa majani ya mlonge unao uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya 300 mwilini, magonjwa hayo ni pamoja na;

1. Huko Afrika magharibi madaktari hutumia mlonge kutibu Kisukari
2. Huko India mlonge hutumika kutibu shinikizo la juu la damu
3. Hutibu matatizo au maumivu ya mishipa
4. Hutuliza mapigo ya juu ya moyo (stroke),
5. Hutibu Kansa
6. Pumu
7. Hutuliza wasiwasi
8. Kikohozi
9. Maumivu ya kichwa
10. Inazuia na kushusha lehemu (cholesterol) hata ile ya juu zaidi (hypocholesteremia)
11. Inapunguza mafuta tumboni
12. Inaweka sawa homoni
13. Inatibu maumivu wakati wa hedhi (dysmenorrhea),
14. Unasafisha ini (hepatic detoxification),
15. Unasafisha mkojo na kibofu cha mkojo
16. Unarekebisha matatizo kwenye tezi
17. Unatibu kipindupindu na kuharisha
18. Kifua kikuu
19. Kichwa kizito
20. Uchovu
21. Mzio (aleji)
22. Vidonda vya tumbo
23. Maambukizi kwenye ngozi
24. Maumivu mbalimbali mwilini
25. Huondoa madoa doa meusi kwenye ngozi (blackheads),
26. Husafisha damu,
27. Hutibu matatizo kwenye koo
28. Huondoa makohozi mazito kooni
29. Huondoa taka na msongamano kifuani
30. Hutibu kipindupindu
31. Huondoa mtoto wa jicho au uvimbe kwenye jicho
32. Hutibu maambukizi kwenye macho na kwenye masikio
33. Unatibu homa
34. Maumivu kwenye maungio
35. Huondoa chunusi
36. Hutibu matatizo karibu yote ya ngozi na kinga ya mwili
37. Matatizo kwenye mfumo wa upumuwaji
38. Inatibu Kiseyeye (scurvy)
39. Huongeza uwingi wa mbegu za kiume na nguvu kwa ujumla
40. Unatibu minyoo
41. Huongeza maziwa kwa wingi kwa mama anayenyonyesha
42. Huondoa uvimbe kwenye utumbo mpana (colitis)
43. Unatibu gauti (dropsy),
44. Unatibu kuhara damu (dysentery)
45. Unatibu kisonono ( gonorrhoea)
46. Unatibu tatizo la kukosa usingizi,
47. Unatibu homa ya manjano (jaundice),
48. Unatibu malaria
49. Unatibu U.T.I na matatizo mengine kwenye mfumo wa mkojo
50. Unasidia pia kujenga na kuimarisha misuli
51. Unatibu magonjwa ya mifupa

Mlonge unasafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno, ngozi na nywele. Wakati unatumia mlonge unakufanya ujisikie vizuri, ujisikie mpya (fresh) na mwenye nguvu. Watu wengi wanaotumia mlonge huwa ni wenye afya nzuri hata kwa muonekano tu hata wanapokuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 90.

Majani ya mti wa mlonge pia yanaweza kutumika kutengeneza biogas (aina ya nishati ya umeme inayotokana na kinyesi cha ng’ombe au takataka). Hutumika pia kama chakula cha wanyama kama sungura, mbuzi, ng’ombe, mbwa nk. Sungura wanaonekana kupenda zaidi mlonge kuliko wanyama wote.

MBEGU ZA MLONGE:
1. Mbegu zake hutumika kama kiuaji sumu na pia hutibu uvimbe. Hutibu maumivu ya kwenye mishipa, baridi yabisi, gauti, kukamaa mishipa, magonjwa ya ngono na majipu. Mbegu hizi hukaangwa kidogo, hupondwapondwa na kuchanganywa na mafuta ya nazi na kupakwa sehemu yenye tatizo.

2. Mbegu za mlonge zilizokaangwa na mafuta yake husaidia watu wanaoshindwa kuzalisha mkojo.

3. Mbegu zake hutumika pia kumtuliza au kumfanya mtu mwenye kifafa a-‘relax’.

4. Mbegu za mti wa Mlonge ni kinga dhidi ya vijidudu (bacteria) wasababishao magonjwa na kuathiri ngozi ikiwemo fangasi.

5. Pia mbegu hutumika katika kusafisha au kuchuja maji ambapo zikipondwa na kuwekwa kwenye maji yenye tope au machafu husababisha uchafu kujikusanya na kuzama chini kisha kuacha maji yakiwa safi na salama kwa kupikia au kunywa badala ya kuchemsha.

6. Mbegu za mlonge pia huongeza kwa kiasi kingi kinga ya mwili (CD4), Kama una tatizo la kinga ya mwili wako kushuka basi tumia mbegu za mlonge kwa mwezi mmoja mpaka mitatu na kinga yako itaimarika sana.

Chukuwa punje 3 na uzimenye ganda lake la juu na utafune mbegu ile ya ndani yote hizo tatu na ukimaliza kuzitafuna kunywa maji ya kawaida siyo ya kwenye friji glasi 2 (nusu lita), fanya hivi kutwa mara tatu.

MLONGE UNATOA WAPI MAAJABU YOTE HAYA?
Matatizo mengi ya kiafya ni matokeo ya lishe yenye viinilishe duni au hafifu jambo linalopelekea kuwa na kinga ya mwili isiyo na nguvu kupigana na magonjwa mbalimbali. Unaporekebisha usawa huo usio sawa wa kinga yako ya mwili kwa kutumia mimea na lishe zingine mhimu za asili hutakawia kuona matokeo mazuri kwenye afya yako.

Uwezo wa mti wa mlonge kuyaweza yote hayo ni kutokana na kuwa na vitamini, madini mbalimbali na viondowaji sumu vingi kuliko mmea mwingine wowote. Wagonjwa wengi wenye UKIMWI katika sehemu nyingi za afrika magharibi wameripoti kuongezeka kiasi kikubwa cha kinga yao ya mwili baada ya kutumia mlonge kiasi cha kutokuhitaji dawa.

NGUVU, UMAKINI, NGOZI YENYE KUPENDEZA, KUTOZEEKA MAPEMA NA KUPUNGUZA UZITO NA UNENE:
Mlonge una viinilishe mhimu vinavyosaidia kuuongezea uwezo mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Vitamini, madini na homoni mhimu zilizomo kwenye mti huu huufanya mwili wako kuwa na usawa unaohitajika kiafya na hivyo kukupa kinga dhidi ya magonjwa mengi bila idadi.

Mlonge una kiinilishe mhimu sana kwa wingi kuliko mmea au mti mwingine wowote duniani mara maelfu kadhaa kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘Zeatin’. Zeatin ndiyo hutengeneza seli mpya za ngozi pia huzifanya seli mpya kutengenezwa kwa haraka na kwa wingi zaidi ya zile seli zinazokufa. Hii huleta matokeo mazuri ikiwemo kuondoa mikunjo ya ngozi au ngozi kuzeeka sehemu za uso na sehemu nyingine za mwili na kukupa afya nzuri ya ngozi.

Kwenye mlonge kuna ‘Sulfur’, hii sulfur ni mhimu katika kuunda vitu mhimu kwenye ngozi kama collagen na keratin huku viuaji au viondowaji sumu zaidi ya 30 vinavyopatikana kwenye mlonge ni mhimu kwa ajili ya afya ya ngozi yako.

Mlonge ambao umekuwa ukitumika kwenye vituo vingi vinavyojihusisha na kupunguza uzito huwa una nguvu ya asili ya kupunguza njaa, huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kukung’arisha wewe huku ukikuacha na virutubishi vingi mhimu zaidi.

HUIRUDISHA UPYA AFYA YA MWILI WAKO;
Baada ya kufikisha umri wa miaka 30 hivi nguvu zako za mwili huanza kushuka. Mwili wako utaanza kuleta mchonyoto. Utaona unaanza kupoteza umakini nyakati za mchana sababu hukuzingatia nini ule wakati ulipokuwa kijana. Baadhi ya kuharibika kwa afya hakuwezi kurudishwa nyuma ikiwa ni pamoja na kuzorota kwa afya ya meno.

AFYA MBOVU YA MENO INAPELEKEA MAGONJWA KADHAA NA VIFO;
Calcium, Magnesium, Manganese, Potassium, Boron na Vitamini D yote ni madini mhimu ili uwe na meno yenye afya. Magonjwa mengi sugu ni matokeo ya upasuaji wa kwenye kinywa. Kila mtu anapaswa kulinda afya ya meno yake kuanzia leo kwani meno yakishaoza au kuharibika huwa ni vigumu kupona na kurudi kwenye hali yake ya mwanzo. Afya ya meno yako itaamua ni miaka mingapi unaweza kuishi.

Kila mmoja wetu anatakiwa kutimiza wajibu wake linapokuja suala la afya ya mwili wako. Tumia google tafuta taarifa za kile unachokula au kunywa kila siku. Kichwa kitakuuma utakapojua ni nini unakula!. Nenda YouTube angalia video hizi: “Food Matters” na “Dying to have know”. Tafuta kwenye chaneli ya Discovery movie inaitwa “Moringa The Miracle Tree” na video nyingine inaitwa ‘Moringa Oleifera’.

BIDHAA NYINGI ZA AFYA HAZINA AFYA YOYOTE;
Bidhaa nyingi za afya hazina utafiti halisi (genuine) unaojitegemea au zina maelezo kutoka kwa mtengenezaji tu wa hiyo bidhaa. Mlonge una mfululizo wa tafiti za watu wengi na shuhuda za watu kote duniani zaidi ya miaka 4000 iliyopita. Ni mtishamba kwa asilimia 100 unaoota wenyewe.

Matumizi ya mlonge kama kiua vijasumu (antibiotic) kwenye tiba asili yalianza miaka maelefu iliyopita. Mlonge ulitumika kwa mara ya kwanza kama dawa zaidi ya miaka 2000 kabla ya Kristo. Watabibu wazamani wa Misri na Ugiriki waliona faida nyingi za mti huu na wakautambulisha kwa Warumi na baadaye mlonge ukaenea mashariki mwa India na sehemu ya chini ya nchi ya Uchina, kusini mashariki mwa Asia na Ufilipino na magharibi mwa Misri kuzunguka mediterania na mwishowe ukafika kwa Wahindi mashariki mwa Amerika. Leo zaidi ya watu milioni 400 wanatumia mlonge. Shirika la afya duniani (W.H.O) limekuwa likitumia mlonge zaidi ya miaka 40 sasa.

Unga wa majani ya mlonge unapaswa uwe ni wa kijani kweli kweli na majani yake yawe yalianikwa kivulini na siyo juani. Anza na kijiko kidogo kimoja ukichanganya na vimiminika kama maji ya uvuguvugu au juisi yoyote ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani kutwa mara moja na taratibu ongeza kiasi cha dawa kadri unavyohitaji. Unaweza kuuchanganya pia kwenye wali wakati unakula au unaweza kuweka ndani ya kikombe cha uji au unaweza kutumia kama majani yako ya chai ingawa hautakiwi uchemshe sana kwenye moto.

Mti wa mlonge sasa umeanza kuwa maarufu huko Marekani hii ni kutokana na mti wenyewe kuendelea kupata umaarufu miongoni mwa watu wanaojali afya zao. Ingia google andika ‘Moringa plants for sale’ utagundua keyword hiyo inatafutwa kila siku mara maelfu. Watu wengi pia wameanza kilimo cha mlonge kama biashara ya kuwaingizia kipato. Ukiwa na miti 200 tu ya mlonge shambani kwako tayari wewe siyo mwenzetu.

Mti wa mlonge ni moja ya miti mhimu katika sehemu yote ya dunia. Kadri watu wanavyoendelea kuutafiti na kuusoma mti huu ndivyo mahitaji ya unga wa majani yake, mbegu zake, unga wa mbegu zake na mafuta ya mbegu zake yatakavyozidi kuongezeka na kuongezeka.

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger