Alikiba amedai anaweza kumshirikisha Diamond kama tu akipata wimbo unaomfaa msanii huyo.
“Ngoja nikwambie ukweli, sidhani kama ninaweza kuja kufanya kolabo na
Diamond, ila nikipata wimbo ambao nadhani kwamba anastahili kuwapo,
kiukweli nitamshirikisha lakini kama hastahili haitawezekana,” Alikiba
aliliambia gazeti moja la kila siku.
Kwa upande mwingine akijibu swali la kama ana mpango wa kuja
kumshirikisha staa wa Marekani, Chris Brown, Alikiba alisema: "Uwezekano
wa kufanya upo kwa sababu kila kitu ni mipango kwa hiyo naweza kufanya
kolabo na wasanii wa kimataifa na mashabiki watarajie kufanya hivyo.”
0 comments:
Post a Comment