Mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa
kundi la Jahazi Modern Taarabu,Mzee Yusuph anatarajia kuoa tena mke wa
tatu hivi karibuni huku wake zake wawili wakiwa kwenye bifu zito
wakitupiana vijembe mtandaoni.
Akipiga stori na Uheard na Soudy Brown alisema kuwa anatarajia kuoa mke
huyo ambaye anaishi huko visiwani Pemba,na kwamba mipango ikiwa tayari
kila kitu kitakuwa hadharani.
Hivi karibuni wake zake wawili ambao ni Malkia Leila Rashid ambaye pia
ni mwimbaji wa kundi hilo na mke wake mdogo aitwaye Chiku wamekuwa
wakirushiana vijembe kwenye mtandao wa kijamii wa ‘WathsAAp’ kwa
kuandikiana ‘Status’ za vijembe.
Habari zinasema kuwa wake hao wamekuwa kama chui na paka na mzee Yusuph
hana mpango wa kuwapatanisha kwa kuwa hakuna hata mmoja aliyeonyesha
chuki kwa mwenzake akiwa na nao.
‘’Waache tu warushiane vijembe tena ndiyo vizuri na dawa yao nawaletea mke wa tatu na wala sina mpango wa kuwapatanisha,"alisema Mzee Yusuph.
Mzee Yusuph kuoa tena mke wa watatu,Wake zake watupiana vijembe mtandaoni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment