Muimbaji wa kundi la Chamber Squad, Maze B, amefariki leo saa nne
asubuhi, kwa mujibu wa mtu aliyekuwa akimuuguza.
Msanii huyo aliyewahi
kufanya vyema na wimbo wake ‘Fikiria’ alikuwa amelazwa katika hospitali
ya Mwananchi mjini Dodoma.
Mez B aliyezaliwa kwa jina la Moses Bushagama alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Pneumonia.
Hivi karibuni aliongea na E-News ya EATV na alikuwa anaendelea vyema:
“Nilikuwa na tatizo la Pneumonia tokea mwezi wa 12 nikawa nipo vizuri
nilivyo kuja tena Dodoma hali ikabadilika ndo nipo hospitali nimelazwa
nasumbuliwa na maumivu ya kichwa na shingo,” alisema.
“Nategemea kuruhusiwa muda wowote na sasa hivi naendelea vizuri.”
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
0 comments:
Post a Comment