Mkazi wa kijiji cha Ibosa, kata ya Nyakato, Bukoba Vijijini, Amelia
Richard (50) anatuhumiwa kumuua mwanamke mwenzake kwa kummwagia mafuta
ya taa na kumchoma moto baada ya kumfumania na mumewe.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alitaja tukio
hilo ni la Februari 15, mwaka huu saa 3 usiku katika kijiji cha Ibosa
kata ya Nyakata Bukoba vijijini.
Alimtaja aliyeuawa ni Pelagia Martin (46) aliyeunguzwa mwili mzima.
Kamanda alisema mwanamke huyo alicheleweshwa kufikishwa Hospitali ya
Mkoa hadi kesho yake; Februari 16 baada ya wanafamilia kuomba wayamalize
bila kwenda Polisi.
Makubaliano ya wanafamilia hao yalitokana na kile kilichoonekana kwamba
Amelia alimfumania Pelagia akiwa na mumewe, Richard Bulebo (57) ndani
ya nyumba yao.
Kwa mujibu wa Kamanda, Februari 16 walipoona hali ya majeruhi inazidi
kuwa mbaya, ndipo walifika katika Kituo cha Polisi mjini Kati wakiomba
msaada.
Polisi walimpeleka majeruhi huyo Hospitali ya Mkoa lakini alifariki
kabla ya kupatiwa matibabu. Polisi inamshikilia Amelia na Bulebo kwa
tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
Mwanamke Amuua Mwanamke Mwenzake kwa Kummwagia Mafuta ya taa na Kumchoma Moto baada ya Kumfumania na Mumewe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment