Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amepokea samansi ya
mashtaka kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Abdallah
Sharia Ameir (CCM) ambaye amedai amlipe fidia ya kumdhalilisha sh.
Milioni 500 au amuombe radhi kupitia kipindi chake.
Akiongea na Mwandishi wetu, Joyce Kiria alisema kuwa amepokea barua hiyo
kwa mikono miwili na anawasubiri wanasheria wake ili
waijadili.“Nilimpokea mke wa Mbunge aitwaye Hawa kama mwanamke mwenye
matatizo ambaye alifika kutoa sauti yake ili watu wamsaidie mtoto wake
mwenye ulemavu.
"Baada ya kuongea naye nilimtafuta mheshimiwa ili kumpa nafasi naye
aongee ya kwake kama wajibu wangu, lakini cha kushangaza yeye
alinikamata na kunipeleka polisi, leo anasema nimemdhalilisha,” alisema
Joyce .
Joyce anadaiwa fidia na Mbunge huyo kwa kuitangaza habari ya kumtelekeza
mtoto mlemavu ambaye alipelekwa kwenye kipindi chake na mkewe, Hawa
Deusi.
Joyce Kiria Adaiwa Milioni 500 kama Fidia ya Kumdhalilisha Mbunge Kupitia Kipindi cha Wanawake Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment