Mwigizaji na mwanamziki, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ambae ni mama wa
watoto wawili wa kike , akiwa na mchumba wake Nuh wamechafua hali ya
hewa baada ya kutupia picha yao inayowaonyesha wakiwa watupu.
Nuh Mziwanda ndio alioibandika picha hiyo kwenye ukursa wake kwenye
mtandao wa instagram na baada ya kuona wengi wanamshabulia aliamua
kuibandua. Kwa kiufupi picha hii haina maadili na ukizingatia mwanadada
Shilole ni mama na sijui watoto wake watajifunza nini hapa.
Wapo walioona kuwa kitendo hiki alichokifanya Mziwanda labda ni kutokana
na umri wake hivyo hayo ni baadhi ya matokeo ya kuwa na mahusiano na
mtu mtoto mdogo na kuona Mziwanda hana kosa hapa. Lakini pia wapo
walioona kuwa wawili hawa wanatafuta KIKI tu ili media za hapa Bongo
ziwazungumzie kama Zari na Diamond, ila pia wapo amabo wanaona hii ipo
poa na haina tatizo.
Nadhani kitendo cha Mziwanda kubandua picha hii ni kutokana na akili
yake ku-CLICK kuwa amekosea, nampongeza kwa hilo na naamini atakuwa
amejifunza kitu.
Nia na madhumuni ya kuileta hapa ni kutaka watu watambue kuwa mtandao ni
zaidi ya tunavyofikilia kwani kosa la sekunde moja mtandaoni linaweza
kukuhalibia maisha yako yote..Siku nyingine naamni watakuwa makini.
Mzee wa Ubuyu
Shilole na Mchumba Wake Nuh Mziwanda Wachafua Hali ya Hewa Mtandaoni!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment