Mwigizaji wa filamu mwenye mikasa ya aina yake, Manaiki Sanga ‘The Don’
amesema kuwa hajakata tamaa kumuoa msanii mwenzake, Jacqueline Wolper
na kwamba bado anaendelea kuwashawishi wazazi wake.
Akiongea na Gazeti la Uwazi, Manaiki aliweka wazi kuwa bado
anawashawishi wazazi wake wakubaliane na uchaguzi wake kwakuwa ndiye mtu
anayempenda.
“Ni upande mmoja tu wa ndugu zangu ambao wapo kijijini Mbeya na
hawamfahamu Walper ila sijakata tamaa na naamini watanielewa tu kwa
maaana ndoto yangu mimi ni kumuoa mtu ambaye ninampenda,” alisema
Manaiki.
Hivi karibuni Manaiki alitangaza nia ya kumuoa Walper ambapo wazazi wake
walimkatalia na kumwambia atafute msichana wa kutoka mkoa wake.
MANAIKI: Bado Sijakata Tamaa Kumuoa Jack Wolper
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment