Vyakula bora kwa ajili ya Kupunguza Shinikizo la Damu


BP
Linapokuja suala la kupunguza shinikizo la damu yako,ulaji wa vyakula vyenye mafuta kidogo na madini ya potasiamu na magnesiamu kwa wingi ni muhimu sana.
Shinikizo la damu limekuwa moja kati ya matatizo makubwa ya afya miongoni mwa watu walio katika mazingira mbalimbali ya kimaisha duniani.

Utafiti unaonesha kwamba katika Afrika kwa mfano tatizo kubwa kwa siku za nyuma lilikuwa magonjwa ya kuambukiza kama malaria, UKIMWI(HIV-AIDS), surua n.k. Lakini leo magonjwa yasiyo ya kuambukiza wakati mwingine yanaitwa magonjwa ya staili ya maisha kama vile magonjwa ya moyo; kisukari na saratani yamekuwa yakiua watu wengi kama tu magonjwa ya kuambukiza, hali inayoitwa “Mzigo Mara Mbili”

Mikakati mipya inahitajika ili kukabiliana na hali hii. Kama tunaweza kubadili jinsi tunavyoishi kwa kubadilisha tabia ya kula kwa mfano, tunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo hili.

Shinikizo la damu (msukumo wa juu wa damu)
Ni hali mbaya ambayo inaweza kusababisha ugonjwa wa moyo, moyo kushindwa kufanya kazi, kiharusi, kushindwa kwa figo kufanya kazi, na matatizo mengine ya afya.

“Msukumo wa damu” ni nguvu ya kusukuma damu katika kuta za mishipa ya moyo (ateri) wakati moyo unaposukuma damu.
Kama shinikizo hili linaaongezeka na kuwa juu kwa muda mrefu linaweza kusababisha madhara mwilini katika njia nyingi.

Sababu za Shinikizo la Damu:
Uwezekano wa kupata shinikizo la damu linaongezeka kadiri umri wako unavyoongezeka.

Sababu halisi za kupata shinikizo la damu halijulikani, lakini mambo kadhaa yanaweza kuwa chanzo cha tatizo ikiwa ni pamoja na:
  • Kuwa mnene (kitambi) na uzito mkubwa
  • Kutofanya kazi zenye kushughulisha mwili(Mazoezi,kutembea na kazi za shamba)
  • Kutumia chumvi katika vyakula
  • Unywaji wa pombe kupita kiasi (Zaidi ya chupa moja 1 hadi 2 kwa siku)
  • Kunywa kahawa kwa wingi (au vinywaji vingine aina hiyo ambavyo vina kemikali ya caffaine)
  • Msongo wa mawazo
  • Umri mkubwa (zaidi ya miaka 65)
  • Asili au ukoo
  • Historia ya shinikizo la damu katika familia
  • Kisukari sugu
  • Matatizo ya grandi za Adrenal na thyroid
  • Uvutaji wa sigara
  • Kutokula kula matunda ya kutosha na mboga

Vyakula ambayo vinaweza kusaidia kupunguza shinikizo la damu:
Njia bora ya kupunguza shinikizo la damu ni kula vyakula ambavyo vinasaidia kufanya mishipa ipanuke na hivyo kufanya moyo kutofanya kazi kupita kiasi.
Vifuatavyo ni baadhi ya vyakula ambavyo vinasaidia kupunguza shinikizo la damu:
1. Zambarau:
zambarau
Kuwa kula kiasi kidogo cha zambarau kwa wiki kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya shinikizo la damu.
Kwa mujibu wa tafiti za hivi karibuni, zambarau, kama vile stoberi na raziberi, vyenye kemikali ya asili iitwayo anthocyanins  ambayo husaidia kulinda dhidi ya shinikizo la damu.

 2. Nafaka
serials
Kula nafaka, hasa nafaka zisizokobolewa na kutolewa viini, na zenye fiba. Nafaka kama vile mahindi yasiyokobolewa au ngano, vinaweza kupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la damu.

 3. Juisi ya Biti (Beet Root Juice)
beet juice
Kunywa glasi moja ya juisi ya biti kunaweza kupunguza shinikizo la damu ndani ya masaa machache tu, nitreti iliyomo katika biti ina faida sawa na ile inayopatikana katika vidonge
Vyakula vingine vyenye nitreti kwa wingi ni pamoja na mchicha, kabichi na karoti.

4. Spinachi
spinach
Spinachi au mchicha vina kalori kwa kiwango kidogo na faiba kwa wingi na ina virutubisho mohimu vya moyo kama potasiamu, foleti, na magnesium – madini muhimu kwa ajili ya kupunguza viwango vya shinikizo la damu.

5. Viazi mviringo vya kuokwa
viazi_mviringo
Viazi mviringo vina madini ya magnesiamu na potasiamukwa kiwango kikubwa, ambayo muhimu kwa afya ya moyo. Wakati potasiamu inapokuwa chini, mwili unabakiza na sodiamu nyingi na sodium huongeza shinikizo la damu.

6. Maziwa ya mtindi yaliyotolewa mafuta (Skim Milk)
skim milk
Kunywa maziwa haya hutaongeza kalsiamu na vitamini D – virutubisho hivi kufanya kazi kwa pamoja kusaidia kupunguza shinikizo la damu kwa asilimia 3 hadi 10.
7. Maharage
beans
Maharagwe ya aina zote yana kiwango kikubwa cha faiba, magnesiamu, na potasiamu, ambavyo vyote ni muhimu kwa ajili ya kupunguza shinikizo la damu na kuboresha afya ya moyo kwa ujumla.

8. Alizeti
alizetiMbegu za alizeti pia ni chanzo kikuu ya magnesium
Kama potasiamu, magnesiamu husaidia kutoa sodiamu mwilini hivyo kusaidia kupunguza shinikizo la damu.

9. Chokulati
chocolate
Chokulati ina kemikali ya flavanols ambayo hufanya mishiba ya damu kunyumbuka zaidi na kupunguza shinikizo la damu katika mishipa.
Kutokana na utafiti,kula kipande kidogo tu cha chokulati kila siku kunaweza kusaidia kupunguza shinikizo la damu, hasa kwa watu ambao tayari wana shinikizo la damu.
Angalia chokulati ambayo ina asilimia 50 hadi 70 ya kakao.

10. Ndizi
bananaMatunda haya yana potasiamu kwa wingi.
Ndizi inaweza kuliwawakati wa mlo wako. Pia ni matunda yanayopatikana wakati wote na kila mahali.


Chukua hatua leo kwa kufuata ulaji wa vyakula tajwa. Ufumbuzi upo katika kubadili tabia ya ulaji.
Afya yako iko katika mikono yako mwenyewe
Kuwa mwenye afya njema, ishi za

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger