Msanii
anayefanya vizuri kunako kiwanda cha filamu Bongo, Wastara Juma
amefunguka kwamba tasnia ya filamu kwa sasa inaonekana kama imeingiliwa
na pepo mbaya kutokana na mambo kwenda ndivyo sivyo kila kukicha.
Akizungumza
na Gpl, Wastara alisema tasnia ya filamu imekuwa ni ya migogoro, chuki
huku bei ikishuka jambo ambalo siyo sahihi kwani litawarudisha nyuma
wasanii wakati hata kazi hiyo hailipi kihivyo.
“Mimi sitengenezi filamu mpaka nielewane na bosi bei kabisa lakini vinginevyo ndiyo maana nimeamua kujikita kwenye biashara ili niweze kuendeleza maisha ya kila siku maana tasnia haieleweki sasa hivi, naona kama pepo mbaya ametuvamia inatakiwa tumuombe Mungu sana,” alisema Wastara.
0 comments:
Post a Comment