Mbunifu
wa mavazi na mtangazaji Bongo, Jokate Mwegelo amesababisha shosti yake,
Wema Sepetu ‘Madam’ afurahi baada ya kumpelekea zawadi ya kandambili
zake za Kidoti pamoja na vipodozi mbalimbali.
Jokate
alisema Wema ni miongoni mwa watu ambao anawakubali kutokana na mchango
mkubwa katika tasnia ya filamu Bongo, hivyo ameamua kumpelekea zawadi
ya bidhaa zake za Kidoti kuonesha heshima yake.
“Zawadi zangu niliwapa watu mbalimbali mmoja wapo akiwa ni shoga yangu wa kitambo Wema, hii inaonyesha ni jinsi gani nina mapenzi makubwa kwake,” alisema Jokate.
Kwa
upande wake Wema, alifurahi na kusema amependa zawadi hiyo anamuomba
Mungu azidi kumfungulia milango Jokate katika bidhaa zake mbalimbali
anazosa-mbaza.
0 comments:
Post a Comment