Jux na Vanessa Mdee hawataki tena kuficha uhusiano wao. Tangu mwaka
mpya uanze, waimbaji hao wameuachia ulimwengu ufahamu kuwa ni wapenzi na
wanapenda baada ya kipindi kirefu cha tetesi za uhusiano wao ambazo
walikuwa wakizikanusha.
Uhusiano huo umepelekea hadi Jux amtumie Vee Money kama mpenzi wake
kwenye video ya ‘Sisikii’ na kama umeitazama utakuwa umegundua chemistry
ya kuvutia kati yao.
Weekend hii wawili hao wakiwa pamoja na Navy Kenzo, walikuwa na show
visiwani Zanzibar ambapo Jux pamoja na kutumbuiza nyimbo zake, alipanda
jukwaani kumpa kampani mpenzi wake huyo kwa kuchukua nafasi ya Barnaba
wakati alipokuwa akitumbuiza wimbo ‘Siri’.
Baada ya show hiyo wapenzi hao walijumuika pamoja kula upepo kwenye
beach za Zanzibar na mashabiki wao wanafurahia tu kuwaona pamoja.
Jack Patrick Kabla hajakamatwa na Madawa ya Kulevya Maccau Ndio alikuwa Mpenzi wa Jux , Akitoka Jala Atakuta Jux si wake Tena…..
Jux na Vanessa Mdee Hawalifichi Tena Penzi Lao, Jack Patrick Hana Chake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment