Daktari Matatani baada ya kumbusu na kumtomasa Mgonjwa wakati wa Matibabu

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo, ameliagiza Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Lucas  Mweri, kumchukulia hatua daktari anayetuhumiwa kumbusu mgonjwa wake wakati akimtibu.

Gambo alitoa agizo hilo jana baada ya kupokea malalamiko ya tukio hilo na kueleza kuwa ni la ukiukwaji wa maadili ya kidaktari na aibu kwa wilaya.
Aliliagiza jeshi la polisi kufanya uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria ili iwe fundisho  kwa mtaalamu huyo na wengine wenye tabia kama hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo
Awali ilidaiwa kuwa daktari huyo, Ally Naah  anayefanyakazi  Hospitali ya Wilaya ya Korogwe ya Magunga,  anadaiwa kumbusu mwanamke aliyekwenda kupata matibabu hospitalini hapo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema siku ya tukio mwanamke huyo aliambatana na mumewe hadi hospitalini hapo kwa ajili ya  kupata matibabu na baada ya kufika daktari huyo alimtaka aingie ndani kumfanyia uchunguzi.
Ilidaiwa kuwa, mume wa mwanamke huyo  aliyekuwa nje akimsubiri mkewe alipata hofu baada ya kuona muda mrefu umepita bila mkewe kutoka, ndipo alipochungulia dirishani  na kumuona daktari huyo akimbusu.
“Yule bwana hakuamini alichokiona, hakuvumilia  na alipiga kelele akiomba msaada…Kwa kweli jambo hili ni aibu na limetuondolea uaminifu,” alisema mmoja wa shuhuda wa tukio hilo.
Hata hivyo,  habari za kipolisi zinaeleza kuwa tayari tukio hilo limeshaanza kufanyiwa kazi ikiwamo kufuatiliwa eneo lilipotendeka kosa hilo kwa hatua zaidi za kisheria. Mganga Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Dk  Olden Ngasa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa alitoroka baada ya tukio hilo.

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger