MREMBO
Mariam Mohamed ambaye alishiriki na kushika nafasi ya pili ya Shindano
la Miss Mara mwaka 2003, wiki iliyopita alizusha vurumai kubwa kwa
kuzichapa kavukavu na mumewe usiku baada ya kumkuta akiwa na baamed
ndani ya nyumba moja iliyopo Njiro eneo linalojulikana kama Nguzo Moja
jijini Arusha, Amani lina mkanda kamili.
Mrembo Mariam Mohamed akizichapa kavukavu na mumewe, Rasha Idrisa (38).
Licha ya kuzichapa na mumewe huyo ambaye
ni mfanyabiashara aitwaye Rasha Idrisa (38), mkazi wa Sinza jijini Dar
es Salaam, baamed huyo aitwaye Prisila, naye alipata kipigo kikali toka
kwa Miss huyo aliyekuwa akisaidiana kutoa dozi na mpambe wake.Prissila anayefanya kazi kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Njiro (jina linahifadhiwa) alijaribu kujitetea kuwa hakufahamu kama mpenziwe huyo alikuwa mume wa mtu, alishambuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake, ikiwa ni pamoja na kukabwa shingo, hali iliyomuacha hoi na kuapa kutoendelea tena kuiba vya watu.
Operesheni
Fichuo Maovu (OFM) ya Global Publishers ilitonywa mapema juu ya kuwepo
kwa mpango wa kumfumania Rasha, anayedaiwa kuwa alisafiri kibiashara
akimuaga mkewe kuelekea Zambia, tokea Agosti mwaka huu.
Mrembo Mariam Mohamed akizidi kumtaiti mumewe.
Chanzo chetu kinadai kuwa kitu
kilichompa mashaka Mariam ni wakati alipokuwa akiwasiliana kwa simu na
mumewe, kwani miito yake ilionyesha kuwa mpigiwaji alikuwa nchini. Baada
ya kuona hivyo akaanza udadisi wa kujua ni wapi hasa alipo mumewe.
Siku chache
zilizopita, chanzo hicho kilisema msichana huyo alipata taarifa kutoka
kwa marafiki zake waliopo Arusha, juu ya kuonekana kwa mumewe akila
maisha na msichana mmoja mhudumu wa baa, na kwamba alikuwa akitanua naye
kila siku na mara nyingi walilala pamoja.
“Mariam amepanga kesho ndiyo aende
akawafumanie, kama ni pale baa au wanakoendaga, kwa hiyo nyinyi mnaweza
kwenda pale ili mjue kitakachoendelea,” chanzo chetu kiliwasiliana na
OFM ambao walifika katika baa anayofanya kazi Prisila bila yeye kufahamu
na baadaye Mariam akiwa na mpambe wake nao waliwasili.
Baamedi, Prisila akipokea kichapo kutoka kwa rafiki wa Mariam Mohamed kwa kula ujana na mume wa mtu.
Akiwa hatambui kama anafuatiliwa,
Prisila pamoja na rafiki yake mmoja ambaye hakufahamika jina lake,
waliondoka eneo hilo na kwenda kupanda daladala lililokuwa likielekea
Njiro na kuteremka eneo la Nguzo moja. Mariam naye aliondoka na kuchukua
usafiri binafsi kwa ajili ya kuwafuatilia wasichana hao huku nyuma yao
wakiwa OFM.
Prisila
aliingia katika nyumba moja iliyokuwa na geti jeusi majira ya saa tatu
na muda mfupi baadaye Mariam na mpambe wake nao waliwasili na kuukuta
mlango ukiwa wazi.Baada ya kuingia ndani, waliwakuta wawili hao wakiwa
katika mkao wa kimahaba na mara moja Mariam akiwa na fimbo, alianza
kumchapa mumewe aliyejaribu kumsihi kwa kupiga magoti ili walimalize
jambo hilo kwa mazungumzo. Wakati mume akipigwa na mke, mpambe alikuwa
akimpa kichapo cha maana Prisila.
Mume wa mtu na baamedi kwa pamoja wakiwajibishwa kwa kuvunja amri ya sita.
Rasha hata hivyo, baadaye alifanikiwa
kumnyang’anya fimbo mkewe huyo na kuanza kutoa vitisho kwa OFM waliokuwa
wakipiga picha za tukio hilo. Akizungumza wakati wa sekeseke hilo,
Mariam alisema amekuwa akimfumania mumewe mara kwa mara akiwa na
wanawake tofauti na mara zote huomba msamaha.Ingawa hawajafunga ndoa, Mariam alisema alianza kuishi na mwanaume huyo tangu mwaka 2004 na kwamba maisha yao yametawaliwa na migogoro kutokana na ukware wa mumewe.
Kwa upande wake, Rasha alisema yupo tayari kuachana na mkewe ili awe huru na maisha yake.
0 comments:
Post a Comment