Uraia wa RWANDA wamtesa Miss Tanzania

NI balaa juu ya balaa! Miss Tanzania mpya wa mwaka  2014 aliyepokea taji kutoka kwa Sitti Abbas Mtemvu, Lilian Deuce Kamazima, amejikuta akimwaga chozi kufuatia kuanza kusakamwa kwa madai  kwamba ni raia wa nchi jirani ya Rwanda kwa kuzaliwa wazazi wake.
Hali hiyo ilimpata juzikati aliposakwa na paparazi wetu aliyetaka ufafanuzi kutoka kwake kwamba hata yeye hana sifa ya kuwa Miss Tanzania 2014 kwa vile si raia wa Tanzania, achilia mbali Sitti aliyedaiwa kudanganya umri.
ALIANZA KWA KUPANGUA
Akizungumza na gazeti hili, Lilian alisema uvumi wa watu unaonea juu yake kuwa yeye si raia wa Tanziani si mzuri kwa vile unaanza kuchafua taji lake bila sababu za msingi na jambo hilo linamfanya awe analia kila wakati kwa vile yeye ni mzaliwa wa Bongo kwa baba na mama wa kutoka Bukoba mkoani  Kagera.
“Watu waache kuzungumza kwa hisia jamani, mimi ni Mtanzania na wazazi wangu wote ni Watanzania

Miss Tanzania mpya, Lilian Deuce Kamazima.
Hata vitambulisho vyangu vyote vinaonesha uraia wangu wa Tanzania, sasa sijui wanaosema mimi Mrwanda wamehisi nini au jina la Kamazima ndiyo linawafanya kusema hivyo na kama ni jina mbona Bukoba jina hili halipo kwetu tu, kuna akina Kamazima wengi na wala si geni, jambo hili limeniumiza sijui nitafanya nini lakini ukweli utajulikana,” alisema Lilian
Aliyekuwa Miss tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu.
BOSI TAKUKURU ATAJWA
Hata hivyo, Lilian alipata utetezi kufuatia vielelezo kuanikwa  na wadau kwamba, hata aliyewahi kuwa bosi wa Taasisi ya Kuzuia  Rushwa Tanzania ‘Takuru’ (sasa Takukuru), Meja Jenerali Mstaafu, Anatoly Kamazima ambaye alistaafu mwaka 2006, alikuwa Mbongo kamili.
JIOGROFIA YADAIWA KUMUUMIZA LILIAN
Mwenyeji mmoja wa mji wa Bukoba, Isaya Rwechungura ambaye anafanya kazi wizara ya elimu jijini Dar, mkazi wa Sinza D alisema majina yanayopatikana kwenye mipaka ya Tanzania yanaunga nchi mbili.
“Mfano, ukienda Ruvuma kuna akina Banda, ukienda Malawi pia Banda wapo na hizi nchi mbili zimepakana, Malawi na Tanzania ambayo Mkoa wa Ruvuma upo ndani yake.
“Ukienda Tarime, Mara utakutana na akina Ondieki, lakini pia Kenya wapo. Kwa hiyo kama Rwanda kuna Kamazima hata Bukoba Tanzania wapo,” alisema Rwechungura.
 
Mratibu wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga ‘Anko’.
AMANI LAMSAKA LUNDENGA
Baada ya maelezo hayo, Amani lilimsaka Mratibu wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga ‘Anko’ na kumuomba ufafanuzi juu ya utata huo ambao unazidi kuchafua mashindano hayo.
“Jamani, sijui niseme nini? Kusema ukweli tunasakamwa sana, sijui kwa nini! Lilian ni Mtanzania mwenzetu, hata vyeti alivyovileta kwenye kamati vinaoesha hivyo.
“Sasa hivi ninavyoongea na wewe yupo Uganda, amekwenda kwa kutumia hati za Tanzania,” alifunguka Anko Lundenga.
KUMBE WENYE WAZAZI WOTE SI RAIA RUKSA KUSHIRIKI
Lundenga alikwenda mbele zaidi kwa kuanika jambo moja kwamba, sheria ya Miss Tanzania si kama sheria za nchi.
“Kwanza nataka kukwambia kwamba, sheria za mashindano haya si kama sheria za nchi. Sisi ikitokea baba Mwingereza, mama Mwingereza, wakaja nchini na kuzaa. Mtoto akifikisha miaka 18 akaamua kuukana uraia wa wazazi wake, anaruhusiwa kushiriki hata kama ni Mzungu.
Miss tanzania 2014, Lilian Kamazima  akifanya yake.
KAULI YA BASATA
Baada ya kauli ya Lilian na Lundenga, Amani lilimtafuta Afisa Mawasiliano wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Aristides Kwizera ambaye alisema baada ya Sitti kuvua taji na Lilian kushika usukani biashara imekwisha.
“Kaka, Sitti kavua taji, sasa analo Lilian Kamazima, mchezo umekwisha. Sidhani kama kuna lingine tena hapo.”
Amani: “Vipi kuhusu Sitti, hakuna hatua zozote za kuchukuliwa na Basata?”
Kwizera: “Hamna. Unajua Basata huwa haimgandi msanii, yenyewe kukitokea tatizo inashughulika na aliyepewa leseni. Mwenye leseni ya Miss Tanzania ni Lino Argency, kama kuna tatizo wao wanajieleza kwetu si msanii au mrembo.
“Lakini kama kuna lolote kuhusu Sitti basi tusubiri uongozi wa juu wa Basata kama utasema chochote.”
“Kuhusu Lilian na mambo yake mengine mimi sina la kusema lakini najua yuko sawa.”
Lilian Kamazima katika pozi.
ETI HATA MISS TZ NAMBA 3 TATIZO?
Wakati gazeti hili linakwenda mitamboni, kulikuwa na madai kwamba, hata mshindi wa nafasi ya tatu ambaye kwa sasa ni wa pili, Jihan Dimachk eti naye ni tatizo.
Baadhi ya wadau wa urembo wanaomfahamu mrembo huyo wanadai kuwa, ana asili ya nchi ya Yemen ambayo inapatikana kwenye Bara la Asia yenye mji mkuu wake, Sanaa.
Hata hivyo, Lundenga aliporudiwa tena na paparazi wetu ili kuulizwa kuhusu madai hayo hakupokea simu.

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger