Staa wa filamu hapa Bongo mwenye mvuto
wa kipekee, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa kamwe hapendi kuwa
katika uhusiano wa kimapenzi na masharobaro akidai kuwa siku zote ni
pasua kichwa ila anazimikia watu wazima waliomzidi sana umri.
“Masharobaro hawana
nafasi kwangu, kwa sababu hawafikirii maisha kabisa, hata mwanaume
atakayenioa nafikiri atanipita zaidi ya miaka kumi, hapo ndiyo itakuwa
sawa tofauti na hivyo sitaki masharobaro,” alisema Lulu.
LULU: Masharobaro hawana nafasi kwangu, kwa sababu hawafikirii maisha kabisa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment