Aunty Ezekiel, Odama watimuliwa Bongo Muvi

UPEPO mbaya unaendelea kuvuma ndani ya Klabu ya Bongo Movie Unity! Safari hii umewakumba mastaa wakubwa klabuni hapo, Devotha Mbaga, Aunt Ezekiel na Jennifer Kyaka ‘Odama’ ambao wanadaiwa kutimuliwa kundini kwa sababu ya kujiweka karibu na mwenyekiti wa klabu hiyo aliyejiuzulu, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichozama katika kikao kilichofanyika juzikati, uongozi ambao ulibaki madarakani kundini baada ya Steve kujiuzulu, ulifanya tathmini upya ya memba waliobaki kisha kuwachuja hadi kubaki na wasanii 20 pekee wenye sifa.

“Wamewaengua baadhi ya wasanii ambao wameona hawana sifa ya kubaki kundini, miongoni mwao ni Devotha, Aunt na Odama. Wamesema wanahitaji mastaa wenye msimamo siyo kujipendekeza upande wa Steve, siku si nyingi watayaanika majina ya wenye sifa za kubaki kundini,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ‘ubuyu’ kuwa, wasanii walioenguliwa ni wanachama hai lakini si wanachama wenye msimamo na baadhi yao wameonesha udhaifu wa kuwa karibu na Steve Nyerere ambaye sasa anafanya harakati zake peke yake.

Staa wa sinema Bongo, Aunt Ezekiel
Staa wa sinema Bongo, Aunt Ezekiel

Baada ya habari hizo kutua katika rada ya Ijumaa, mapaparazi wetu waliwaendea hewani mastaa hao wakubwa waliodaiwa kufukuzwa, mambo yalikuwa hivi:

Devotha: Mimi ndiyo kwanza nakusikia wewe siku zote nipo nyumbani sijui hata habari za kikao hicho na sielewi wameniengua vipi wakati mimi ni mwanachama hai na ni miongoni mwa waanzilishi toka tulipokuwa watu saba, lakini kama wameamua hivyo sawa kwani siyo kwamba ukitoka ndiyo mwisho wa maisha.
Odama
Odama

Odama: Hakuna kitu kama hicho, wanaoenguliwa ni viongozi siyo wanachama, watanienguaje bila kunipa taarifa? Kwanza ndiyo nasikia sijui chochote ndiyo napata taarifa kutoka kwako.
Kwa upande wa Aunt Ezekiel, simu yake iliita bila kupokelewa.

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger