Mama anapomaliza first trimester (miezi 3 ya mwanzo) tumbo
linaongezeka ukubwa kutokana na ukuaji wa mtoto. Ukuaji wa mtoto
unadhiri pisition ya ulalaji wa mama,hivyo mama anashauriwa mimba
ikifika miezi 4 (wiki 16)asilalie tumbo au mgongo.
MAMA ASILALIE TUMBO AU MGONGO
Kulalia mgongo sio vizuri kwa sababu uzito wa mtoto unazuia baadhi
ya mishipa ya mgongoni inayosafirisha damu toka kwenye uti wa mgongo
kwenda kichwani,na kutoka miguuni kuja kichwani kushindwa kusafirisha
damu vizuri na kunabadili mfumo wa mzunguko wa damu unaoweza
kumuadhiri mama au mtoto.
PICHA
INAONYESHA MAMA AKILALIA TUMBO ,JINSI MTOTO ANAVYOLALA VIBAYA ,NA
PICHA YA PILI MTOTO ANAJISIKIA VIZURI MAMA ANAPOLALIA UPANDE WA KUSHOTO.
Adhari atakazo zipata mama mjamzito atakapo lala kwa mgongo (chali) / kulalia tumbo
Kutokana na damu kushindwa kusafirishwa vizuri inapelekea kumsababishia mama mjamzito kupata matatizo kama,
:Kuvimba kwa misuli na inayo ambatana na maumivu (miguu na mikono)
:Kushuka au kupanda kwa blood pressure
:Ini kuelemewa uzito
:Kupunguza mzunguko wa damu ambayo ni hatari kwa uhai wa mtoto
:Kusikia kizunguzungu mara kwa mara
:Mama kupata kiungulio mara kwa mara nyakati za usiku
:Kukoroma
:Maumivu ya mgongo
:Mama na mtoto ushindwa kupumua vizuri kwa kusosa hewa (oxygen)
:Mtoto kukosa virutubisho vya kutosha.
Mama anatakiwa alalie position gani ili awe salama?
Tafiti nyingi zinamshauri kwamba mama mjamzito alalie upande wa
kushoto .Sababu damu husafirishwa kwa Urahisi zaidi kutoka kwenye moyo
wa mama na kwenda kwenye kondo la mtoto na kumpa virutubisho vingi
zaidi. .
Iwapo mama atalalia tumbo au mgongo ifamfanya mtoto asiwecomfortable
atahangaika na kumpiga piga mama ili abadili position ya kulala.
USHAURI
Mama anapolala ni vizuri akaweka mto katikati ya miguu usibane miguu
ipitanishe, inakusaidia kulala comfortable,damu kusafirishwa vizuri na
kutopata maumivu ya mgongo.Nyakati za usiku ni kawaida kwa watoto
kupiga piga tumboni ,ila akipiga sana jua umelala vibaya anataka
ubadilishe position.
0 comments:
Post a Comment