Kupata mtoto wa kiume ni jambo linalohitaji ushirikiano wa
pande zote mbili, yaani mke na mume na ni jambo linalohitaji hatua kwa hatua na
kwa umakini, ingawa njia nitakayoeleza hapa haimaanishi kuwa inaweza kufanya
kazi kwa asilimia 100. Bali ni njia
ambayo imekuwa ikitumika mara kwa mara na ndiyo njia rahisi na ukiifuata unaweza ukapata kwa asilimia 75.
Mwaka 1960 mwanasayansi Landrum Shettles aliandika kitabu
kinachohusu uchaguzi wa jinsi ya mtoto.
Mwanasayansi huyo wa tiba ndiye aliyeileta nadharia yake iliyojikita
zaidi katika vitu vilivyomo ndani ya seli, yaani malighafi za kijenetiki
ziitwazo chromosomes ambayo ndiyo inayotumika na kama ikifuatwa vizuri basi
huweza kuwa na mafanikio.
Sayansi ya kijenetiki inaeleza kuwa mwanamke huwa na mbegu
ya XX na ya kiume huwa na XY, na pale yai la kike linaporutubishwa hutokea
mgawanyiko wa seli na mbadilishano wa malighafi za kijenetiki hutokea.
Hivyo kiumbe kinachotungwa yaani mtoto, huwa na nusu ya
malighafi za kijenetiki kutoka kwa mama na nusu nyingine kutoka kwa baba, na
akipata mbegu XX huwa ni jinsi ya kike na akipata XY ni wa kiume.
Kiasilia mbegu Y huwa ni ndogo kimaumbo, zina mwendokasi
mkubwa lakini hufa mapema ukilinganisha na za kike X ni kubwa, hazina kasi,
lakini huishi kwa muda mrefu. Kwa
kutumia ufahamu huu ndipo mwanasayansi Shettels aliweka nadharia ambazo
zinatumika katika uchaguzi wa jinsia.
Kuna hatua tano za kufuata kwa umakini ili uweze kufanikiwa,
ingawa haimaanishi kuwa ni lazima ufanikiwe kwani hatua hizi huongeza nafasi
zaidi ya kupata jinsi ya kiume na kwa yule atakayehitaji jinsi ya kike afanye
kinyume cha hatua hizi.
Hatua ya kwanza
Hatua ya kwanza ni kugundua wakati wa ovulation, ama siku
ambayo yai la kike linatoka. Hiki ni
kipindi ambacho yai la mwanamke lipo tayari kurutubishwa na mbegu ya kiume
hivyo mimba huweza kutungishwa.
Ili kugundua kuwa upo katika ovulation, inabidi kufuatilia
yafuatayo: Inabidi uwe na chati ya kuangalia na kufuatilia ute wa kizazi
unaotoka ukeni, maana muda mfupi kabla ya ovulation ute huwa wa majimaji na wa
kuvutika hufanana kama vile wa mayai
ya kawaida, nikimaanisha ya kuku, ambayo yamezoeleka kwa wengi.
Ni vizuri kupanga chati hii kwa zaidi ya miezi mitatu ili
kusudi uwe na uzoefu wa kugundua tofauti ya ute. Vilevile inabidi uwe na chati ya kuweka
rekodi ya joto la chini la mwili wakati ukiwa umepumzika, nikiwa na maana mara
nyingi ukiwa umelala.
Joto la chini la mwili hupanda kwa nyuzi joto 0.5 sentigredi
kipindi cha ovulation. Ni vizuri chati
hii iwe pamoja na ya ute wa kizazi, kusudi uweze kufuatilia mabadiliko haya kwa
pamoja.
Kipimo cha kugundua ovulation ni kipimo ambacho huangalia
wingi wa homoni aina ya Lutenizing ambayo hutolewa kwa wingi kipindi hiki. Kipimo hiki ni vizuri kufanya mara mbili kwa
siku, kati ya saa 5:00 asubuhi na saa 9:00 mchana. Vilevile kati ya saa 11:00 jioni na saa 4:00
usiku.
Hatua ya pili
Hii ni hatua ya kutegea wakati muafaka wa kufanya tendo la
ndoa. Ni vizuri kufanya tendo la ndoa
kipindi cha saa 24 kabla ya ovulation na saa 12 baada ya ovulation. Kwa sababu tindikali na utelezi katika ute wa
kizazi hupungua na hivyo husaidia mbegu za mwanaume hasa aina ya Y kusafiri
haraka na kulifikia yai la mwanamke na kulirutubisha.
Hatua ya tatu
Pendelea mtindo au staili inayofanywa na wanyama kama mbuzi
wakati wa tendo la ndoa, yaani mtindo wa mwenza wako kuinama.
Mtindo huu huwezesha mlango wa uzazi kuwa karibu na sehemu
ya kiume pia kuingia umbali mrefu zaidi ndani ya uke, hivyo basi mbegu za kiume
humwagwa karibu na shingo ya kizazi na kulifikia yai haraka zaidi.
Hatua ya nne
Ni muhimu mwanamke kufika kileleni kabla ya mwanaume; kufika
kileleni kwa mwanamke husaidia kubadili mazingira katika uke kuwa ya ukakasi
(alkaline) hivyo kusaidia mbegu za kiume “Y” kuwa imara zaidi. Uke kuwa na tindikali huipunguza uimara wa
mbegu ya kiume.
Hatua ya tano
Hii ni kwa upande wa mwanaume. Ni vizuri kuvaa nguo zisizoweka joto kali na
kubana. Unapaswa kuvaa chupi au nguo
ambazo hupwaya na zimetengenezwa kwa pamba.
Nguo za ndani zinazobana ambazo huongeza joto hupunguza idadi ya mbegu
za kiume. Joto pia hupunguza ubora na
utengenezaji wa mbegu za kiume.
Vilevile inabidi kunywa vinywaji vyenye caffeine kabla ya
tendo la ndoa. Hii huongeza nguvu ya
mbegu za kiume aina Y.
Mambo mengine ya kuzingatia ni mlo. Hakikisha unakula vizuri wiki moja kabla na
siku ya tendo. Tafiti zinaonyesha kuwa
ulaji wa vyakula vyenye sukari huiwezesha mbegu ya Y kuimarika zaidi na
kuongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume.
Vyakula hivi ni kama matunda matamu, vyakula vya wanga na vinywaji
vyenye glukosi.
Vyakula vingine ni kama vile nyama nyekundu, mayai, maziwa,
vyakula vya baharini kama vile samaki, kamba na pweza.
Kwa upande wa mwanamke, anapaswa kula zaidi vyakula visivyo
na tindikali kama vile kuepuka kula matunda yenye uchachu na vyakula jamii ya
kunde kupitia kiasi.
Mambo mengine ni kuzingatia mazingira ya tendo lenyewe,
hakikisha upo vizuri kiafya, kimwili na kiakili. Usiwe na msongo wa mawazo na sonona kwa
sababu huleta mwingiliano na tendo, hivyo kulifanya kuwa dhaifu.
Ni vyema pia kutafuta mazingira mazuri ya kufanyika kwa
tendo lenyewe. Lengo ni kuwa na utulivu
wa kimwili na kiakili pia. Hii
itakuepusha pia na usumbufu utakaoweza kuleta mwingiliano na tendo lenyewe.
0 comments:
Post a Comment