Mungu anaposema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa hamaanishi
maarifa ya kutengeneza au kuendesha ndege, ni maarifa ya kawaida tu
katika maisha yetu ya kila siku ambayo yanaweza kubadilisha afya na
ustawi wetu. Moja ya mmea ambao umependelewa sana na Mungu kwakuwa na
viinilishe vingi na mhimu sana kwa afya ya binadamu ni kitunguu swaumu.
Kitunguu swaumu ni dawa karibu kwa kila ugonjwa.
Kitunguu swaumu
ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii
hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia,
Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati
hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.
Kitunguu swaumu
kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika
kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika
mapafu, matatizo katika mfumo wa umen'genyaji chakula, na matatizo ya
kuishiwa nguvu.
Historia inaonyesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika nchini
China mwaka 510 kabla ya Kristo na pia vilitumiwa na wanajeshi wa
Ugiriki na Warumi. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini
pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana. Kuna baadhi ya imani
watu wanaamini kitunguu swaumu kina uwezo wa kufukuza hadi wachawi!
hivyo kama unatokewa unapata usingizi wa usioeleweka au unakabwa kabwa
na wachawi hebu jaribu kitunguu swaumu na utuletee mrejesho
Mwaka
1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua
uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha
magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na
kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia.
Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii
hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash).
Huko sokoni tayari nimeviona vitunguu swaumu kutoka China na Afrika
kusini ambavyo vyenyewe huwa vina punje kubwa nene na huwa rahisi
kuvimenya, hata hivyo ili upate faida hizi zote hapa chini naendelea
kukushauri utumie vitunguu swaumu vyetu vinavyolimwa hapa Tanzania kwani
hivyo vya kutoka nje pamoja na kuwa ni rahisi kuvimenya lakini ubora
wake si kama ule wa vitunguu vyetu.
Hakikisha kila mboga
unayopika haikosi kitunguu swaumu ndani yake na ikibidi ukiweke mwishoni
mwishoni unapokaribia kuipuwa mboga yako toka katika moto kwamba
kisiive sana hata kupoteza viinilishe vyake. Kama una friza au friji ya
kawaida unaweza kumenya vitunguu swaumu hata kilo nzima na kuvitwanga
kidogo katika kinu, vifunge vizuri katika bakuli au mfuko wa plastiki na
uvihifadhi katika friza au friji na hivyo kila unapopika unachukuwa tu
na kukitumia ili kuepuka usumbufu wa kukimenya kila siku.
Lakini
ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji
au ukichanganye na mtindi kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika
moto au kuwa kimepikwa.
1. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
2. Kigawanyishe katika punje punje
3. Chukua punje 6
4. Menya punje moja baada ya nyingine
5. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10
6. Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu kila unapoenda kulala. Namna
nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha
mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupenguza
harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu
zilizomo kwenye mtindi.
Katika zoezi hili nimetumia mtindi wa
Tanga freshi na nimeona matokeo mazuri sana ikiwemo ngozi kuendelea
kung'aa na kitambi ni kama kimeisha kabisa kwa siku 7, hivyo siyo lazima
uwe mtindi uliotengeneza nyumbani bali hata huo wa dukani wa Tanga
fresh bado ni mzuri pia (bila shaka Tanga fresh watanipa hela ya soda
kwa kuwapigia promo)!
Fanya hivi kila siku au kila mara unapopata
nafasi na hivyo utakuwa mbali na kuuguwauguwa. Mama mjamzito chini ya
miezi 4 ni vema asitumie, kwa ujumla tu mjamzito uwe makini utakapotumia
kitunguu swaumu kwa namna hii kama wewe ni mjamzito.
Kitunguu swaumu hutibu magonjwa 30
Haya ni baadhi ya magonjwa yaliyothibitika kutibika na yanatibika au kukingika na kitunguu swaumu:
1. Huondoa sumu mwilini
2. Husafisha tumbo
3. Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)
4. Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I
5. Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine
6. Huzuia kuhara damu (Dysentery)
7. Huondoa Gesi tumboni
8. Hutibu msokoto wa tumbo
9. Hutibu Typhoid
10. Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi
11. Hutibu mafua na malaria
12. Hutibu kifua kikuu (ukitumia kitunguu swaumu kesho yake unaweza
kutokwa na makohozi mengi tu ambayo ni ishara kwamba kweli kinatibu
kifua kikuu (TB)
13. Hutibu kipindupindu
14. Hutibu upele
15. Huvunjavunja mawe katika figo
16. Hutibu mba kichwani
17. Huupa nguvu ubongo. Kazi nzuri niliyopenda zaidi katika kitunguu swaumu.
18. Huzuia meno kung'ooka na kutuliza maumivu
19. Huongeza SANA nguvu za kiume pia hutibu uanithi (kushindwa kusimama kabisa uume)
20. Hutibu maumivu ya kichwa
21. Hutibu kizunguzungu
22. Hutibu shinikizo la juu la damu
23. Huzuia saratani/kansa
24. Hutibu maumivu ya jongo/gout
25. Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
26. Huongeza hamu ya kula
27. Huzuia damu kuganda
28. Husaidia kutibu kisukari
29. Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi (ni kweli, na ni moja ya
kazi nyingine ya kitunguu swaumu iliyonishangaza zaidi) pia kinaondoa
msongo wa mawazo/stress na kukufanya uishi miaka mingi
30. Huongeza SANA kinga ya mwili na kwa muda mfupi, kijaribu na ulete majibu
Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida
zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa
(ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa
kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;
Vina uwezo wa
kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha
polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli
nyekundu za damu.
Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini
kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara
ya kisukari.
Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu
hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na
phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo hutolewa baada ya kuvila.
Nini madhara ya vitunguu swaumu?
Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;
1. Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl
methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa
kunywa maziwa, kunywa maji mengi au kutafuna karafuu. Na nimeshuhudia
nikinywa kwenye mtindi hii harufu ni kama haipo kabisa na hata ukijamba
haikutokei ile harufu mbaya sana kama ukinywa vitunguu swaumu katika
maji
2. Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
3. Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha. Ikikutokea kuharisha siku mbili tatu furahi kwani ni njia mojawapo ya mwili kujisafisha
4. Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya
seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa
kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya
upasuaji au mara baada ya kujifungua.
5. Huingiliana katika
utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets,
saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel
blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile
ciproflaxacillin.
6. Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.
Kumbuka kitunguu swaumu kinaweza kuwa na faida nyingi zaidi ya hizi
lakini bado nakushauri utumie kiasi kidogo (punje 6 tu) kila siku kwa
kipindi kirefu wiki 2 au 3 hata mwezi ili uone faida zake zaidi.
Ikikutokea tangu umeanza kutumia kitunguu swaumu kichwa kinauma zaidi
unaweza kupumzika siku mbili hivi na baadaye unaendelea hivyo.
KITUNGUU SWAUMU HUTIBU MAGONJWA 30
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment