Kwa kawaida mtu mwenye afya njema anatakiwa kwenda chooni angalau
mara tatu kwa siku,lakini si ajabu kusikia mtu hajaenda chooni siku tatu
na tunaona ni kawaida sana kwenda chooni mara moja kwa siku.
Tatizo la kukosa choo (Constipation) linatokana na chakula tunachokula kuchelewa kuunguzwa tumboni hivyo kuchukua muda mrefu katika mfumo wa usagaji.
Tatizo hili linasababishwa na mfumo wa chakula kukosa baadhi ya
mahitaji ili kufanya kazi yake ya usagaji. Vitu hivi ni maji na vyakula
vya fiba(Vyakula vyeneye nyuzinyuzi) ambavyo ni muhimu sana kuharakisha
zoezi la usagaji wa chakula tumboni.
Baadhi ya Vitu vinavyosababisha Tatizo la Kukosa Choo:
- Kutokunywa Maji ya Kutosha
- Kutokula vyakula vyenye fiba kama matunda na mboga za majani
- Ulaji wa nyama nyekundu kwa wingi
- Unywaji wa maziwa kupita kiasi
- Kutofanya kaziza kushughulisha mwili na kukosa mazoezi
Vyakula Vinavyosaidia Kutibu Tatizo la Kukusa Choo
-
Tende
Tende zikiwa kavu au kama juisi inasaidia kuondoa tatizo la kukosa choo. Tende zina fiba kwa wingi hivyo kusaidia zoezi la usagaji chakula tumboni. Pia Tende zina kemikali ya sorbitol–aina ya sukari ambayo inatajwa kusaidia usagaji chakula.
-
Maji
Wataaramu wa afya wanashauri kunywa galsi 6 mpaka 8 za maji kila siku( Lita 1-2 kwa siku)
Kama kunywa maji ni ngumu kwako basi jaribu kuweka vipande vya matunda kama ndimu ,limao,tikiti maji na aina nyingine ya matunda.
[Soma: Faida 11 za Kunywa Maji Yenye Ndimu Kila Asubuhi]
-
Kahawa na Vinywaji Vingine vya Moto
Kahawa na vinyaji vingine vya moto husaidia kusukumwa kwa chakula tumboni na kupata choo.
Matumizi ya muda mrefu ya kahawa yanaweza pia yakaongezea tatizo. Kama unatumia kahawa kwa wingi unashauriwa kunywa maji mengi pia,vinginevyo itaongezea tatizo la kukosa choo
-
Ulaji wa Matunda au Saladi
Matunda yanasaidi kutibu tatizo la kukosa choo kwa vile yana fiba kwa wingi. Lakini matunda yanasaidia kuongeza maji maji hasa matunda kama matikiti.
Pia ulaji wa matunda ni muhimu kuzingatia muda wa kula, ni vyema kula matunda saa moja au dakika 30 kabla au baada ya chakula. Kula matunda mara baada ya kula kama wengi wanavyofanya ni makosa na kunakukosesha faida zinazotarajiwa.
-
Ulaji wa Mboga za Majani
Mboga za majani kama ilivyo matunda ni chanzo kizuri cha faiba ambazo ni muhimu sana katika usagazi na usukumaji wa chakula.
Mchicha, Spinachi,karoti na mboga mboga nyingine ni muhimu kuwepo katika chakula cha kila siku.
Maharage na aina nyingine za kunde kunde pia zina fiba kwa wingi na zinasaidia kupunguza tatizo.
Mazoezi Husaidia Kutibu Tatizo la Kukosa Choo Pia:
Ukiachia vyakula,ufanyaji mazoezi au kazi zinazoshughulisha mwili zinazaidia kuzuia na kutibu tatizo la kukosa choo.Kufanya mazoezi kila siku angalau kwa dakika 30 ni jambo linalowezekana kama utalipa muda na kuweka katika ratiba zako.
Mazoezi rahisi kabisa ni kukimbia (jogging) na pia hushughulisha mwili mzima(Total Body Exercise).
Ukiachia kutibu tatizo la kukosa choo pia mazoezi yanasaidia kuzuia magonjwa mengine mengi kama presha na kisukari.
Kama unasumbuliwa na tatizo la kukosa choo au unamfahamu mtu mwenye shida hii basi mshilikishe na ajaribu kufuta maelekezo kama yalivyotolewa hapa ili kuweza kutibi tatizo la kukosa choo kwa kupangilia vyakula tu unavyokula kila siku.
Tafadhari changia mada hii kwa kuandika katika kisanduku cha maoni. Kama una swali kuhusiana na mada hii usisite kuuliza kwa kuandika katika kisanduku cha maoni hapa chini.
Asanteni na nawatakieni afya nje
0 comments:
Post a Comment