Kutengeneza bajeti ya nyumbani inaweza kuwa ni mawazo kutisha kwa watu wengi. Watu wengi huangalia bajeti ya nyumbani kama kitu ambacho huzuia kufanya mambo yao. Katika hali halisi bajeti ni chombo ambacho kitakusaidia kukuongoza wewe kifedha katika kufanya manunuzi na mambo mengine ya kimaendeleo yanayohitaji fedha.
Mojawapo ya mambo muhimu kwa ustawi wako wa kifedha katika familia ni kuweza kutengeneza bajeti na kufuata.
Watalamu wa falsafa za mipango wamesema “Usipopanga basi unapanga kushindwa” . Ili uweze kupima mafanikio yako basi sharti uwe umepanga nini ufanye kwanza.
Zifuatazo ni faida utakazozipata kwa kuwa na bajeti ya ndani:
Faida 5 za Kutengeneza Bajeti ya Nyumbani
1. Udhibiti wa fedha zako kwanza
Udhibiti wa fedha zako na za familia ni kitu muhimu sana. Ukijua kiasi gani cha fedha unaingiza na kiasi gani unatoa itakusaidia sana kufanya maamuzi sahihi juu ya fedha zako.Badala ya kuelekeza nguvu juu ya jinsi ya kutengeneza pesa zaidi, unaweza kupunguza matumizi yako yako.Kuwa na bajeti kutakuonyesha unatumia fedha kwenye vitu gani na hivyo itakusaidia kujua wapi upunguze hivyo kukupa uwezo wa kufanya maamuzi bora.
2. Tengeneza mpango fedha(“Financial Plan”)
Hakuna mtu anataka kufanya kazi sikuzote za maisha yake . Bajeti itakusaidia kuanza kutengeneza Mpango Fedha , ili uweze kuhakikisha kwamba unafikia malengo yako ya kifedha. Tunafanya kazi kwa wastani wa miaka 35-40 ya maisha yetu, hivyo kwa nini tusifanye fedha zetu sisifanye kazi kwa ajili yetu badala ya kuzitumia kwa matumizi ambayo si ya msingi sana na kutufanya tuwe masikini daima?.3. Itakupunguzia msongo wa mawazo
Kama unajua wapi fedha yako inakwenda kila mwezi , utakuwa hutakuwa na shida juu ya kutumia fedha au hata kutokuwa nazo za kutosha.Mara baada ya kuwa na uelewa mzuri wa hali yako ya kifedha na kuanza kufanya baadhi ya mabadiliko , hutasumbuka sana juu ya kipato chako cha kila mwezi.
4. Ishi kwa kipato chako
Kumbuka bajeti inatuambia nini tunaweza kumudu kununua , lakini haiwezi kukuzuia kununua. Hivyo kama hufuati haifanyi kazi, unahitaji kuiheshimu na kuifuata.Unapojua nini unamudu katika mwezi inakufanya uanze kuishi kwa kipato chako na hivyo kuishi bila madeni.
5. Kugundua nini ni muhimu
Unapoweza kuona fedha inayoingia na kutoka kila mwezi ,unaweza kuanza kuona kwamba baadhi ya mambo si muhimu sana na hivyo itakupunguzia msongo wa mawazo juu ya wapi upate fedha ya ziada kama vile kuazima au kufanya kazi masaa mengi zaidi ambayo mwishowe itakuweka mbali na familia na kuhatarisha afya yakoFahamu kwamba kutengeneza bajeti ya familia inaweza kuchukua muda mrefu . Lakini mara ukianza utaona jinsi hali yako ya kifedha inavyoboreka .
Kuna sababu nyingi za kutengeneza bajeti zaidi ya zilizosemwa. Kama hujaanza,unasubiri nini? Anza leo na uone faida zake kwako binafsi na kwa familia yako
0 comments:
Post a Comment