Madhara ya Kupongeza Watoto-Kama unafikiri umekuwa ukifanya vyema basi fikiri tena.

pongezi_kwa _mtoto_3
Je wewe ni mzazi au mlezi,au mwalimu? Je unafanyaje mtoto wako au mwanafunzi anapofanya vizuri katika kazi zake? Najua wengi mtampongeza kwa namna tofauti. Maneno kama “wewe ni bora kuliko wote”,”una akili sana” n.k.

Lakini unafahamu madhara ya kupongeza watoto? Ukweli ni kwamba kuna madhara makubwa kwa kutoa pongezi za aina hii kwa watoto kuliko ambavyo unaweza kufikiria. Kuna faida kwa muda mfupi tu na madhara makubwa siku za mbeleni.

Watoto watafurahi sana watakapopongezwa, mfano “hongera sana, umepata “A” hakika wewe ni mtoto mzuri sana” mtihani unaofuata mtoto anapopata alama ”C”,unajua atakachofikiri? atakufa moyo sana na kujiona kwamba “yeye si bora”,”si mtoto mzuri” sababu hakuweza kupata alama “A”.
Atajisikia vibaya na pengine hata kudanganya juu ya matokeo yao kwasababu hatapenda kusikia vinginevyo toka kwa mzazi wake.

Wataalamu wa saikolojia ya watoto wanashauri kupongeza watoto kwa njia tofauti na zile ambazo tunazitumia sana kama nilivyoeleza hapo juu. Badala ya kupongeza matokeo peke yake badala yake tuangalie njia na jitihada walizotumia kufikia matokeo hayo ya mwisho na kutoa maoni yetu inavyofaa.

Njia iliyo bora zaidi kumpongeza mtoto aliyepata alama “A” kwa mfano ingekuwa kumpongeza kwa jinsi alivyosoma kwa muda mrefu na kuuliza maswali kwa walimu na wazazi ambavyo vimefanya kufikia matokeo hayo-“Hongera sana,uliweka muda mwingi sana na umesoma kwa bidii,hakuna nguvu zinazoenda bure,unastahili matokeo haya”.
Kwa kusema hivi unamfanya mtoto aelewe kuwa kumbe mafanikio yanakuja kwa kufanya kazi na wala si kwa bahati mbaya au njia za mkato kama ambavyo kushindwa hakuji kwa bahati mbaya pia.
kupongeza-watoto_kujifunza
Pongezi ziendane nakuainisha juhudi na njia zilizopelekea mafanikio
Pale mtoto anapofanya vibaya ni jukumu la mzazi au mwalimu kutoa maoni yake ya kweli kwa mtoto. Sema mfano “unajua kuna wanafunzi wengi darasani kwako ambao wanasoma kwa bidii pia kama wewe,hivyo ili upate matokeo bora zaidi kuliko haya inakupasa kuongeza jitihada ili uwe moja ya kati ya wale wanaofaulu zaidi”.

Usiseme maneno ambayo yamvunja moyo wa kupenda masomo au kazi zake. Kama ambavyo pongezi zinaumiza lawama zina madhara makubwa zaidi. Hivyo tafuta jinsi ya kufanya kwa kipimo au kiasi kinachofaa. Maneno kama “wewe ni mjinga wa kwanza,unaniabisha sana” au “wewe huwezi kufanya sayansi” yanashusha kujiamini na uwezekano ni kuwa mtoto ataendelea kufanya vibaya.
kupongeza-watoto_lawama
Lawama pekee bila kuonyesha njia ya kuondokana na kushidwa hupelekea mtoto kushindwa zaidi

Ujumbe mkuu hapa ni kuwa pongeza kwa jinsi ambavyo mtoto ataelewa kuwa amefanikiwa kwa sababu alifanya kitu fulani. Kuwa matoke mazuri yanatokana na kufanya baadhi ya mambo kama kusoma kwa bidii,kufanya majaribio mengi,ushirikiano na wanafunzi wengine n.k.
Hiyo italeta maendeleo endelevu na pale atakapo anguka atajua hakufanya yale yanayostahili kuleta matokeo mazuri.

Nakutakieni malezi mema!!!.

Tafadhari toa maoni yako hapa chini,shiriki nasi yale ambayo umekuwa ukifanya kwa watoto wako katika kupongeza na kushauri pale wanapofeli katika kazi.

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger