Pia, Rais Magufuli amewaomba wana-CCM kumuombea ili awe na uvumilivu kama wa mtangulizi wake, Jakaya Kikwete katika kukabiliana na utovu wa nidhamu kwenye chama.
Alisema hayo kwenye hotuba yake ya shukrani baada ya kupata kura zote 2,398, katika uchaguzi uliokuwa wa mgombea mmoja wa nafasi ya mwenyekiti wa CCM uliofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa chama hicho uliopo mjini hapa.
Mwenyekiti huyo mpya alisema utendaji kazi ni suala muhimu, hivyo atajenga chama madhubuti ili kiweze kuisimamia Serikali.
0 comments:
Post a Comment