Kocha Julio anbaye yupo Dar es Salaam na timu yake ya Mwadui inayofanyia mazoezi kwenye Viwanja vya Leaders, alisema kwa asilimia 90 amekamilisha usajili, lakini kuna nafasi chache za kujaza.
Kocha huyo aliyeiongoza Mwadui kumaliza nafasi ya tano katika msimu uliopita, alisema yupo kwenye mazungumzo na Kimwaga aliyetupiwa virago na Azam.
“Hivi sasa nafanya mazungumzo na Kimwaga nimesikia Azam imemuacha, hivyo naamini kama akikubali kuja huku atarudisha makali na kila mmoja atamshangaa,”alisema Julio.
0 comments:
Post a Comment