UTAFITI: WANAUME HUVUTIWA ZAIDI NA SURA WANAPOTAFUTA MKE LAKINI HUVUTIWA NA UMBO WANAPOTAFUTA MWANAMKE WA "KUCHEZEA"







.Mabinti: Siri imeshafichuka na inavyoonekana wanasayansi tayari wameshafumbua lile fumbo tata la nani mwoaji na nani mbabaishaji tu mtaka uroda.*.Siku nyingine mpenziyo mpya akikuambia kwamba sababu yake kuu ya kukupenda nimiguu yako, macho, kiuno, matiti, umbo namba nane au sababu zingine za kiumbo, kuna uwezekano mkubwa kwamba huyo njemba si mwoaji bali ni mtafuta uroda tu.*.Utafiti mpyauliofanywa katika Chuo Kikuu cha Texas, Austin unaonyesha kwamba wanaume hutumia vigezo tofauti wanapotafuta mwenzi.*.Kama lengo ni kutafuta mwenzi wa kudumu (mf. mke) basi wanaume wengi hupendelea wanawake wenye sura nzuri lakini kama lengo ni uhusiano wa muda mfupi tu (mf. kutimiza tamaa za ngono za muda mfupi) basi wanaume wengi hutafuta wanawake wenye maumbo mazuri wayatamaniyo.*.Watafiti hawa wamegundua kwamba, japo umbo ni muhimu kidogo katika mahusiano ya muda mrefu, uso ni muhimu zaidi kwa sababu ndicho kiashiria kizuri cha umri na “rutuba” ya mwanamke.*.Swali:Kuna ukweli wo wote katika utafiti huu?Kinachonishangaza mimi ni kwamba suala la tabiaya mwanamke - na hataNoeclexis-halitajwikabisa katika utafiti huu, jambo ambalo nafikiri lilikuwa (na pengine bado) ni la muhimu katika jamii nyingi za Kiafrika.

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger