akizungumzuia
kuhusu matamshi aliyasema Dk.Slaa kwamba haongei na waziri mkuu
mstaafu,Sumaye,mama rose kamili alisema kuwa wiki tatu zilizopita waziri
mkuu huyo mstaafu aliomba namba za dk.slaa akampatia wakaongea vizuri
bila shida yoyote ila anamshangaa juzi aliposema mbele ya waandishi wa
habari kwamba hazungumzi na sumaye.
akizungumzia kuhusu kuja kwa
lowassa chadema mama huyo alisema kuwa Dk.slaa alikuwepo katika
kumkaribisha waziri mkuu mstaafu,Edward Lowassa kujiunga na chama hicho
ni jambo la kushangaza akizungumza kwamba hakushiriki na pia wakati
chokochoko hizo za kustaafu ukatibu wake alisema kuwa viongozi
waandamizi wa chama cha mapinduzi walimfuata na kumshawishi kutoludi
kwenye ukatibu mkuu wake huo atapewa ubunge wa kuteuliwa na rais
atakayeapishwa na kupewa uwaziri katika serikali ya awamu ya tano.
Kamili
alimaliza kwa kutoa rai kwa watanzania wote nchini kutomsikiliza
Dk.Wilbrod Slaa na kuwasihi kuendelea kuwa na matumaini na mgombea wa
urais wa Chadema,Edward Lowassa aliyesimamishwa na chama chao pamoja na
umoja wa katiba ya wananchi (Ukawa) ili kukiondoa madarakani chama
tawala.
Linus Slaa.
Emiliana Slaa.
Mama Rose Kamili akizungumza kwa hisia kali.kushoto ni mtoto wake aliyezaa na Dk.Slaa aitwaye,Emiliana Slaa.
Mama Rose Kamili akizungumza kwa hisia kali.kulia ni mtoto wake, Linus Slaa.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini leo
Mbunge
wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Rose Kamili,
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya mume
wake Dk.Wilbrod Slaa kuzungumza wakati akiwa Katibu mkuu wa chadema
familia yake ilikula kwa shida kwa sababu ya kujenga chama hicho jambo
ambalo si la kweli. Wengineo ni watoto wake, Linus Slaa (kulia) na
Emiliana Slaa.
Mke Halali wa DR SLAA Ajitokeza Akiwa na Watoto Halali wa Slaa na Kumchana Slaa na Kudai Ametumwa na CCM
Mbunge wa Viti Maalumu
kupitia chadema,Rose Kamili,akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam leo jioni kuhusiana na tuhuma alizozitoa mume wake kwamba
waliishi kwa maisha ya kula mihogo na familia yake ili kuhakikisha
chadema inastawi na kuimarika jambo ambalo si la kweli walikuwa na
maisha mazuri ya kawaida tu na kusema kuwa Dk.Slaa anapaswa awaombe
radhi wataznzania kwa kufafanisha kula mihogo kuwa ni umaskini na
kuongeza kwa kusema mbona ukienda katika mahoteli makubwa mihogo na
viazi ipo na watu wenye pesa zao wanakula kama kawada.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment