Abubakary Zubeiry achaguliwa rasmi Mufti Mkuu wa Tanzania


Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) jana limemchagua Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania.

Katika uchaguzi huo uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Africa Dream mjini Dodoma, Tume ya Dini ya Kiislamu imemchagua Sheikh Zubeiry kwa kura 310 za ndiyo baada ya kuingia kwenye uchaguzi huo akiwa mgombea pekee.

Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Alhaji Habib Ndassiwa alisema majina mawili yaliyotoka kwenye Baraza la Ulamaa yalikuwa ni ya Sheikh Ally Muhidini Mkoyogole na Sheikh Zubeiry.

Hata hivyo Sheikh Mkoyogole alijitoa na hivyo kumuacha Sheikh Zebeiry kuwa mgombea pekee.

Mufti Zubeiry aliteuliwa kukaimu nafasi hiyo ya juu katika dini ya Kiislamu mnamo Juni 22 mwaka huu baada ya kifo cha Mufti Issa Shaaban Simba kilichotokea katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Alitakiwa kushikilia nafasi hiyo kwa muda wa miezi mitatu (Siku Tisini) hadi Septemba mwaka huu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa kujaza nafasi hiyo

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger