Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Dk. Willibrod Slaa amesema anakwenda Marekani pamoja na familia yake kwa mapumziko.
Hata hivyo, taarifa zinasema Dk. Slaa amekwishandoka nchini kuelekea Marekani pamoja na familia yake tangu jana jioni.
Huku
akiwa Marekani kupumzika na kujiendelea katika kozi fupi katika tasnia
ya Sheria na Lugha, Dk. Slaa amesema nyumba yake itakuwa chini ya ulinzi
wa Jeshi la Polisi.
Akizungumza
katika mahojiano yaliyorushwa leo asubuhi na kituo cha televisheni cha
Azam, mwanasiasa huyo amesema akiwa mapumzikoni Marekani, nyumba yake
itakuwa inalindwa na Jeshi la Polisi kutokana na vitisho ambavyo
amekumbana navyo tangu alipoamua kuachia ngazi Chadema.
“Ninatishiwa maisha, ni lazima nichukue tahadhari….., ninatishiwa kupigwa mawe. Ni kweli ninalindwa na usalama,” amesema Slaa akiwa anahojiwa na mwanahabari nguli, Tido Mhando.
Hata
hivyo, Dk. Slaa ambaye ameshawahi kuwa mbunge wa Karatu mkoani Arusha
amesema anashangazwa na taarifa zinazoenea kuwa amelala katika hoteli ya
kifahari ya Serena jijini Dar es Salaam na kuhoji wakati wa uchaguzi
mkuu, 2010, alilala mahali hapo lakini hakuna aliyehoji.
Kuhusu
gharama alizotumia kufanya mkutano na wanahabari katika hoteli ya
Serena, Dk. Slaa amesema, alipoenda Marekani katika ziara ya kichama,
alizuru majimbo 13 na hakutumia fedha za Chadema bali marafiki zake
ambao hakuwaweka bayana.
Dk.
Slaa amesema licha ya kuwa ng’ambo katika kipindi hiki muhimu kwa
taifa, ataendelea kufuatilia yanayojiri nchini. Ameahidi kurudi kupiga
kura muda ukifika.
Hapo chini Kuna Audio ya Mazungumzo yaliyorushwa leo na Azam Tv wakati akihojiwas na Tido Mhando
Hapo chini Kuna Audio ya Mazungumzo yaliyorushwa leo na Azam Tv wakati akihojiwas na Tido Mhando
0 comments:
Post a Comment