Polisi
nchini imepiga marufuku vikundi vya ulinzi vya vyama vya kisiasa ,
vyenye mwelekeo wa kijeshi kufanya kazi za ulinzi hadharani kwa madai
kuwa vinaingilia majukumu yao.
Onyo
hilo lilitolewa jana na Kamishna wa Polisi–Operesheni na Mfunzo, Paul
Chagonja wakati akizungumza na waaandishi wa habari Makao Makuu ya
Polisi, Dar es Salaam.
Chagonja
alivitaja vikundi hivyo na vyama vyao kwenye mabano kuwa ni Green Guard
(CCM), Red Brigade (Chadema) na Blue Guard (CUF), ambavyo hutumiwa na
vyama vya siasa hususan katika mikutano yao.
Agizo
la Chagonja limekuja ikiwa ni miezi minne baada ya agizo la Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu
kupiga marufuku vikundi hivyo vya vyama vya siasa ambavyo vina muonekano
na muundo wa vyombo vya usalama, kwani ni kinyume cha katiba na sheria
ya nchi.
Alivitaka
vyama hivyo kuhakikisha vinafuata muongozo uliotolewa na Ofisi ya
Msajili wa vyama hivyo na kama vikienda kinyume jeshi litapambana navyo.
IGP
Mangu aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Baraza la
Vyama vya Siasa, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Polisi uliokuwa
ukijadili namna ya kuondoa vikundi hivyo pamoja na namna ya kuboresha
shughuli za uendeshwaji wa vikundi hivyo.
Alisema
vikundi hivyo vipo kinyume cha sheria na kwamba kuendelea kuvimiliki
kwa kisingizio chochote ni uvunjifu wa Katiba ya nchi na sheria ya vyama
siasa, jambo ambalo polisi haliwezi kulivumilia.
“Polisi
imejipanga vizuri kuhakikisha mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa
inafanyika katika hali ya utulivu hadi siku ya uchaguzi,“ alisema
Kamishna Chagonja.
Alisema
katika kipindi cha kuelekea katika kampeni zinazoanza leo ni muhimu
kila mmoja kujiepusha na makosa yanayoweza kupelekea jinai.
Huku akitoa mfano wa makosa hayo ni kubandua picha ya mgombea wa chama fulani kinyume cha sheria.
Kamishna
Changonja aliwakumbusha wagombea kwa nafasi zao kuwaelimisha wafauasi
wao umuhimu wa kuheshimu sheria ili kudumisha amani, usalama na utulivu
katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi.
“Tunatoa
tahadhari kwa wananchi pia kuzingatia sheria zinazowaongozwa ikiwamo
sheria ya vyama vya uchaguzi na miongozo mbalimbali iliyotolewa na
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),” alisema Chagonja.
Akizungumza
hatua hiyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa askari
polisi hawatoshi kulinda mkutano wa watu wengi hivyo wataendelea
kuwatumia kulinda wanachama wao.
Naye
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema katika chama
chao hakuna kikundi kinachoitwa Green Guard kwani hata Katiba ya chama
hicho hakina watu kama hao.
Mkurugenzi
wa uchaguzi wa Chama cha CUF, Shaweji Mketo alisisitiza chama chake
kuendelea kuwatumia, kwa sababu wapo kikatiba na katiba yao ilipitishwa
na Serikali na inatambuliwa na msajili wa vyama vya siasa.
Kwa
mujibu wa Mketo, kauli ya Chagonja ni kutaka wavunje katiba ya chama,
kwani maamuzi ya kuwatumia yalipitishwa na mkutano mkuu, “Tutawatumia
hiyo ya kutukataza haipo, wapo na katiba ya chama iliweka hilo na
msajili wa vyama vya siasa akalipitisha hilo, ina maana hakuona tatizo,
”alisema.
Alifafanua
kuwa Red Guard hawajawahi kusababisha matatizo zaidi ya kulinda amani,
hivyo hawana sababu ya msingi ya kuacha kuwatumia. Mketo alilalama kuwa
kila unapofika uchaguzi kunakuwa na kauli za kukatisha tamaa na
kutishwa, wao hawaogopi kwa sababu wamefuata sheria
Jeshi la Polisi Lapiga Marufuku vikundi vya Ulinzi vya vyama
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment