Staa wa muziki wa mduara, Snura Mushi ameingia katika tuhuma nzito
akidaiwa kutoka kimapenzi na mume wa rafiki yake Halima Yahya ‘Davina’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, kwa kipindi kirefu, Snura amekuwa
akionekana nyakati za usiku akiwa na mume wa Davina, wakati mwingine
mwanaume huyo anaenda nyumbani kwa Snura au wawili hao kuzungumza kwa
muda mrefu ndani ya gari la mwanaume huyo.
Staa wa sinema na muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi.
“Yaani mastaa wa Bongo bwana, wanapenda sana kuchukuliana mabwana.
Huyu Snura anatoka na mume wa mwenzake. Mume wa Davina huwa anakuja
nyumbani kwa Snura mara kwa mara hasa nyakati za usiku.“Wakati mwingine anakuja na gari na kupaki jirani na nyumbani kwa Snura kisha wanakaa kwenye gari kwa saa kibao. Snura anamzunguka rafiki yake, fuatilieni mtaujua ukweli,” kilisema chanzo chetu.
Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Ijumaa Wikienda liliamua kuingia mzigoni kwa kumsaka Snura na alipopatikana, akasomewa tuhuma zake ambapo katika hali ya kushangaza, msanii huyo, alimwaga chozi.
Staa wa Bongo Movies, Halima Yahya ‘Davina’.
Alipomaliza kulia, Snura alianza kufunguka ukweli wa kisa hicho
ambapo alikiri kuwa ni kweli mume wa Davina alikuwa akienda nyumbani
kwake mara kwa mara lakini ilikuwa ni kipindi ambacho Davina na mwanaume
huyo walikuwa wametibuana kiasi cha msanii huyo kufungasha virago vyake
na kutokomea kusikojulikana.“Mimi nilikuwa nahangaika kuwapatanisha kwa sababu walikuwa kwenye mgogoro mkubwa, mumewe akawa ananiomba nimsaidie kumbembeleza Davina arudi wayazungumze na kumaliza matatizo yao ili kuokoa ndoa yao isivunjike.
Ijumaa Wikienda halikuishia hapo, lilimtafuta pia Davina ili kujua kwa upande wake analizungumziaje sakata hilo ambapo msanii huyo alitema nyongo. Hebu msikie:
“Watu wengine hawana kabisa kazi za kufanya, yaani walikuwa wanataka kunigombanisha na shosti wangu lakini wameshindwa. Ni kweli na mimi niliwahi kuletewa taarifa kwamba mume wangu anaonekana nyumbani kwa Snura usiku lakini ilikuwa ni kipindi ambacho nilikuwa kwenye matatizo na mume wangu.
“Kiukweli Snura hawezi kufanya hivyo kwa sababu yeye ndiye aliyepigania ndoa yangu isivunjike. Isitoshe sisi tunaishi kama ndugu, watoto wangu huwa wanaenda kushinda kwake na wakati mwingine huwa namtuma mume wangu akawachukue kwa hiyo hata kama wanamuona kwake, siyo kwa nia mbaya, watu aache uchonganishi,” alisema Davina.
0 comments:
Post a Comment