STAA anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa anatamani aone mastaa wawili ambao wana bifu kali, Wema Sepetu na Kajala Masanja wanamaliza tofauti zao kwani maisha ni mafupi.
Wema na Kajala enzi wakiwa bado mashosti.
Akizungumza na gazeti hili, Aunt alisema kati ya mabifu ambayo
angependa yaishe ni la Wema na Kajala kwani wapo wasanii wamefariki
dunia wakiwa na bifu huku wale waliobaki ambao walikuwa na mabifu nao
wakitamani waamke walau mara moja wamalize tofauti zao lakini
haikuwezekana.“Jamani maisha haya ni mafupi sana na tunatakiwa kujifunza kutoka kwa wenzetu tuliokuwa nao lakini sasa hivi hawapo tena, natamani sana Wema na Kajala wamalize tofauti zao kwani ipo siku watakuja kujuta siku ambayo mmoja wao atakapokuwa hayupo japo siwaombei ila hilo ndilo tamanio langu kuwaona wakizungumza,” alisema Aunt.
0 comments:
Post a Comment