Wastara Azimia Kisa Penzi la Bond

Diva wa filamu nchini, Wastara Juma ambaye kwa sasa anaripotiwa kuwa katika mapenzi na mwigizaji mwenzake, Bond Bin Suleiman anadaiwa kupoteza fahamu mara tu baada ya kupewa taarifa kuwa mpenziwe huyo amepata mtoto wa nne kwa mwanamke mwingine.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Wastara alipenyezewa ubuyu na mpenzi wa zamani wa Bond, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ na kuambiwa kwamba asijishebedue kwani Bond ana mwanamke mwingine ambaye amejifungua mtoto wa nne hivi karibuni.
 
“Tunakushangaa unavyojinadi kuwa Bond ni wako na kumpa zawadi ya keki ya bethidei wakati mwenzako amezaa na mwanamke mmoja baamedi hivi karibuni. Tena si kwamba mtoto huyo ni wa kwanza, ni wa nne,” kilisema chanzo hicho kikimnukuu Aunty.

Chanzo hicho kifunguka kuwa, baada ya kupewa taarifa hizo na Aunty Lulu, alizimia ghafla na kulazwa hospitali.“Wastara alizimia punde tu baada ya kupewa taarifa hizo, nasikia walimkimbiza hospitali, akapewa huduma nasikia kidogo sasa hajambo. Ishu ilikuwa mbaya, Aunty Lulu alimmchana laivu.”

Risasi  lilimtafuta Aunty Lulu ambaye hapo awali alikuwa akilalamikia penzi la kitumwa la kupigwa mara kwa mara na Bond na hata kufikia mahali na kushukuru Mungu kwa kutengana kwao na kumuuliza kama habari hizo zilikuwa na ukweli wowote.
 
“Ni kweli nilimwambia kila kitu Wastara na tulikuwa tumepanga kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa ili kujua kama kweli ni wa Bond.
 
“Mimi niliamua kufunguka baada ya Bond kunitukana na kunitolea maneno mazito, kwani nilichoka, kama amepata presha na kulazwa hilo mimi silijui,” alisema Aunty Lulu.

Kwa upande wake, Wastara naye alikiri kupoteza fahamu na kulazwa hospitalini, lakini akakataa mambo hayo kumtokea kwa sababu ya kusikia taarifa hizo, bali kutokana na kuzidiwa na malaria.
 
“Nimepata nafuu na nimeshatoka hospitali, nilikuwa nimepatwa na homa kali ya malaria, madaktari waliniambia nilikuwa na malaria 10, kwa muda wa wiki mbili nilikuwa naumwa, lakini nikazidiwa kidogo, hivi sasa niko sawa na hapa ndiyo nashuka uwanja wa ndege natokea Mwanza,” alisema.

Mwanahabari wetu alipombana zaidi Wastara kutaka kujua kuzimia kwake kama kulitokana na kupata habari za Bond kuwa na watoto wanne, alisema siyo kweli kwani asingeweza kushangazwa na jambo hilo hasa kwa vile Bond ni mwanaume lijali na pia ana maisha yake ambayo hayamhusu.
 
“Mimi nina maisha yangu, yeye ana maisha yake, sasa jamani mimi nitapatwaje na presha kwa mambo hayo? Labda nikuambie tu kuwa hakuna lolote linaloendelea kati yangu na yeye zaidi ya masuala ya kikazi tu. Ninaomba uelewe hivyo kwa sababu huo ndiyo ukweli,” alisema.

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger