Chama
cha NCCR-Magezi kimesema, vigogo wote waliohusika kutoa na kupokea
mgawo wa fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow wafikishwe mahakamani
akiwamo Mkurugenzi wa VIP Engineering Ltd, James Rugemalira .
Kashfa
hiyo imesababisha Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko madogo ya
baraza lake la Mawaziri kutokana na mawaziri wawili kujiuzulu.
Mawaziri
waliotajwa kwenye sakata hilo ni Profesa Anna Tibaijuka, ambaye alikuwa
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na aliyeingiziwa Sh1.6
bilioni na mwanahisa wa zamani wa Kampuni ya IPTL, James Rugemarila.
Wengine
waliopata mgao huo kutoka kwa Rugemarila na kiasi katika mabano ni
Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge (Sh1.6 bilioni), Mbunge
wa Sengerema (CCM), William Ngeleja (Sh40.4 milioni), aliyewahi kuwa
Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona (Sh40.4 milioni), Mbunge wa
zamani wa Sumbawanga (CCM), Paul Kimiti (Sh40.4 milioni) na aliyekuwa
mjumbe wa Bodi ya Tanesco, Dk Enos Bukuku (Sh161.7 milioni).
Akizungumza
na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe
alisema waliofikishwa mahakamani hadi sasa ni vidagaa lakini na vigogo
mashuhuri wakiendelea kutamba.
“Mpokeaji
na mtoaji wa rushwa wote ni wahalifu na wanatakiwa kufikishwa mbele ya
mahakama ili wajibu tuhuma zinazowakabili…Rugenarila naye ni miongoni
mwa watu wanaotakiwa kufikishwa mahakamani.”
“NCCR
tunataka kujua kwa nini baadhi waliopewa rushwa wamefikishwa mahakamani
lakini watu wengine kama Profesa Tibaijuka, Chenge, Ngeleja, Yona,
Kimiti na wengineo hawafikishwi mahakamani? Wote wanatakiwa kwenda
kujibu tuhuma zao,” alisema Nyambabe
Hata
hivyo, Mkurugenzi wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk
Edward Hoseah alipotafutwa kuzungumzia kauli hiyo ya NCCR alisema, “Sipo
ofisini hivyo nisingependa kulizungumzia hilo.”
Waliofikishwa
mahakamani hadi sasa ni Mhandisi Mkuu wa Mradi wa Umeme Vijijini (Rea),
Theophillo Bwakea na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma, ambao kwa
pamoja wanadaiwa kupokea rushwa ya Sh485.1 milioni.
Wengine
ni Meneja Misamaha ya Kodi wa TRA, Kyabukoba Leonard Mutabingwa,
Mwanasheria Mwandamizi wa Tanesco, Steven Roman Urassa na Mkurugenzi wa
Fedha BoT, Julius Rutta Angello wanaokabiliwa na mashtaka ya kuomba na
kupokea rushwa ya jumla ya Sh1.923 bilioni.
0 comments:
Post a Comment