Nampenda sana boyfriend wa rafiki yangu.


MSAIDIENI HUYU MSICHANA:
  Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 22, nina rafiki yangu ambaye nimesoma naye na ni kama ndugu yangu wa damu kutokana na tulivyo na watu wote wanajua kwamba mimi ni yeye na yeye ni mimi.
Rafiki yangu huyu nimesoma naye kuanzia O-leve, mpaka advance na sasa tupo wote chuo hapa dar  es salaam, kwa kifupu ni urafiki wa damu.

Mwaka jana katikati rafiki yangu huyu alinitambulisha kwa boyfriend wake ambaye ni kaka anayesoma chuo kingine ambacho hakiko mbali na chuo chetu, kwa kweli wanapendana sana na ni kaka mzuri sana ambaye rafiki yangu anajivunia kuwa naye, na kutokana na ukaribu wangu na rafiki yangu, nimekuwa nikiwasiliana sana na shemeji yangu huyu kiasi kwamba naye amekuwa ni mtu wa karibu sana, na muda wowote asipompata rafiki yangu amekuwa akinipigia mimi, na hata mara nyingine tumekuwa tukienda matembezeni watu watatu, yaani mimi rafiki yangu na shemeji, ukaribu nilionao na shemeji yangu huyu umenifanya nianze kumthamini na kumjali hadi naogopa, mara ya kwanza nilidhani ni kwa sababu nampenda rafiki yangu, lakini kwa sasa naona imepitiliza na nimegundua kwamba nampenda huyu kaka na natamani siku nifanye naye mapenzi sababu mimi nipo single kwa sasa kwakuwa nilikorofishana na aliyekuwa mpenzi wangu.

Hali imekuwa mbaya kwani hata sasa naona hata huyu shemeji yangu nae ananipenda lakini hawezi kuniambia, natamani siku aje hostel wakati huyu rafiki yangu hayupo ili alale hapa hapa. 

Kwa kweli nimechanganyikiwa kwa kifupi nahisi kuumwa kwa sababu nina mpenda kupita maelezo sema nahofia kumuumiza rafiki yangu kwani najua siku nikimpindua lazima shemeji amuache rafiki yangu aje kwangu sababu nina shepu ya kumtamanisha mwanaume yoyote.
Naombeni msaada wana jamii.

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger