Mahabusu
mmoja Shabani Ramadhani (28), amekutwa amejinyonga katika choo cha
Kituo cha Polisi Ubungo- Urafiki, jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea jana baada ya mahabusu huyo kufikishwa katika kituo hicho juzi akituhumiwa kufanya tukio la unyang’anyi.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Augustino Senga, alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa marehemu alijinyonga kwa kutumia
kamba ya kaptura aliyovaa.
Kamanda
Senga alisema marehemu alijinyonga alfajiri katika choo wanachokitumia
mahabusu hao na mwili wake kugundulika nusu saa baadaye.
“Alikwenda
chooni kati ya majira ya saa tisa na saa kumi alfajiri wakati wenzake
wakiwa wamelala na ndiko alikojinyongea kwa kutumia kamba ya kaptura
yake, lakini uchunguzi unaendelea,” alisema Senga.
Mama
mdogo wa marehemu ambaye hakutaka jina lake liandikwe, alisema kuwa
Ramadhani alikamatwa na Polisi Ijumaa iliyopita na kufikishwa katika
kituo hicho akiwa salama.
Alisema
jana walifika katika kituo hicho kwa ajili ya taratibu za kumwekea
dhamana, ndipo walipoelezwa kuwa ndugu yao amefariki dunia kwa
kujinyonga na kamba.
“Sisi
wenyewe tunashangaa iweje kajinyonga wakati tunavyofahamu mtuhumiwa
anapofikishwa polisi anatolewa vitu vyote alivyonavyo na kuingizwa
mahabusu?,” alihoji mama huyo.
0 comments:
Post a Comment