Msichana mrembo ambaye jina lake halikuweza
kufahamika mara moja, hivi karibuni aliponea chupuchupu kubakwa baada ya
kuzidiwa na kilevi na kuangukia mikononi mwa wanaume wakware.
Mrembo ( jina halikufahamika mara moja) akiwa hoi baada ya kufakamia pombe kwa wingi.
Tukio hilo lilijiri mjini Iringa kwenye Uwanja wa Samora kulikokuwa
na Tamasha la Fiesta ambapo awali msichana huyo alionekana akicheza
kihasara kwa kujigalagaza chini na mzuka ulipomuishia, alijikokota hadi
pembeni akiwa hana nguvu, kitendo kilichowafanya wanaume wasio
wastaarabu kumzingira.
Walinzi wakimsaidia mrembo aliyenusurika kubakwa.
Hata hivyo, walinzi waliokuwa eneo hilo walitumia nguvu ya ziada
kumuokoa mrembo huyo kutoka kwa midume hiyo iliyokuwa imepania
kumkomesha.
0 comments:
Post a Comment