Wakati
wa Vurugu za Asubuhi leo Bungeni, Spika wa Bunge alimtaka
Mwenyekiti wa PAC, Mh Zitto Kabwe aende kusoma taarifa ya kamati
yake….
Unajua ni kwa nini? Zitto Kabwe mwenyewe amekwisha lijibu hilo swali kupitia ukurasa wake wa Facebook.
“Kwa nini sikwenda kusoma taarifa ya PAC leo nilipoitwa na Spika? Jibu rahisi kabisa, siwezi kuona madhila na uvunjifu mkubwa wa HAKI za binadamu nikaendelea na mambo kama hakuna kilichotokea.Kitendo cha polisi kutumia nguvu, kupiga raia hovyo na kumdhalilisha kiongozi wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ni kitendo cha kulaaniwa kwa nguvu zote”- Zitto Kabwe
0 comments:
Post a Comment