“Bora niwe Fundi Nguo ili Niwaepuke ‘Masnichi’ Waliopo Bongo Movie”- Wolper

Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe ‘Wolper’ ameamua kuanika ukweli kuwa sasa hivi anataka kuwa fundi wa kushona nguo ili kuepukana na ‘masnichi’ waliopo kwenye tasnia ya uigizaji.

Jack Wolper
Jack Wolper

Akizungumza na Gpl, Wolper alisema ameamua kujikita huko kwa sababu ameona Bongo Movie hakuna maendeleo zaidi ya umbeya na hata soko la filamu linazidi kushuka.

“Mimi ni msanii wa muda mrefu sana na kwa kazi ambazo tayari nimeshazifanya tangu kipindi hicho mpaka sasa naona tasnia haina maendeleo bali wamejaa masnichi tu yaani umbeyaumbeya tu.”


“Ni bora niwe fundi nguo ili kuepukana na manenomaneno yanayoendelea na mpaka sasa hivi tayari nimeshaanza kujifunza kushona nguo na nina imani nitakuwa fundi mzuri tu kuliko kutegemea kazi ambayo haina masilahi,” alisema

0 comments:

 

LIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA. Just Click Like Button Below...

Powered By OnlineBlogger