SERIKALI imesema Tanzania haina sheria ya kuwaruhusu wafungwa kukutana faragha na wenzao wao.
Hii
ni mara ya tatu kwa serikali kutoa majibu hayo, kutokana na maswali ya
wabunge ambapo mara kadhaa swali hilo limekuwa likiulizwa na Mbunge wa
Viti Maalumu, Maryam Salum Msabaha (Chadema).
Hata
hivyo, jana Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima
alikiri kwa Tanzania kutokuwa na sheria hiyo na akajibu kuwa ujauzito
ambao huwapata wafungwa wanawake, unatokana na wafungwa hao kuupata nje
ya Magereza.
Kauli
hiyo aliitoa jana bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Maalumu,
Rukia Kassim Ahmed (CUF) ambaye alitaka kujua ni kwa namna gani
wafungwa wanawake wanapata ujauzito wanapokuwa ndani ya magereza yao.
Pia,
alihoji kama magerezani kuna usiri, ni kwa namna gani mahabusi ambao ni
mashekhe kutoka Zanzibar wanafanyiwa vitendo vya ulawiti gerezani.
Akijibu
swali hilo, Naibu Waziri huyo alisema jeshi la Magereza lina utaratibu
wa kutenganisha wafungwa wa kiume na wa kike kwani kila watu hutunzwa
kwa sehemu zao na hulindwa na watu wa jinsia zao.
Kuhusu
tuhuma za kulawitiwa kwa mashekhe wa Zanzibar, Waziri wa Mambo ya Ndani
Mathias Chikawe, alisema sakata la Shekhe Salum Ali Salum linafanyiwa
kazi na kwamba kiongozi huyo ameshafanyiwa uchunguzi wa awali katika
Hospitali ya Amana.
“Jambo
hilo lipo mikononi mwetu, tumempeleka Hospitali ya Amana na kesho (leo)
tutampeleka Hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi, lakini
tunachunguza pia tabia ya kiongozi huyo na mwenendo wake kabla ya
kuingia gerezani,” alisema Chikawe.
Hata
hivyo, Chikawe alisema kumekuwa na mkanganyiko mkubwa kwa watuhumiwa
hao, kwani tangu mwanzo hakuwa ameripoti vitendo hivyo, lakini alipofika
mara ya nne gerezani ndipo akaripoti kufanyiwa vitendo hivyo na mmoja
wa polisi.
0 comments:
Post a Comment