Siku chache
baada ya kumwagwa na Wema Isaac Sepetu ‘Beautful Onyinye’, Mbongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amenaswa kwenye mahaba mazito na
msanii, mtangazaji, mjasiriamali, tajiri na mrembo mkali kuliko wote
Afrika Mashariki, Zarinah Hassan a.k.a Zari au Boss Lady.
Mbongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akimhagi msanii mrembo mkali
kuliko wote Afrika Mashariki, Zarinah Hassan a.k.a Zari au Boss Lady.
HABARI YA TAUNIHabari ya ‘mujini’ ilidai kwamba, mahaba ya wawili hao yalianzia safarini walipokutana kwenye ndege moja wiki iliyopita ambapo Diamond alikuwa akitokea nchini Nigeria kupitia Afrika Kusini kisha Dar huku Zari akitokea Afrika Kusini kuelekea Dar kibiashara.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mastaa hao walipokutana kwenye ndege waliungana na kupiga picha za pamoja kisha safari yao ya mahaba niue ikaanzia hapo.
UWANJA WA NDEGE
Chanzo hicho kilimwaga ‘ubuyu’ kwamba, wawili hao walipotua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Diamond alionekana akiwa ‘veri klozi’ na Zari kiasi cha kuibua minong’oni uwanjani hapo kwa namna walivyoonekana wamependezeana.
Chanzo hicho kilimwaga ‘ubuyu’ kwamba, wawili hao walipotua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Diamond alionekana akiwa ‘veri klozi’ na Zari kiasi cha kuibua minong’oni uwanjani hapo kwa namna walivyoonekana wamependezeana.
Diamond Platnumz akipozi na mrembo Zari kimahaba.
KWENYE GARI LA DIAMONDIlisemekana walipofika nje walikwenda moja kwa moja kwenye maegesho ya magari (parking) kisha walizama kwenye ndinga la staa huyo wa Ngoma ya Mdogomdogo ambapo waliongozana hadi hotelini.
WENYEJI WA ZARI
“Boss Lady alifuatwa na wenyeji wake lakini cha kushangaza walishindwa kumpokea kwani baada ya kumuona yuko kwenye mahaba na Diamond nao wakajikata kiaina,” alisema sosi wetu.
HOTELINI UFUKWE WA BAHARI YA HINDI
Mtoa ubuyu wetu huyo aliendelea kunyetisha kwamba, baada ya kutimka airport, siku ya kwanza walilala hoteli moja maarufu jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa sababu maalum) iliyopo kwenye Ufukwe wa Bahari ya Hindi.
‘Diamond Platnumz’ akiwa na mrembop huyo kwenye ‘pipa’.
WASHTUKIWA, WAHAMA HOTELIChanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa Diamond au Dangote, kilizidi kuvujisha kwamba, ilipofika usiku, wawili hao waliamua kuhama kwenye hoteli hiyo kwa madai kwamba walikuwa wameshtukiwa na watu wengi hivyo walihofia kunaswa.Ilisemekana kwamba walihamia hoteli nyingine ambayo nayo ipo pembezoni mwa ufukwe huo.
KOSA LA KIUFUNDI
Katika harakati zao zote, kosa la kiufundi walilofanya ni kujifotoa wakiwa kimahaba ufukweni na kuziachia picha hizo kwenye mitandao ya kijamii huku wakisifiana.
MASHABIKI
Mashabiki wa jamaa huyo kupitia mitandao hiyo, walidai kwamba huenda Diamond mwenye umri wa miaka 26, amefanya hivyo ili kumkomoa Wema ambaye alimtosa Dangote kistaarabu.
Walidai kwamba Zari anaweza kumtangaza zaidi Diamond kimataifa na hasa Uganda tofauti na Wema ambaye angemtangaza Bongo tu.
Mashabiki wa jamaa huyo kupitia mitandao hiyo, walidai kwamba huenda Diamond mwenye umri wa miaka 26, amefanya hivyo ili kumkomoa Wema ambaye alimtosa Dangote kistaarabu.
Walidai kwamba Zari anaweza kumtangaza zaidi Diamond kimataifa na hasa Uganda tofauti na Wema ambaye angemtangaza Bongo tu.
Mrembo Zari au Boss Lady akiteta jambo.
NENO“Diamond mjanja sana. Kenya alizua gumzo na msanii Avri na yule demu wa Malindi, Mombasa na baadaye msanii Victoria Kimani.
NIGERIA
“Kule Nigeria alishakuwa gumzo na akina Davido, Iyanya, Tiwa Savege na Yemi Alade ambaye walikutana Coke Studio Africa jijini Nairobi, Kenya.
NI ZAMU YA UGANDA
“Ishu ilikuwa Uganda lakini sasa ni kama ananawa maana ameshapata ‘kiki’ kupitia Zari,” alisema mmoja wa wachambuzi wa habari za mastaa Bongo.
DIAMOND ANASEMAJE?
Baada ya kunyetishiwa mchongo huo, waandishi wetu walimvutia waya Diamond asubuhi, mchana, jioni na usiku lakini simu haikupokelewa.Zari ni mzawa wa nchini Uganda ingawa ana uraia wa Afrika Kusini ambapo anaishi kwa sasa.
Baada ya kunyetishiwa mchongo huo, waandishi wetu walimvutia waya Diamond asubuhi, mchana, jioni na usiku lakini simu haikupokelewa.Zari ni mzawa wa nchini Uganda ingawa ana uraia wa Afrika Kusini ambapo anaishi kwa sasa.
Mkali Zari akiwa na ndinga yake aina ya Black Chrysler (2008).
UTAJIRI WA ZARIPamoja na uzuri wa umbo na sura ikiaminika kuwa ndiye msanii mrembo mkali Afrika Mashariki, Zari ndiye msanii tajiri wa kike namba moja nchini Uganda kwa kuwa ana utajiri wa kutisha.
Zari ana umri wa miaka 32 (anamzidi Diamond kwa miaka 6), akiwa ni mama wa watoto wawili, aliyeolewa na Ivan Semwanga ambaye mwaka jana ndoa yake ilidaiwa kuingia mdudu japo haijavunjika, hivyo bado ni mke wa mtu.
Zari anaingiza mshiko mrefu akimiliki majumba yanayomwingizia fedha ndefu na magari ya kifahari kama yale ya mastaa wa Kimarekani.
Zari amepata
mafanikio makubwa katika muziki na kipindi chake cha The Boss Lady
kwenye Runinga ya UBC nchini humo, kinachomuingizia mkwanja mrefu
kutokana na matangazo kikifananishwa na kile cha mwanamitindo wa
Marekani, Kim Kardashian cha Keep Up With The Kardashians.
Kwa mujibu wa Jarida la Times la Uganda, huenda Zari akaingia kwenye orodha ya wanawake matajiri zaidi Afrika siku chache zijazo endapo ataendelea kuzichanga.
MAGARIKwa mujibu wa Jarida la Times la Uganda, huenda Zari akaingia kwenye orodha ya wanawake matajiri zaidi Afrika siku chache zijazo endapo ataendelea kuzichanga.
Zari mwenye maskani yake Kampala na Afrika Kusini, anamiliki ndinga kibao za kisasa na zenye thamani kubwa kama BMW (2006) lenye thamani ya dola 47,000 (Sh. milioni 75.2), Black Chrysler (2008) linalouzwa dola 16,000 (Sh. milioni 25.6) na Audi Q7 (2010) linalogharimu dola 53,000 (Sh. milioni 84.8).
Mengine ni Silver Chrysler (2008) lenye thamani ya dola 13,000 (Sh. milioni 20.8), Jetta Volkswagen (2006) linalogharimu dola 27,000 (Sh. milioni 43.2), Mercedes Benz Convertible (2008) linalouzwa dola 26,000 (Sh. milioni 41.6), Range Rover Sport (2010) lenye thamani ya dola 109,000 (Sh. milioni 174.4), Lamborghini Gallardo (2010) linalogharimu dola 198,000 (Sh. milioni 316.8), Hummer H2 la dola 150,000 (Sh. milioni 240) na mengine mengi, yote yakiwa na jina lake badala ya namba za usajili.
Pia Zari anamiliki maduka, hoteli na majumba ya kisasa kwenye miji mikubwa ya Pretoria na Cape Town nchini Afrika Kusini na Kampala, Uganda. Kazi ni kwako Diamond
0 comments:
Post a Comment