“WANANIITA mshamba wa Kimanyema ila poa tu!”Msanii
wa muziki wa kizazi kipya, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amesema baadhi ya
mashabiki wake wanamuita mshamba wa Kimanyema, lakini hilo halimsumbui
na wala halimpi presha.
Nyota huyo anayetamba na wimbo ‘Ndagushima’, amesema hawezi kuacha
kufurahia kupiga picha nyingi iwezekanavyo anavyosafiri nje ya nchi
kwani ni kumbukumbu kwake na pia ni kitu alichokiota kwa muda mrefu.
“Eti wanasema mshamba wa Kimanyema kapata vihela vyake eti
kaenda shopingi, nifanyaje sasa na ni kitu ninachokipenda, sitaacha
kutupia picha nikiwa nje au ndani ya nchi kwa kuwa ni kitu
ninachokipenda na nadhani wengi wanapenda kwani ni sehemu ya kufurahia
maisha,” alisema Ommy Dimpoz.
Msanii huyo amekuwa katika ziara ya wiki mbili sasa katika nchi
mbalimbali ambapo kesho Jumamosi, atatumbuiza katika Ukumbi wa La Bodega
huko Ufaransa baada ya shoo iliyofanyika wiki iliyopita katika mji wa
Rotterdam, Uholanzi.
OMMY DIMPOZ Ang’aka kuitwa mshamba wa Kimanyema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment